Human Nature

Jambo lolote lile linaloacha hisia za maumivu tunaliita baya

Labda kama wewe una jina lingine
Haya ni nijib na mimi
kufanikiwa kwako kuna watu wanaumia nalo jambo mbaya?
Unaweza kuona jambo baya kwako kwa mwingine jambo nzuri.
Mtu amekuibia kama ligekuwa jambo baya wasigegundua mifumo ya ulinzi ambayo wengine imewapatia ajira.
Ukiona mtu amefanya jambo linalokuumiza wewe jua amefanya kwaajili yake yeye ameona lipo sawa.
Mie sijawah kuagalia hili jambo ni nzuri au baya bali naagalia njia ya kulitumia.
Umenikata mkono ni sawa nitabakiwa na miguu nitajua njisi ya kutumia siwezi kuanza kulaumu wala kuumia et sina mikono. Maana aliyezikata kwake amepata faida.

Vaa viatu vyake utangudua yupo sahih japo watu wanamuona anakosea.
 
NINAKATAA KATA KATA

Jambo lolote unalofanya ambalo linaumiza au kusababisha uchungu kwa wengine ikiwa kuna njia nyingine kedekede za kufikia malengo yako bila kuwaumiza ni vigumu kusema kwamba hilo ni jambo sahihi mimi sikubaliani

Kwa mfano, mtu akukate mkono halafu useme yupo sahihi
Sahihi kwa mantiki ipi?
Kama kulikuwa na njia nyingine ya kutatua jambo bila kukudhuru kwa nini kuchagua njia ya kukuumiza?

Kwa mtazamo wangu, asili ya ulimwengu inaelekea kwenye ustawi
Mvua hunyesha.mimea huchipua
maua huchanua mazao hukua na matunda huzaa
Kuna mchakato wa kuendeleza na kujenga uhai hii ni asili ya dunia

Na mwanadamu naye amezaliwa akiwa na mwili uliokamilika kwa asili yake
Ana mikono, miguu, macho na viungo vingine kwa ajili ya kuishi na kufanya shughuli zake.za kila siku

Sasa kama mwanadamu amezaliwa akiwa na mkono wake kamili halafu mtu mwingine akamkata mkono
tunawezaje kusema hilo ni jambo la kawaida tu?(haingii akilini)

Hapo si tunaenda kinyume na hali yake ya asili na ustawi wake?

Kwa hiyo, kwangu mimi, si kila kitu kinachoweza kufanywa nitasema ni sahihi hapana kabisa yaani
 
Kwenye maisha kuna mambo yapo ndani ya uwezo wetu na mengine nje ya uwezo wetu.
Unapochagua mambo unakuwa umeruhusu kuumia asili ina sheria zake mtu anapovunja awe anajua au hajui lazma apate adhabu ya asili.
Kila mtu na falsafa yake kulingana na asili yake ila mim falsafa ya ustoa ndo nayoishi.
 
Aisee kila la kheri kwa falsafa hiyo mkuu🙏🙏
 
Yaan huku ulipokuja tutahamisha mada mkuu yaani kulikua na mantiki ipi
Mungu aumbe mabaya?
Ndio Mungu ndie aliyeumba mema na mabaya
Kwa faida ipi?
Aliumba mema na mabaya ili nature iweze kubalance.
Kwa lengo gani?
Nature isipo balance bhasi hakuna uhai tena. Hivyo lengo ni kuleta uhai.

-Fikilia simba wakiwa wengi kuzidi nyati Nini kitatokea?

-Fikilia kwanini umeme unapositive chaji na negative chaji?

-Fikilia maisha ya mwanaume bila mwanamke?

-Fikilia mti usingekuwa unapukutisha majani ingekuaje?

Hivyo Mungu ndiye aliumba mema na mabaya lakini changamoto inakuja kutokana na sisi wanadamu kuutumia ubaya kwa maslahi yetu. Mfano
Mtu anaamua kumuua mwenzake ili apate Mali,

Anatumia hila kazini ili apandishwe cheo.
 
Hisia huja naturally na zinatofautiana ukali(ukubwa) kati ya mtu na mtu but how you react or rather how you get driven by your feelings it's a completely different shit, hapo sasa ndipo akili na utashi vinapochukua nafasi. Unavyo-react inakuwa unaelewa madhara(consequences) ya hatua unazozichukua baada kuingiwa na hisia, kama unadhuru, unatesa, unaua, unadhalilisha au vyovyote vile baada ya kupatwa na hisia fulani hayo maamuzi inakuwa umeyafanya kwa kutumia akili na utashi wako na si hisia tena hapo unless kama ni immediate impulse ya papo kwa papo though unapaswa kufahamu kwamba hata hiyo immediate reaction hutofautiana kati ya mtu na mtu, we ain't the same.
 
asante ifatilie falsafa ya ustoa huenda ukajijengea kitu kipya.
Kama hiyo falsafa inasema kua mtu kumfanyia jambo la kuumiza mtu mwingine ni sahihi basi sina haja ya kuifatilia

Mimi naamini kujipenda kujijali kujilinda bila kutawanya maumivu kwa watu wengine
 
Hapa nipo kinyume na wewe
Mungu kuumba mabaya na mema basi ilikua mistake kubwa

Kwa sababu yeye husifiwa kua na uwezo usiomithilika basi angeweza kuiumba dunia kwa namna kila kitu kika balance bila ku mix huo ubaya na kuleta taharuki duniani

Tazama leo hii ubaya umetaradadi
Unaangamiza na kuharibu ladha ya maisha
 
Asante kwa maoni mazuri kaka angu
Karibu tena
 
Kuna mambo yanafanyika hapa kati mpaka naanza kuamini tunaishi na demons kwenye maisha halisia.....😢
 
Mambo gani?
Share kama hutajali
Mkuu unamuuaje mtu bila sababu ya msingi ukijua kabisa hana nguvu ya kukukabili!?😢 Unaenda mbali zaidi unajitapa kufanya hivyo mbele za watu ukiona unastahili sifa kwa kufanya hivyo...
 
Hapa nipo kinyume na wewe
Mungu kuumba mabaya na mema basi ilikua mistake kubwa
Hayo mabaya na mema yote yanampa sifa Mungu, Yaani yote yapo ili kumtukuza yeye.

Fikilia unapopitia magumu na alafu unapata msaada katika mazingira usiyotarajia hapo ni lazima utamtukuza Mungu. Lakini je! Lisingekupata hilo gumu ungemtukuza Mungu?

Pia ukisoma biblia unaona jinsi Mungu alivyojitukuza katika kuwatoa wana wa Israel kutoka Misri. Hapo utaona jinsi Mungu alivyoufanya moyo wa farao kuwa mgumu ili yeye aweze kujitukuza.

Kwa sababu yeye husifiwa kua na uwezo usiomithilika basi angeweza kuiumba dunia kwa namna kila kitu kika balance bila ku mix huo ubaya na kuleta taharuki duniani
Mkuu ukisema hivyo utataka kusema Simba ale nyasi ili asiwaumize swala😂.

Nature ni lazima ibalance kwa namna yoyote. Pia hakuna jambo baya litakupata endapo wewe haufanyi wala kuwawazia wengine ubaya na hata hilo baya likikupata bhasi Mungu ni lazima atajitukuza kwako. Mfano ni TUNDU LISSU

Tazama leo hii ubaya umetaradadi
Unaangamiza na kuharibu ladha ya maisha

Ubaya kutaradadi sio tatizo la Mungu ni tatizo la mwanadamu kupenda kutenda mabaya, Lakini pia ni tatizo la wanadamu wema kutokukemea mabaya.
 
Mkuu unamuuaje mtu bila sababu ya msingi ukijua kabisa hana nguvu ya kukukabili!?😢 Unaenda mbali zaidi unajitapa kufanya hivyo mbele za watu ukiona unastahili sifa kwa kufanya hivyo...
Inasikitisha sana
Mtu asie na tishio kwako wala kwa wengine kama anakosa anaweza kupewa onyo au kuwajibishwa bila kuuawa na kupewa nafasi nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…