Bado hajachelewa sana, kuna njia nyingi za kutumia ili kuboresha uwezo wake wa kutoa hotuba. Kwanza kabisa atengeneze studio humo mwenye kasri lake la magogoni. Studio hiyo iwe ya nusu duara kwa mbele pamoja na audio na video recording system. Sasa kule kwenye nusu duara awe anaweka picha kubwa za kuonyesha mazingira mbalimbali ya hotuba: mikutano ya ngazi ya chini kama ile ya hadhara ambayo nadhani anaijua vizuri zaidi, mikutano ya ngazi ya kati kama kwenye za kitaifa, mikutano ya ngazi za juu kama kwenye kukutana na waandishi wa habari na kuhutubia formal setting kama kwenye vyuo vikuu, umoja wa mataifa nk. Hapa awe na maswali yaliyotayarishwa randomly na ajifunze pia jinsi ya kujibu maswali asiyojua majibu yake kwa njia ya kuridhisha.
Baada ya kuwa na maandalizi hayo, awe na PREP kila jioni kati ya saa mbili na saa nne jioni kama tulivyokuwa tukifanya huko sekondari boarding. Awe anapractice kutoa hotuba na kujirekodi mwenyewe, kisha ajitazame na kujilinganisha na vipanga wengine wa hotuba kama Nyerere. Kila atakapofanya hivyo atagundua weaknesses zake na atarekebisha kwa vile nina imani anao uwezo wa kujirekebisha. Akifanya hivyo, itamchukua miezi mitatu au minne tu kwa yeye naye kuwa kipanga wa kutoa hotuba.