T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 13,899
- 47,067
Trump hajawahi kuwa mfanyakazi wa Tyson.Hakuna ajabu yeyote. Mike Tyson amewahi muajiri Trump na kuwa bosi wake. Maisha ni mzunguko.
Kikwete amewahi kuwa Katibu wa Pius Msekwa. Badae Pius Msekwa akaja kuwa Makamu Mwenyekiti CCM, Jakaya Mwenyekiti na Raisi wa nchi. Anachokifanya Trump ni heshima kwa bosi wake wa zamani (Tyson).
Kesho ni fumbo.
Wabongo wengi huwa wanaamini ukilipwa mshahara/consultation fee na mtu basi lazima awe anakuzidi hela na lazima awe boss wako, kumbe sio lazima. Wakati Tyson anamfanya Trump awe mshauri wake wa masuala ya fedha Trump ni mtoto wa kishua na karithi mali za mzee John na anamzidi Tyson hela miaka yote.
Trump alikuwa na tabia ya kujihusisha na celebrities kulingana na biashara zake zilivyokuwa. Watu maarufu wote enzi zile wawe wapiga dili, waigizaji, wasanii na mabondia yeye alikuwa anawakubali.