Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

Hongera sana na pole naamini sasa ndio umeiva katika uendeshaji wa mtandao.

USHAURI: jitahidi kufuata sheria ukibalance na miiko ya uliyo jiwekea. Kama tuu hapa JF tunaishi kwa masharti na miiko uliyotuwekea. Hakuna shuguli yeyote isiyo na masharti au miiko.
 
Mungu ashukuriwe sana. Hatimaye mzigo umeutua, ila sijapendezwa na hukumu iliyotolewa. Nadhani kuna mtego hapo. Polis wanaweza kuja tena kukutaka utoe taarifa za members kadhaa ukikataa, mahakamani na utaonekana umetenda kosa la kukiuka masharti ya hukumu hii.
 
Sijui kwa nn naona km mmetuuza. Naogopa kufunguka zaidi lkn nimeeleweka na wanaoelewa nadhani.
 
"Safari itaendelea, Maisha yataendelea na hakuna kurudi nyuma" - Melo.

Vyema umetambua hilo, haya mapambano yataendelea kuwepo siku zijazo ni vyema uwe tayari kukabiliana nao wakati wowote, usiogope.

All the best.

Maneno yako ni kweli, maadamu hawa CCM wangalipo, lazima tuwe tayari kuwakabili tena kwani wanaweza kurudi wakati wowote kujaribu kuliharibu shamba.
 
Asante, pole - ukiona nyani kazeeka basi jua kakwepa mishale mingi - naona ukiifaa tuzo ya Mo Ibrahim!

God and time jipe moyo mkuu
 
Hongera sana na pole naamini sasa ndio umeiva katika uendeshaji wa mtandao.

USHAURI: jitahidi kufuata sheria ukibalance na miiko ya uliyo jiwekea. Kama tuu hapa JF tunaishi kwa masharti na miiko uliyotuwekea. Hakuna shuguli yeyote isiyo na masharti au miiko.

Hata makaburu wa Afrika kusini walitunga sheria, ila zilikuwa sheria zenye nia ovu na kandamizi. Keep it in your mind.
 
Mimi na familia yangu tunatuma salamu za pole na hongera kwako Melo,

Kila jambo huja kwa makusudio na hii ni changamoto najua imezidi kukuweka imara,
Siku zote Mungu yupo kwa wale wasimamia ukweli na haki,

Hongereni sana uongozi wote wa JamiiForums, tunajivunia Forum yetu, tunajivunia nyinyi.
 
Huu ndio ukweli unaofichwa, kuna watu kadhaa wanatumia JF lakini wanafurahia unyama huu na wanaunga mkono, nakaribia kuishiwa uvumilivu siku chache zijazo nitawataja waziwazi, nitakaowakwaza wanisamehe, hatuwezi kufuga majini ndani ya chupa, iko siku yatachoropoka na kuanza kula watoto.

Liwalo na Liwe.
Ni kweli. Kuna mijitu ya hovyooo kabisa humu. Wametumia JF kuwabeba watesi ambao ni CCM na genge lake la vibaka wa kura, waua demokrasia na madikteta dhidi ya uhai wa watu, haki na uhuru wa habari. Wanafahamika hata kwa majina. Ushindi huu wa JF dhidi ya kesi haramu iwe laana kwa waganga njaa hawa wanaojikomba kihasara kutafuta uteuzi.
 
JamiiForums nisawa na dunia,

Imejaa watu wakila aina, wapo wanao jaribu kuitoboa, wapo wanao jaribu kuichoma, wapo wanao jaribu kujimwambafai, wapo wanao jaribu kutawala wenzao lakini wapo waliojaribu kumtukana Muumba wa hii dunia na wengine walijaribu kumshitaki Muumba (creator)
Lakini wote tunaishi nao hapa hapa duniani na uhai wao ni hapa hapa

Ndivyo ilivyo kwa JamiiForums hata watesi wako hunao hapa hapa kwenye forums na lengo lao ni kuitikisa na kuibomoa forums
Lakini kila kitu kina makusudi yake na yote yanayo fanyika chini ya jua ni ubatiri.

Unayo yapitia Mungu anakuandaa kuwa mtu fulani yaani kuifikia Destiny yako aliyo kuitia hapa duniani ili siku ikifika usije ukamwangusha Mungu.
 
Back
Top Bottom