Hudhuria msiba

Hudhuria msiba

Hudhuria msiba
78599e2c1afe365357e64f6c4cfd2cdf.jpeg

Jr[emoji769]
 
U
Ukitaka ujue raha ya msiba kaage maiti iliyolala Kimya kwenye jeneza huku imefumba macho na huku imepauka kwa damu kuganda halafu ina pamba mdomoni na puani na huo mkao ndio wa milele Kama alikuwa anakudai hutamlipa milele milele milele na Kama mlikuwa hamJasameheana ndio milele na milele yeye anaenda kuliwa na funza na mafunyo yatakayotoka sehemu zote za matundu ya mwili Kwahiyo mwanamke mafunyo mengi yanatokea kwenye uke yakitokea tumboni Kwahiyo uke uliotunyima duniani sasa ndio njia kubwa sana ya mafunyo ya njano huku sanda ikilowa ujiuji WA njano na kijani unaonuka vibaya mnoooo
Hivi wewe mzima kichwani kweli?!
 
[emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji87][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
U
Ukitaka ujue raha ya msiba kaage maiti iliyolala Kimya kwenye jeneza huku imefumba macho na huku imepauka kwa damu kuganda halafu ina pamba mdomoni na puani na huo mkao ndio wa milele Kama alikuwa anakudai hutamlipa milele milele milele na Kama mlikuwa hamJasameheana ndio milele na milele yeye anaenda kuliwa na funza na mafunyo yatakayotoka sehemu zote za matundu ya mwili Kwahiyo mwanamke mafunyo mengi yanatokea kwenye uke yakitokea tumboni Kwahiyo uke uliotunyima duniani sasa ndio njia kubwa sana ya mafunyo ya njano huku sanda ikilowa ujiuji WA njano na kijani unaonuka vibaya mnoooo

Jr[emoji769]
 
Kama Mshana ni mkristu, huenda ulisomea upadre ukaacha maana hizo ni nasaha za kipadri. Huenda watu wengine wanaamini binadamu anakufa kama mnyama asiye na utashi, ndio maana ushetani umezidi. Kwa nini mtu anamuua mwenzake akijua nae atakufa? Tukitumie hekima ulizoandika tunaweza kugundua kitu na kuacha uovu. Ubarikiwe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu haya maneno.. Lakini Mi sielewagi sijui kwanini Yale maneno yanayosemwaga pale huwa yana gusa Sana hisia, mpk unasema Leo mwisho . Lakini ukishageuka tu tumesahau kabisa.. Hivi ni Mimi tu ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio wewe tu mkuu[emoji24][emoji24]

Happy dude [emoji67]‍[emoji538]
 
Mie nimeondokewa na Wazazi wangu wote wawili, Baba na Mama. Lakini aliyeniuma kuliko kawaida ni Baba yangu, mama haikuniuma sana maana nilikuwa mdogo kipindi anafariki kwahiyo sikuumia sana. Baba yangu anafariki mimi ndio nimepata kazi na nina mwezi mmoja kazini. Nilitamani sana Baba angu ale jasho alilolipigania kipindi mie nasoma O level na A level mzee wangu alikuwa yupo tayari nyumbani walale njaa siku hiyo ila anitumie pesa ya matumizi au michango shuleni.
Kwa mimi, kama ingelikuwa ni uhakika ukifa unaenda kuonana na ndugu waliotangulia mie ningechagua kifo kinichukue nikamuone mzee wangu, Shujaa wangu.
Pumzika kwa Amani Baba[emoji24]

Happy dude [emoji67]‍[emoji538]
 
*Hudhuria msiba,
- ukauone uchungu na huzuni ya kuondokewa na ndugu/rafiki wa karibu. Hata tunapomlilia na kuzimia kwa sababu ya umuhimu wake (marehemu) kwetu - hawezi kuwa hai tena. Ametoweka tayari.

*Hudhuria msiba,*
- ukauone ukomo wa maisha ya mwanadamu. Labda utakumbuka kuwa hapa(duniani) hatukuja kudumu. Tena tunatoweka haraka kama ua la kondeni.

*Hudhuria msiba,*
- Ukamuone rafiki/ndugu aliyelala mauti. Haijui jana yake wala kesho yake. Hana habari yoyote na hawezi kuinuka wala kufumbua macho tena. Ametoweka kabisa. Hata ukimlilia hasikii, hata ukitaka akusamehe (kama ulimkosea) hawezi tena.

*Hudhuria msiba,*
- ukauone ukomo wa jeuri, kiburi, na majivuno. Yanayokupa jeuri na kiburi punde hayatokusaidia kuikwepa mauti. (Marehemu) alimiliki mali nyingi alizozihangaikia tangu ujana wake, lakini hakuna anachoingia nacho kwenye sanduku dogo la mbao. Tena anaacha vyote na kutelemka kwenye udongo ambao siku chache baadae atafanana nao.

*Hudhuria msiba,*
- Ukajifunze kuwa mnyenyekevu. Tena ukajikumbushe kusamehe na kuishi kwa amani na watu wote. ukamheshimu mkubwa na mdogo, masikini na tajiri, maana utaikosa mbingu kwasababu utakufa na jeuri, hasira, chuki,kinyongo,gubu, na manung'uniko yaliyoujaza moyo wako.

*Hudhuria msiba,*
- ukajikumbushe ukuu wa Yeye anayekupa kuishi leo. Maana akiiondoa pumzi ya uhai aliokupa (bure) ghafla unakuwa takataka, ndege,wanyama, na wadudu watakula mwili wako.

*Hudhuria msiba,*
- ukakumbushwe kujinyenyekeza kwa muumba wako. Yeye aliyekuumba kwa makusudi maalum. Hata ulipoanguka dhambini na kustahili adhabu hii ya kifo- Yeye alikukomboa kwa damu yake, na kukuahidi maisha ya milele kama utachagua kuokolewa. Maana aliyetuumba na kutupatia uhai, ana uwezo wa kuturejeshea uhai. Tena ameahidi kutupatia miili mipya isiyokufa wala kuharibika

*HUDHURIA MSIBA,*
- Ukakumbushwe kuishi maisha matakatifu, ya kumpendeza Mungu- maana katika saa usiyoijua, utalala usingizi wa mauti. Jiweke mikononi mwa Bwana kila siku, kila saa - ili akutumie apendavyo, ukawe baraka kwa jamii inayokuzunguka. Hata saa yako ya kufa ikifika, ulale taratibu kwa ushindi mkubwa- maana maisha yako yamemtukuza Yeye aliye muumba wa mbingu na nchi.

TUMWOMBE MUNGU -atufundishe kutambua ufupi wa maisha yetu, ili tuweze kuwa na hekima. (Zab. 90:12)

Jr[emoji769]
AMINA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado ninawaza mpaka Leo.

Hapa nililia lia kweli mkanipa nauli. Nikaenda Mbeya.

Yaliyonipeleka kubwa ni kupeana mkono na mume wangu wa ndoa ambaye tuliishi miaka kama 18 Kwa kutengana.

Nilimkuta, kweli zoezi likafanikiwa. Asanteni sana mlionipa nauli.

Nilichoshangaa, asubuhi tumeenda rufaa kama kawaida. Bahati mbaya Mungu akawa ameshamchukua mtu wake.

Ile nimerudi pale nyumbani sasa tumeshaatenga msiba.

Kuna uchungu mkubwa sana uliniingia kwenye uti wa mgongo nikazimia.

Wazazi wangu waliondoka sikuwahi kuzimia, hebu niambie Mshana Jr ni kwanini ikawa vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Kama Mshana ni mkristu, huenda ulisomea upadre ukaacha maana hizo ni nasaha za kipadri. Huenda watu wengine wanaamini binadamu anakufa kama mnyama asiye na utashi, ndio maana ushetani umezidi. Kwa nini mtu anamuua mwenzake akijua nae atakufa? Tukitumie hekima ulizoandika tunaweza kugundua kitu na kuacha uovu. Ubarikiwe!

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
Nitakurejea @mamndenyi

Back
Top Bottom