Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

View attachment 1628751

Naam, miaka 4 ya nenda - rudi kortini imehitimishwa leo baada ya hukumu ya mwisho kusomwa mahakamani.

Nachukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake katika safari hii; nawashukuru ndugu na familia kwa kuwa nami bega kwa bega katika kesi hizi na kunitia moyo; nawashukuru uongozi na watendaji wote wa JamiiForums kwa kuwa nami katika kila hatua; asanteni marafiki mliokuwa nami bila kunitupa na kuniombea kila mara; nawashukuru watanzania wote ambao kila mlipokutana nami (na wengine humu mitandaoni) mlisisitiza nisitetereke mpo nami; nawashukuru wanasheria mliokuwa nami mwanzo hadi mwisho na pia nawashukuru wadau wote wa habari na #UhuruWaKujieleza ambao mmekuwa mkitupa ushirikiano kwa namna moja ama nyingine.

Hakuna kesi ndogo, yamepita mengi lakini nikiri safari hii imekuwa na mafunzo mengi kwangu. Imekuwa safari ngumu lakini yenye faida kubwa kwani nimepata marafiki wa kweli, nimepata uelewa mpana zaidi na nimekuwa imara zaidi ya awali.

Sipendi kuongelea content ya kesi, ila niseme tu: Safari itaendelea, maisha yataendelea na hakuna kurudi nyuma. Milima, mabonde, mitikisiko n.k. havina budi kutokea - tutapimwa mwishoni kwa kusimama imara kwetu katika mawimbi haya. Asitiwe yeyote hofu, JamiiForums will always be JamiiForums! Niwaombe wadau wote kuzingatia mwongozo wa ushiriki katika Majukwaa, ni vipengele 16 muhimu sana.

Kwa wadau wengine wa Uhuru wa Kujieleza: Tunajenga nyumba moja, tusigombanie fito!


Hongera Mkuu.

God has been good.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom