Hudhuria msiba

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,720
*Hudhuria msiba,
- ukauone uchungu na huzuni ya kuondokewa na ndugu/rafiki wa karibu. Hata tunapomlilia na kuzimia kwa sababu ya umuhimu wake (marehemu) kwetu - hawezi kuwa hai tena. Ametoweka tayari.

*Hudhuria msiba,*
- ukauone ukomo wa maisha ya mwanadamu. Labda utakumbuka kuwa hapa(duniani) hatukuja kudumu. Tena tunatoweka haraka kama ua la kondeni.

*Hudhuria msiba,*
- Ukamuone rafiki/ndugu aliyelala mauti. Haijui jana yake wala kesho yake. Hana habari yoyote na hawezi kuinuka wala kufumbua macho tena. Ametoweka kabisa. Hata ukimlilia hasikii, hata ukitaka akusamehe (kama ulimkosea) hawezi tena.

*Hudhuria msiba,*
- ukauone ukomo wa jeuri, kiburi, na majivuno. Yanayokupa jeuri na kiburi punde hayatokusaidia kuikwepa mauti. (Marehemu) alimiliki mali nyingi alizozihangaikia tangu ujana wake, lakini hakuna anachoingia nacho kwenye sanduku dogo la mbao. Tena anaacha vyote na kutelemka kwenye udongo ambao siku chache baadae atafanana nao.

*Hudhuria msiba,*
- Ukajifunze kuwa mnyenyekevu. Tena ukajikumbushe kusamehe na kuishi kwa amani na watu wote. ukamheshimu mkubwa na mdogo, masikini na tajiri, maana utaikosa mbingu kwasababu utakufa na jeuri, hasira, chuki,kinyongo,gubu, na manung'uniko yaliyoujaza moyo wako.

*Hudhuria msiba,*
- ukajikumbushe ukuu wa Yeye anayekupa kuishi leo. Maana akiiondoa pumzi ya uhai aliokupa (bure) ghafla unakuwa takataka, ndege,wanyama, na wadudu watakula mwili wako.

*Hudhuria msiba,*
- ukakumbushwe kujinyenyekeza kwa muumba wako. Yeye aliyekuumba kwa makusudi maalum. Hata ulipoanguka dhambini na kustahili adhabu hii ya kifo- Yeye alikukomboa kwa damu yake, na kukuahidi maisha ya milele kama utachagua kuokolewa. Maana aliyetuumba na kutupatia uhai, ana uwezo wa kuturejeshea uhai. Tena ameahidi kutupatia miili mipya isiyokufa wala kuharibika

*HUDHURIA MSIBA,*
- Ukakumbushwe kuishi maisha matakatifu, ya kumpendeza Mungu- maana katika saa usiyoijua, utalala usingizi wa mauti. Jiweke mikononi mwa Bwana kila siku, kila saa - ili akutumie apendavyo, ukawe baraka kwa jamii inayokuzunguka. Hata saa yako ya kufa ikifika, ulale taratibu kwa ushindi mkubwa- maana maisha yako yamemtukuza Yeye aliye muumba wa mbingu na nchi.

TUMWOMBE MUNGU -atufundishe kutambua ufupi wa maisha yetu, ili tuweze kuwa na hekima. (Zab. 90:12)

Jr
 
Alikuwa anajichoma ili iweje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa na depression nadhani so akawa anazitumia kama antdepresant ,mwanzon alikua anachoma diazepam lakini baadae akawa anachoma ketamine kabisa ( hii ni dawa ya nusu kaputi wakat wa opareshen) basi majuzi alivyochoma ndio hakuamka. Very sad aisee Last seen yake wasap ijumaa saa kumi ,í don believe..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mhubiri 7:2
afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu,
kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu,imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.
7:4
Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha.
 
72 Reactions
Reply
Back
Top Bottom