Pole kwa Rais Samia Kufuatia Msiba wa Mama Karume

Pole kwa Rais Samia Kufuatia Msiba wa Mama Karume

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
889
Reaction score
774
Mpendwa Mama Samia

Shikamoo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mama wakati mwingine ninapotazama safari yako, najikuta nikijiuliza ni wapi msichana anayekaribia kukata tamaa anaweza kujifunza nguvu, uvumilivu na moyo wa kusimama tena na jibu ninaloliona ni kwako Mama Rais. Hakuna kitabu kizuri kwa kijana, kwa binti wa kitanzania kama maisha yako. Ni kitabu kilicho wazi; kitabu kinachofundisha kwamba changamoto hazipaswi kuwa sababu ya kukata tamaa, bali ni sehemu ya safari ya kujenga nguvu na kufikia unapotamani kufika.

Wewe ni mwanamke wa shoka, mwamba wa kweli, mwenye kutufundisha kwa vitendo maana ya uvumilivu, uthubutu na kusimama imara hata pale safari inapokuwa ngumu, mawimbi mengi na dhoruba.

Pole sana kwa msiba wa Mama Fatma Karume.

Sifahamu mengi kuhusu historia yenu, lakini kwa nilichokiona kwa mbali, uhusiano wa mama na mtoto uliokuwa wa kweli, wa dhati na wenye upendo wa kipekee.

Katika kipindi hiki kigumu, naomba upokee pole zangu za dhati. Endelea kusimama imara, Mama. Mungu akupe nguvu, faraja na moyo wa kuvumilia katika nyakati hizi za majonzi.

Allah azidi kukupa nguvu, afya njema, hekima na ulinzi katika kila hatua ya safari yako.
Tunakuombea na tunakupenda, Mama. Allah akulinde na akupe nguvu zaidi kila siku.

Apumzike kwa amani, Mama Fatma 🕊️🤍Karume. Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un. 🤲🏽

IMG-20260921-WA0118.jpg
 
Ndugu Moderators hapo kwenye reaction ilifaa muongeze reaction ya "🖕🏼" tuwe tunaitumia kwenye baadhi ya threads
Ingependeza sana
 
Back
Top Bottom