Hukumu ya mahakama mtuhumiwa

Hukumu ya mahakama mtuhumiwa

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,750
https://www.jamiiforums.com/
Mtu anaweza kufunga kula chakula kwa mwaka mmoja na akabaki hai na salama. Mr Angus Barbiel, mwanaume wa Scotland, alifunga kula chakula (akiwa nyumbani kwake) kwa siku 382 kuanzia tarehe 14 June 1965 hadi tarehe 30 June 1966. Katika muda huo alikuwa anatumia tu maji, chai, kahawa na vitamins. Alikuwa na uwezo wa kutembea hadi kwenye hospitali yake ya karibu ya Maryfield Hospital for medical evaluation.

Muda wa kuishi bila kula chakula hutegemea wingi wa mafuta mtu aliyonayo mwilini mwake. Mafuta ni hifadhi ya chakula cha akiba. Kwa wanaume mengi ya haya mafuta huhifadhiwa kwenye tumbo (abdominal wall) na kuitwa kitambi. Kwa wanawake mengi ya mafuta haya huhifadhiwa kwenye makalio na chini ya ngozi (subcutaneous) na kuifanya ngozi kuwa laini yenye kuvutia. Akiba ya chakula ambayo mwili huwa inaihifadhi kwenye ini kama glycogen inatosha kwa siku tatu tu.

Hivyo mtu akifunga au kususa kula chakula mwili wake huanza kutumia hifadhi (stoke) yake ya akiba. Kwa siku takribani tatu za kwanza hutumia akiba yake ya glycogen iliyohifadhiwa kwenye ini lake. Baada ya hapo mwili huaza kutumia ile akiba yake ya mafuta (fat acids) kama chakula. Hii akiba ya mafuta ikimalizika mwili hugeukia protein zilizoko kwenye misuli (muscles) kwa kuzi deaminate na kuzitumia kama chakula. Misuli ndiyo akiba ya mwisho na baada ya hapo zikimalizika huwa hamna njia nyingine bali kurejea kwa Muumba. Huu mchakato hadi kurejea kwa Muumba huchukua miezi 3 kwa wengi lakini kwa wenye hifadhi ya kutosha kama huyo Mr Angus Barbiel wa Scotland unaweza kuchukua hata mwaka.

Asilimia 60% ya mwili wa binadamu ni maji ambayo hutumika kwenye processes mbali mbali (metabolism) ya cells za mwili. Maji haya yanahitaji constant and continuous refilling kutoka nje. Hivyo kususia kunywa maji ni suicidal attempt. Usipokunywa maji cells za mwili zitayatumia maji yaliyomo mwilini na mwili utapungukiwa maji. Hali hii inaitwa dehydration na ikiendelea ndani ya siku tatu cells zote hazitaweza kufanya kazi na utarejea kwa Muumba.

Kwa hiyo huyo jamaa aliyetishia kuanza kususa kula chakula, watu wala wasiwe na waswasi. Ameamua tu kupunguza akiba yake ya mafuta aka kitambi ambalo ni jambo jema kwa afya yake. Ila atakaposusia kunywa maji na kuwa severely dehydrated atundikwe dripu ya maji na kushitakiwa kwa kutaka kujiua (suicidal attempt
 
Endeleeni kudanganyana, yule mlafi kule unafkiri ataweza kukaa siku 3 bila kula.
Msiletewe porojo mwenyewe anakula mikuku mle mahabusu.
Ndio mana hataki kutolewa.
 
Back
Top Bottom