Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
715D2CBB-EAAC-4827-8893-A34252A9689B.jpeg


Naam, miaka 4 ya nenda - rudi kortini imehitimishwa leo baada ya hukumu ya mwisho kusomwa mahakamani.

Nachukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake katika safari hii; nawashukuru ndugu na familia kwa kuwa nami bega kwa bega katika kesi hizi na kunitia moyo; nawashukuru uongozi na watendaji wote wa JamiiForums kwa kuwa nami katika kila hatua; asanteni marafiki mliokuwa nami bila kunitupa na kuniombea kila mara; nawashukuru watanzania wote ambao kila mlipokutana nami (na wengine humu mitandaoni) mlisisitiza nisitetereke mpo nami; nawashukuru wanasheria mliokuwa nami mwanzo hadi mwisho na pia nawashukuru wadau wote wa habari na #UhuruWaKujieleza ambao mmekuwa mkitupa ushirikiano kwa namna moja ama nyingine.

Hakuna kesi ndogo, yamepita mengi lakini nikiri safari hii imekuwa na mafunzo mengi kwangu. Imekuwa safari ngumu lakini yenye faida kubwa kwani nimepata marafiki wa kweli, nimepata uelewa mpana zaidi na nimekuwa imara zaidi ya awali.

Sipendi kuongelea content ya kesi, ila niseme tu: Safari itaendelea, maisha yataendelea na hakuna kurudi nyuma. Milima, mabonde, mitikisiko n.k. havina budi kutokea - tutapimwa mwishoni kwa kusimama imara kwetu katika mawimbi haya. Asitiwe yeyote hofu, JamiiForums will always be JamiiForums! Niwaombe wadau wote kuzingatia mwongozo wa ushiriki katika Majukwaa, ni vipengele 16 muhimu sana.

Kwa wadau wengine wa Uhuru wa Kujieleza: Tunajenga nyumba moja, tusigombanie fito!


 
kuna mwenye hamu na CCM?! Mwanakijiji, Pascal Mayala tunatumia jukwaa moja huku mkiunga mkono watesi
Huu ndio ukweli unaofichwa, kuna watu kadhaa wanatumia JF lakini wanafurahia unyama huu na wanaunga mkono, nakaribia kuishiwa uvumilivu siku chache zijazo nitawataja waziwazi, nitakaowakwaza wanisamehe, hatuwezi kufuga majini ndani ya chupa, iko siku yatachoropoka na kuanza kula watoto.

Liwalo na Liwe.
 
Nafuraha kuwa kile nilikiamini ndicho kimetendeka leo. Wacha leo ipite maana Mungu naijuwa kesho kuliko leo. Kazi yako na mchango wako ktk uchumi kama hawatoigubali basi mawe yatasema. Hongera sana Mkuu.
 
Sipendi kuongelea content ya kesi, ila niseme tu: Safari itaendelea, maisha yataendelea na hakuna kurudi nyuma. Milima, mabonde, mitikisiko n.k. havina budi kutokea - tutapimwa mwishoni kwa kusimama imara kwetu katika mawimbi haya.
Hakika umenena mkuu!
 
Mtu imara huonekana anapopata matatizo. Hakika wewe Max ni mtu imara. Wako wengi wamelegea na wamekubali kumtumikia shetani, wako wengi wamefikia mpaka kuomba msamaha huku ikiwa wao ndio wamekosewa!

Tumebakiza muda kidogo tutavuka zama hizi za shetani, kwani shetani huwa na nguvu kubwa, lakini ni nguvu za muda mfupi tu.
 
Pole Sana Kwa Yote, Hatimaye Hakuna Marefu Yasiyokuwa Na Ncha. Kesi Imekwisha Ila Oops, Hawa Watu Siyo!!!

Mungu Ni Mwema Wakati Wote.

Haki Huinua Taifa Bali Dhambi ni Aibu Kwa Watu Wote
 
Back
Top Bottom