ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 20,068
- 47,001
- Thread starter
-
- #101
Kwamba Mungu aliweka struggle naHayo mabaya na mema yote yanampa sifa Mungu, Yaani yote yapo ili kumtukuza yeye.
Fikilia unapopitia magumu na alafu unapata msaada katika mazingira usiyotarajia hapo ni lazima utamtukuza Mungu. Lakini je! Lisingekupata hilo gumu ungemtukuza Mungu?
Mungu aliufanya moyo wa farao kua mgumu kama jiwePia ukisoma biblia unaona jinsi Mungu alivyojitukuza katika kuwatoa wana wa Israel kutoka Misri. Hapo utaona jinsi Mungu alivyoufanya moyo wa farao kuwa mgumu ili yeye aweze kujitukuza.
Kwa sifa kuu anayopewa Mungu angeweza kumfanya Simba ale nyasi kama angetaka si ndio?Mkuu ukisema hivyo utataka kusema Simba ale nyasi ili asiwaumize swalaπ.
Fafanua hapa sijakuelewaNature ni lazima ibalance kwa namna yoyote. Pia hakuna jambo baya litakupata endapo wewe haufanyi wala kuwawazia wengine ubaya na hata hilo baya likikupata bhasi Mungu ni lazima atajitukuza kwako. Mfano ni TUNDU LISSU
Hayo mabaya kayaumba nani si Mungu kama unavyosema au?Ubaya kutaradadi sio tatizo la Mungu ni tatizo la mwanadamu kupenda kutenda mabaya, Lakini pia ni tatizo la wanadamu wema kutokukemea mabaya.
umenielewa vibaya. Tunatumia kanuni ya almasi na dhahabu hatuwezi kumuumiza mtu wala kujiumiza sisi maana kwenye misingi yetu kuna HAKI.Kama hiyo falsafa inasema kua mtu kumfanyia jambo la kuumiza mtu mwingine ni sahihi basi sina haja ya kuifatilia
Mimi naamini kujipenda kujijali kujilinda bila kutawanya maumivu kwa watu wengine
Mkuu keep aside God and let's go back to our topic. Siwezi kumtetea Mungu mimi ππ.Kwamba Mungu aliweka struggle na
mambo negative ili apewe sifa
Kwamba bila hayo yote kwenye maisha na mengineo mabaya Mungu asingepewa sifa hii ni maajabu aisee
Farao alikua na nafasi ya kuwaachia wana wa Israel waondoke pasipo kupata yale mapigo, Lakini Farao aliukaza moyo wake na Mungu akaufanya moyo wake kuwa mgumu zaidi ili kwamba kila mtu ajue kwamba aliyefanya vile ni Mungu.Mungu aliufanya moyo wa farao kua mgumu kama jiwe
Then aka ahidi kumchoma moto siku ya mwisho
Kumbuka moyo wa farao ni Mungu mwenyewe aliufanya mgumuππΌππΌ
Kwa sifa kuu anayopewa Mungu angeweza kumfanya Simba ale nyasi kama angetaka si ndio?
Kwahiyo hakuna haja ya kumuwajisha mtu aliekosea ?umenielewa vibaya. Tunatumia kanuni ya almasi na dhahabu hatuwezi kumuumiza mtu wala kujiumiza sisi maana kwenye misingi yetu kuna HAKI.
mtu anapokuja kwa lengo la kutuumiza tunamchukulia kama mtoto mdog asiyejua njema na baya.
YESU KRISTO ameishi falsafa hii ambayo mzizi mkubwa ni upendo unaoanza ndani ya mtu, kujipenda, kupenda wengine.
unajua kinyume cha hofu ni nin? Ni UPENDO.
Na huwezi kweli mkuu we tulia tu π πMkuu keep aside God and let's go back to our topic. Siwezi kumtetea Mungu mimi ππ.
Back to Nature, kwamba nature imeweka mambo mabaya na mambo mema. Kinachofanya mtu atende mambo mema au mabaya ni akili yake mwenyewe wala sio nature.
Kumbuka struggling kwenye maisha sio jambo la asili bali ni laana baada ya Adam kula tunda.
Sijui kama huwa unasoma biblia ila biblia imeweka vyema sana haya mambo.
Farao alikua na nafasi ya kuwaachia wana wa Israel waondoke pasipo kupata yale mapigo, Lakini Farao aliukaza moyo wake na Mungu akaufanya moyo wake kuwa mgumu zaidi ili kwamba kila mtu ajue kwamba aliyefanya vile ni Mungu.
Ni kama hivi leo, Moyo wa CCM ulivyofanywa mgumu Yaani wao wanaona kama hawafanyi makosa na wananchi wamebaki kusubiri neema ya Mungu tuu. Siku CCM ikianguka lazima Mungu atatukuzwa tuu.
Hata leo hii Mungu anaweza kumfanya Simba akala majani lakini Mungu hawezi kutukuzwa bali Simba ndio atapewa sifa za upekee hivyo Mungu hawezi kufanya huo ujinga.
Yaani ili maisha yaende ni lazima jambo zuri na baya litokee at some/same moment. MfanoFafanua hapa sijakuelewa
Mithali 16:4Hayo mabaya kayaumba nani si Mungu kama unavyosema au?
Kwahiyo yeye Jehova hakukujua madhara ya kuumba mabaya?
Hata wanyama wengi wa porini, Paka na Mbwa wako hivyo pia.Hello Great thinkers π«‘
Mwanadamu ana baadhi ya mambo ambayo huwa yanatokea ndani yake bila yeye kuyapanga au kuyachagua kwa makusudi(Unakubaliana na mimi?)
Hayo tunaweza kuyaita Human Nature asili ya mwanadamu
Mfano:
Kupenda : binadamu anaweza kujikuta anampenda mtu au kitu bila hata kupanga kukipenda
Hii ni sehemu ya nature ya mwanadamu
Kutamani: kutamani mtu au kitu, mafanikio maisha bora au kupata zaidi ni jambo ambalo linaweza kutokea naturally ndani ya mwanadamu
Kukosea kwa kawaida hua tunasema kwamba mwanadamu si perfect π―
Ikiwa na maana kukosea haiepukiki
Kukosea ni sehemu ya maisha na ni sehemu ya asili ya mwanadamu
Mimi tangu nazaliwa nimekuta huo msemo
Kuhisi maumivu unapoumizwa, ni natural kuhisi maumivu
Huwezi kila wakati kuamua kwamba sitahisi au sitaumia ni ngumu kudhibiti hisia za maumivu kwa sababu huja natural
Huo ni upande mmoja wa Human Nature ambao tunaweza kuuita positive (chanya)
Lakini vipi π
Human Nature inaweza kuwa negative?
Kwa sababu kama binadamu anaweza kupenda anaweza pia kuchukia
Kwahiyo hapa tutasema chuki nayo ni sehemu ya human Nature?
Anaweza kuwa na wivu
MF: ameona mtu kamzidi kitu fulani akaingiwa na wivu gafla bila kupanga
Anaweza kutamani kitu vitu bila kupanga ni hisia tu zinamjia
Anaweza kukosea
Kuwa m binafsi
Najiuliza je, haya mambo nayo ni sehemu ya human nature?
Ikiwa baadhi ya hisia na impulses zinatokea naturally ndani ya mwanadamu je kuwa na hisia hizo kunamaanisha kwamba lazima uzifanyie kazi?
Yaani uwe selfish kwa wengine...
Uumize wengine pengine kwa sababu una history ya maumivu kwa kisingizio una hisia za maumivu
Uachonganishe watu...
Uchukie watu..
Uwe mtu anayefanya dunia isiwe salama kuishi kwa kisingizio kwamba hii ni human nature na kwamba hizo ni tabia zisizoepukika?
Utasikia kawaida binadamu sisi hatupendani hapo mtu anatafuta kuhalalisha mabaya anayofanya kwa watu wengine
Ex:π
Kuna tabia moja ambayo sisi wanadamu tunayo
Mtu anakosea dhahiri, lakini anapofika kwenye kuomba msamaha hawezi kusema tu
JAMANI imekosea naomba nisamehewe
Badala yake anakimbilia kusema
Mimi ni binadamu, hakuna binadamu mkamilifu
Hii huwa naiona kama ina kiburi fulani ndani yake
Kwa nini usikubali tu kwamba umekosea na uombe radhi, bila kuambatanisha sababu ya kuhalalisha kosa lako?
Kwa maoni yangu binafsi, nakubali kabisa kwamba wakati mwingine kuna hisia zinaweza kukuingia bila hata kupanga
Labda ukapatwa na wivu
Labda ukakasirika
Labda ukahisi chuki
Lakini pamoja na yote hayo, huwezi kuendekeza hizo hisia zako kwa sababu tu zimekuja naturally
Wakati mwingine mtu ana uwezo wa kuzikataa hisia hasi zenye uharibifu, hasa zile ambazo hazina faida kwake wala kwa wengine
Naamini sio kila kitu unachohisi unapaswa kukiweka kwenye akili na kukifanyia kazi mara moja
Kuna tofauti kati ya kuhisi kitu na kuchagua kufanya kitu kwa sababu umehisi
Unaweza kuwa na wivu bila kumdhuru mtu
Unaweza kuwa na hasira bila kumtukana mtu
Unaweza kuumia bila kuamua kuwaumiza wengine
Unaweza kuhisi chuki bila kugeuza chuki hiyo kuwa tabia yako
Mwanadamu yeyote anaweza kuwa mtu mzuri sana bila kuwa kikwazo kwa wengine, pale tu anapojifunza ku.control hisia zake negative na kuchagua kwa busara jinsi ya kuzitendea kazi
Kwa sababu mwisho wa siku, hisia zinaweza kutokea naturally, lakini matendo ni choice
Dunia ingekuwa sehemu nzuri zaidi kama wote tungetumia Human Nature yetu kwa upande wa positive
Karibu kwenye mada
Blue Monday π
ShesRise_1 π€
Nakubaliπ€Na huwezi kweli mkuu we tulia tu π π
Na ndio maana hii mada sijataka iwe upande huo pasingetosha
Mkuu hapa nimejaribu kujadili matukio ya kibinadamu tuu.Huko juu umesema huwezi kumtetea Mungu ukashauri turudi kwenye mada lakini sasa naona bado umerudi huko huko π
Bibilia nasoma sana tu subiri tutaunda mjadala wa kidini tutawekana sawa
Kwa leo acha tuishie hapa π
Yaani umeshahamisha mjadala umeufanya kua wa kidini ujueYaani ili maisha yaende ni lazima jambo zuri na baya litokee at some/same moment. Mfano
-Mti ni lazima upukutishe majani ili ukue.
-Umeme ili uwake ni lazima hasi na chanya ziungane na shoti kidogo itokee.
-Ili gari litembee ni lazima magurudumu yasuguane na lami. Pia ni lazima vyuma viumane na kusukumana ndani ya gear box.
-Pia binadamu tunakufa na wengine wanazaliwa na maisha yanasonga.
-Ili upate pesa ni lazima mwingine iondoke mikononi mwake iwe kwa hiari au kwa lazima.
Haya yote yanatokea katika maisha lakini kwa kiasi kinachostahili, Ndio maana biblia inatufundisha kuwa na kiasi. Usipokuwa na kiasi ukatenda kwa uzuri zaidi utapata matokeo yake lakini pia ukitenda kwa ubaya zaidi utapata matokeo yake.
Henoko alimpendeza sana Mungu, yeye alifanya kila jambo kwa haki mpaka Mungu akamuonea wivu akamchukuaπππ
Farao alitenda kwa ubaya zaidi Mungu akamlipa kwa ubaya wake pamoja na watu wake.
Daudi yeye alibalance mzani, Kuna muda alitenda kwa haki na Kuna muda alifanya ukatili wa kutosha. Mungu akampenda sana Daudi
Pia Sauli ambaye baadae aliitwa mtume Paulo alifanya ukatili mkubwa sana mwanzo wa maisha yake alafu baadae akahubiri habari za Mungu kwa bidii sana. Mungu pia alipendezwa nae
Hivyo nahitimisha kwa kusema nature ni lazima ibalance. Usitende wema tuu, Bali tenda wema panapohitajika wema na ubaya kwa yule unaeona anakufanyia ubaya.
Mithali 16:4
BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.β
Sawa bwana Einstein AKA YodaHata wanyama wengi wa porini, Paka na Mbwa wako hivyo pia.
Kwani simba kula majani na akapewa sifaa za pekee kuna tabu gani πNakubaliπ€
Mkuu hapa nimejaribu kujadili matukio ya kibinadamu tuu.
Mfano hapo ikatokea Simba ameanza kula majani si atapewa sifa za pekee make tuu.
Anyway nakubali tuishie hapa kujadili kuhusu Mungu.
Mkuu refer kauli yangu ya kwanza nilisema nitajibu kwa mtazamo wa kidini. Hivyo huu ni mtazamo wangu tuu pia wengine wana mtazamo wao.Yaani umeshahamisha mjadala umeufanya kua wa kidini ujue
Una hakika kila mtu anaamini hicho kitabu cha biblia?
Sio kwamba sitaki kujibu, HAPANA.Swali langu ni moja tu !
Kwa kua Mungu ni muweza wa yote
Kwanini asinge balance vitu vyote
Bila kuleta mkanganyiko wa maumivu
Hili hutaki kujibu kwanini ?
Ndio maana nimesema ni lazima kubalance mzani usitende mema sanaaaa wala usitende ubaya sanaaa, wewe balance mzani tuu.Hapo kwa Henoko ndio kabisa unazidi kunichosha Mungu alimuonea wivu Henoko aiseee!
Henoko si ni kazi ya Mungu?
ππππ Mkuu kwani anaetenda ubaya na hakutendei wewe Kuna tabu Gani?Kwani simba kula majani na akapewa sifaa za pekee kuna tabu gani π
Ahaaaaaa basi sawa mkuu umeeleweka naona umepania kunishushia upako asubuhi hiii amen amen mtumishiMkuu refer kauli yangu ya kwanza nilisema nitajibu kwa mtazamo wa kidini. Hivyo huu ni mtazamo wangu tuu pia wengine wana mtazamo wao.
Katika huu mtazamo wa kidini ndio umenifanya Mimi naamini kwamba nahitaji kutenda mambo pasipo kumuumiza mwingine lakini ikitokea maumivu yamezidi au nimeshindwa kusamehe bhasi nahitaji kutumia sehemu ya ubaya uliopo ili kubalance natureππ
Sio kwamba sitaki kujibu, HAPANA.
Nikijibu hili swali nitakuwa naingilia majukumu ya Mungu lakini pia nitalazimisha watu wote tuwe sawa kitu ambacho hakiwezekani.
Nikupe mfano mdogo Magufuli alipoingia madarakani aliharibu mifumo ya watu wengi sana, Mimi binafsi nilipoteza mtaji pamoja na biashara haya yalikua ni maumivu, lakini huyo huyo Magufuli aliifanya akili yangu itazame upande mwingine wa maisha, nikajifunza kilimo biashara na fursa ya madini hii kwangu ilikua ni faida kutoka kwa mtu yuleyule.
Hivyo naweza kusema watu wote hatuwezi kuwa sawa lakini pia maumivu yanatufundisha kuwa watu wema na bora zaidi.
Mfano mwingine ni TUNDU LISSU huyu Mzee amepitia maumivu na mateso lakini siku moja Sheria zetu zikibadilishwa haya mambo ya Tundulisu yatabaki kuwa historia tuu.
Ndio maana nimesema ni lazima kubalance mzani usitende mema sanaaaa wala usitende ubaya sanaaa, wewe balance mzani tuu.
Kosa la Henoko lilikua ni kutenda mema sana Mungu akaamua amchukue wakakae wote huko mbinguni.
Binafsi nimejifunza kubalance mzani/kuwa na kiasi ili niweze kuishi hapa duniani kwa amani na maisha marefu Yaani ukinizingua nakuzingua, ukija kwa amani natangaza amani.
Kuna ubaya kwa sababu binafsi sifurahishwi kuona watu wengine wakiumizwa π’ππππ Mkuu kwani anaetenda ubaya na hakutendei wewe Kuna tabu Gani?
Amen, amen barikiwa sana kwa maada mujarabu.Ahaaaaaa basi sawa mkuu umeeleweka naona umepania kunishushia upako asubuhi hiii amen amen mtumishi
Mkuu mimi ukitangaza vita nakupima wewe na vita yako, kama Haina madhara wala maslahi sipotezi nguvu zangu.Hiyo paragraph ya mwisho umesema mtu anavyokuja ndio unampokea
Haya mimi natangaza vita na wewe π jokes π
UNAAKILI NZURI SANA. wabarikiwe wazazi wako.Kuna ubaya kwa sababu binafsi sifurahishwi kuona watu wengine wakiumizwa π’
Mimi pia sipendi kuumizwa
Chai chai chaiAmen, amen barikiwa sana kwa maada mujarabu.
Umenifanya nibaki kambini mpaka sahivi, uzuri Jana tulipika wali kwahiyo nalinda kiporo hapaπππ
Hapa kwa watu nisiowafahamu vizuri kimeshanilamba mara nyingiUNAAKILI NZURI SANA. wabarikiwe wazazi wako.
Wengine hawapo kama wewe wala hawafikiri vizuri hivi. Ndio maana tunafundishwa kujihami pia na watu tusiowafahamu vizuri.