Maxence Melo awatambua Dr. Gwajima na Dr. Mwigulu kwa kushiriki mijadala JamiiForums

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Katika siku ya kuwazawadia washidni wa stories of change 2023, sherehe zilizofanyika Hyatt Regency, usiku wa Oktoba 7, 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums alitambuamchango mkubwa wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Doroth Gwajima.

Dr. Gwajima ametajwa kama mmoja wa mawziri ambao wameingia JamiiForums ili kusikia Mawazo ya wananchi, kuelezea baadhi ya vitu na kutoa taarifa kuhusu wizara yake. Jambo hili limechukuliwa kipekee kwa kuwa ni viongozi wachache ambao wako humu kwa majina yao halisi na kuwa verified.

Kwasababu sawa na hiyo, Maxence amemtambua Dr. Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa fedha na mipango kwa kushiriki na kujibu hoja za wadau ndani ya JamiiForums.

Katika sherehe hizo ambazo zilimpatia Athanas Myonga Tsh. Milioni 7 kwa kuwa mshindi wa kwanza, ndugu yetu maarufu humu JamiiForums Mshana Jr, pia alitajwa na Maxence Melo. Mshana ni kati ya wanachama walioalikwa kwenye shughuli hiyo Kwenda kula bata. Alipiga suti kali na tai ya buluu Kwenda sawa na mazingira.

Nadhani Mshana amejijengea heshima kubwa ndani ya JF na nje ya JF ndio sababu ya JamiiForums kumualika katika shughuli zake. Suala kama hili ni wito kwa wanachama wengine kuwa wazuri ili kupata fursa za kuinteract na wadau wengine kujenga connections.

Aidha kuhusu mada yangu kuu nadhani ni vyema kwa viongozi wengine kujiunga JamiiForums ili kupata Mawazo ya wadau na kushauriana ili wananchi wasione wameachwa Upweke.

Kutoka Morogoro Ndanindani (Nimerudi baada ya kula kuku wa Stories of Change 2023). Ni mimi Analogia Malenga

9u9a5402-jpg.2777953
 
Attachments

  • 9U9A5402.JPG
    1.4 MB · Views: 28
Hawa JF wa siku hizi wame ajiri hadi TISS, ni Thread za upuuzi tu ndio zipo JF. Zenye akili hufutwa na Vi moderator vya mchongo.
Kama hauridhishwi na utendaji wa moderators wa JamiiForums una room ya kuwasilisha malalamiko yako kwenye Jukwaa la Complaints. Hii yote ni kuhakikisha wanachama wote wanapata haki ya kutoa mawazo yao ndani ya JamiiForums.

Aidha, moderators wa JamiiForums wanafanyakazi zao kwa kufuata muongozo wa mjadala ( https://www.jamiiforums.com/threads...mwongozo-wa-ushiriki-kwenye-mijadala.1753332/ ). Ukitendewa kinyume na yaliyomo hapo tafadhali andika kwenye Jukwaa la Complaints.

Karibu.
 
Katika siku ya kuwazawadia washidni wa stories of change 2023, sherehe zilizofanyika Hyatt Regency, usiku wa Oktoba 7, 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums alitambuamchango mkubwa wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dr. Doroth Gwajima.

Dr. Gwajima ametajwa kama mmoja wa mawziri ambao wameingia JamiiForums ili kusikia Mawazo ya wananchi, kuelezea baadhi ya vitu na kutoa taarifa kuhusu wizara yake. Jambo hili limechukuliwa kipekee kwa kuwa ni viongozi wachache ambao wako humu kwa majina yao halisi na kuwa verified.

Kwasababu sawa na hiyo, Maxence amemtambua Dr. Mwigulu Nchemba ambaye ni Waziri wa fedha na mipango kwa kushiriki na kujibu hoja za wadau ndani ya JamiiForums.

Katika sherehe hizo ambazo zilimpatia Athanas Myonga Tsh. Milioni 7 kwa kuwa mshindi wa kwanza, ndugu yetu maarufu humu JamiiForums Mshana Jr, pia alitajwa na Maxence Melo. Mshana ni kati ya wanachama walioalikwa kwenye shughuli hiyo Kwenda kula bata. Alipiga suti kali na tai ya buluu Kwenda sawa na mazingira.

Nadhani Mshana amejijengea heshima kubwa ndani ya JF na nje ya JF ndio sababu ya JamiiForums kumualika katika shughuli zake. Suala kama hili ni wito kwa wanachama wengine kuwa wazuri ili kupata fursa za kuinteract na wadau wengine kujenga connections.

Aidha kuhusu mada yangu kuu nadhani ni vyema kwa viongozi wengine kujiunga JamiiForums ili kupata Mawazo ya wadau na kushauriana ili wananchi wasione wameachwa Upweke.

Kutoka Morogoro Ndanindani (Nimerudi baada ya kula kuku wa Stories of Change 2023). Ni mimi Analogia Malenga, .
Tuonyeshe picha ya mshana akiwa kabalia hiyo suti

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Kama hauridhishwi na utendaji wa moderators wa JamiiForums una room ya kuwasilisha malalamiko yako kwenye Jukwaa la Complaints. Hii yote ni kuhakikisha wanachama wote wanapata haki ya kutoa mawazo yao ndani ya JamiiForums.

Aidha, moderators wa JamiiForums wanafanyakazi zao kwa kufuata muongozo wa mjadala ( https://www.jamiiforums.com/threads...mwongozo-wa-ushiriki-kwenye-mijadala.1753332/ ). Ukitendewa kinyume na yaliyomo hapo tafadhali andika kwenye Jukwaa la Complaints.

Karibu.
Nani anaskiliza ushauri wa mtu au malalamishi ya mtu Tz hii?

Siku hizi JF ni kijiwe cha story tena zisizo na mbele wala nyuma.

Hapa pia wata soma maoni.
 
Kama hauridhishwi na utendaji wa moderators wa JamiiForums una room ya kuwasilisha malalamiko yako kwenye Jukwaa la Complaints. Hii yote ni kuhakikisha wanachama wote wanapata haki ya kutoa mawazo yao ndani ya JamiiForums.

Aidha, moderators wa JamiiForums wanafanyakazi zao kwa kufuata muongozo wa mjadala ( https://www.jamiiforums.com/threads...mwongozo-wa-ushiriki-kwenye-mijadala.1753332/ ). Ukitendewa kinyume na yaliyomo hapo tafadhali andika kwenye Jukwaa la Complaints.

Karibu.
Ujumbe nimefikisha tiyari
 
Stories of change. Ila tupo vile vile miaka na miaka. Zimebaki stori tu..

NB: Tuzo za vitabuni tu. Nendeni vijijini mkaone watu wanabadilisha maisha ya wengine, achaneni kupoteza pesa Kwa kuwalipa walamba lips hapo Hyatt
Kabisa mkuu,hizo story of change hazina impact zozote. Zinaishia kwenye makaratasi tu.
 
Stories of change. Ila tupo vile vile miaka na miaka. Zimebaki stori tu..

NB: Tuzo za vitabuni tu. Nendeni vijijini mkaone watu wanabadilisha maisha ya wengine, achaneni kupoteza pesa Kwa kuwalipa walamba lips hapo Hyatt
Acha makasiriko Mkuu, umefatilia kweli ukaona yanayotolewa hayana maana? Umefatilia kujua washindi wametokea maeneo gani? Tupunguze lawama kidogo, yakitokea mengine shiriki na wewe acha wivu kwa washindi?😂😂😂
 
Kwa kweli tumpe maua yake Mh. Gwajima kwa ushiriki wake mzuri hapa JF.

Mungu akubariki sana Maxence Melo na Dk. Gwajima.
 
Back
Top Bottom