Hudhuria msiba

Hudhuria msiba

niliwahi msikia padre mmoja alisema msiba ili ukufikie una hatua tatu.....ya kwanza utampata rafiki yako...yapili utasogea kwa ndugu yako kama binamu.shangaz...na ya tatu unafika kwako ambapo unamkuta mama au mzee wako..hapo ndo utapohisi dunia chungu
Yeah exactly this happened to me.... Rest in peace ever loved Mom & Dad

Jr[emoji769]
 
Kama nimetoka nje ya reli huwa nalud mwenyewe tu maana madini unayo nipa ni fundisho Tosha. God bless u bro
 
Mie jamani nashindwa kwenda misibani
Naweza nikajitayarisha kabisa
Nikarudi kukaa chini
Kwa misiba ya majirani na marafiki
Ila ile ya kifamilia nahudhuria japo sitizami marehemu,

Nikitoka hapo na kuwa na huzuni wiki nzima
 
Msiba hauzoeleki, msiba usikie kwa jirani tu lkn ukikufika haki ya nani maumivu yake hayana kiwango, nlifiwa na mamaang mdogo alokuwa ananilea nikiwa mdogo wa darasa la tano, ni mama alkuwa ananipenda kiwango cha juu mnooo, nkachukuliwa na Uncle na yy akafariki pia,ni vitu ambavyo sijawahi kusahau na kila nkienda kwenye msiba wa mtu nalia kwa kuwakumbuka basi tu kifo jamani
 
Mungu Mwenyezi asingetuumbia kusahau..... wengi wangekuwa wanatembea barabarani wakiwa wanalia....
 
Kama nimetoka nje ya reli huwa nalud mwenyewe tu maana madini unayo nipa ni fundisho Tosha. God bless u bro
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji144][emoji144][emoji144]

Jr[emoji769]
 
Hudhuria msiba,*
- Ukajifunze kuwa mnyenyekevu. Tena ukajikumbushe kusamehe na kuishi kwa amani na watu wote. ukamheshimu mkubwa na mdogo, masikini na tajiri, maana utaikosa mbingu kwasababu utakufa na jeuri, hasira, chuki,kinyongo,gubu, na manung'uniko yaliyoujaza moyo wako.
Umenikumbusha kitu kikubwa sana, nitajitahidi kusawazisha mahusiano yangu na Mungu. Asante Sana Mshana Jr umenisaidia Sana kiroho... Naomba Mungu anipe nguvu ya kusimama katika kweli yake. Amina
 
Umenikumbusha kitu kikubwa sana, nitajitahidi kusawazisha mahusiano yangu na Mungu. Asante Sana Mshana Jr umenisaidia Sana kiroho... Naomba Mungu anipe nguvu ya kusimama katika kweli yake. Amina
[emoji123][emoji120][emoji120]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom