Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Waheshimiwa!
Swala kuu sio kutoa hotuba nzuri au mbaya, bali ni utendaji wa viongozi wetu na waliowazunguka.Mtu mahiri katika uongozi ni yule anayeelewa mapungufu yake na kutumia dhamana aliyopewa kutafuta wasaidizi waliobobea kwenye fani husika(wataalaam elekezi) ambao ni mahiri na makini katika utendaji ili awatumie kuziba hayo mapungufu kwa lengo la kuleta ufanisi.Sasa kama Mheshimiwa Rais ameona anamapungufu katika uandikaji basi alitakiwa atumie maamuzi sahihi katika hilo kwa kutafuta mtaalamu elekezi kwenye fani ya uandishi wa hotuba na huyo ndiye amtumie kwani kwa level yake inawezekana .Sijui wakulaumiwa ni nani kwa hizo hotuba watu wanazoziona hazina hadhi ya cheo chake kwani hata kama hakuziandika yeye lakini ni yeye ndiye aliyewakubali hao waliomuandikia waifanye hiyo kazi na yeye kukubali kwenda kuiwakilisha hadharani kunathibitisha ukubali wake, kwani kila anayeisoma au kuisikia hatasema hotuba ni ya Mwandishi aliyeifanya hiyo kazi, bali ni hotuba ya Rais.
 
Waheshimiwa!
Swala kuu sio kutoa hotuba nzuri au mbaya, bali ni utendaji wa viongozi wetu na waliowazunguka.Mtu mahiri katika uongozi ni yule anayeelewa mapungufu yake na kutumia dhamana aliyopewa kutafuta wasaidizi waliobobea kwenye fani husika(wataalaam elekezi) ambao ni mahiri na makini katika utendaji ili awatumie kuziba hayo mapungufu kwa lengo la kuleta ufanisi.Sasa kama Mheshimiwa Rais ameona anamapungufu katika uandikaji basi alitakiwa atumie maamuzi sahihi katika hilo kwa kutafuta mtaalamu elekezi kwenye fani ya uandishi wa hotuba na huyo ndiye amtumie kwani kwa level yake inawezekana .Sijui wakulaumiwa ni nani kwa hizo hotuba watu wanazoziona hazina hadhi ya cheo chake kwani hata kama hakuziandika yeye lakini ni yeye ndiye aliyewakubali hao waliomuandikia waifanye hiyo kazi na yeye kukubali kwenda kuiwakilisha hadharani kunathibitisha ukubali wake, kwani kila anayeisoma au kuisikia hatasema hotuba ni ya Mwandishi aliyeifanya hiyo kazi, bali ni hotuba ya Rais.
 
Pamoja na kwamba Kalaghe alikuwa anamwandikia Mkapa hotuba, lakini bado Mkapa mwenyewe alikuwa anazihariri hotuba zake na kuna kipindi alikuwa anaandika upya kabisa. Nakumbuka vizuri terehe 16.02.1999 Mkapa alihutubia jumuiya ua UDSM. Kwa utaratibu wa viongozi wetu wakitembelea taasisi huandaliwa hotuba na hiyo taasisi. Hata hivyo siku hiyo Mkapa hakutumia ile hotuba aliyoandaliwa na chuo na alitoa hotuba kali sana ambayo kila mtu ilimwacha hoi. Kwa hiyo pamoja na kuwa na mwandishi wa hotuba, lazima mtoa hotuba naye aweze kuihariri. Bila kuhariri utaisoma kama kasuku na utapwaya. Ndo haya mzee mwinyi alichemsha alipokuwa chancellor UDSM katika graduation moja. katika kutunukuu shahada alipoona BSc Eng. yeye akasema 'Nakutunukuu Bachellor of Science in English' watu weweeeee! Yote haya ni tatizo la kukariri bila kuhariri!

At the end of the day, when it comes to being a leader, ideas matter. All great speech makers had ideas. If a leader cannot make a good speech, the first assumption is that s/he lacks ideas. So the question is Do our leaders have ideas?
 
Mwanasiasa, viongozi wetu wengi hawana mawazo ya kimandeleo. Leo ukiwauliza wanatakakutupeleka wapi baada ya miaka mitano, wanaweza kujiumauma sana! Bora liende

Siamini uwezo mdogo wa muandishi wa hotuba za rasi ndio Tatizo, tatizo ni rasi mwenyewe ambae hajui jambo lipi zuri la lipi baya na kwa vile hana malengo inakuwa ni vigumu hata kutafuta waandishi wazuri wa hotuba. Mtazamo wake ni kujirusha ikulu, kwahiyo lazima ataaalika ndugu na watoto wa washikaji zake kwenye karamu.

Jk anatoa hotoba mbovu kwa sababu huo ndio uwezo wake.
 
All in all hizo ideas inatakiwa zitumike kuwakomboa wazisikilizao.Speech huwa zina faida sana wakati wa vipindi vya transition,au kuinitiate change. Kwa Tanzania ya leo hamna speech bora kama kuwekeza kwenye elimu sahihi ya wananchi, kwa maana ya kwamba hizo ideas ziwe implemented, idea za majukwaani watu kuishia kukenua na kupiga makofi tumezichoka
 
Mwanasiasa,

Naomba nikoleze paragraph ya pili:

Pamoja na kwamba Kalaghe alikuwa anamwandikia Mkapa hotuba, lakini bado Mkapa mwenyewe alikuwa anazihariri hotuba zake na kuna kipindi alikuwa anaandika upya kabisa. Nakumbuka vizuri terehe 16.02.1999 Mkapa alihutubia jumuiya ua UDSM. Kwa utaratibu wa viongozi wetu wakitembelea taasisi huandaliwa hotuba na hiyo taasisi. Hata hivyo siku hiyo Mkapa hakutumia ile hotuba aliyoandaliwa na chuo na alitoa hotuba kali sana ambayo kila mtu ilimwacha hoi. Kwa hiyo pamoja na kuwa na mwandishi wa hotuba, lazima mtoa hotuba naye aweze kuihariri. Bila kuhariri utaisoma kama kasuku na utapwaya. Ndo haya mzee mwinyi alichemsha alipokuwa chancellor UDSM katika graduation moja. katika kutunukuu shahada alipoona BSc Eng. yeye akasema 'Nakutunukuu Bachellor of Science in English' watu weweeeee! Yote haya ni tatizo la kukariri bila kuhariri!

At the end of the day, when it comes to being a leader, constructive ideas matter. All great speech makers had constructive ideas. If a leader cannot make a good speech (like our beloved JK) , the first assumption is that s/he lacks constructive ideas. So the question is Do our leaders have constructive ideas?

Comments: OUR LEADERS DO NOT HAVE CONSTRUCTIVE IDEA, INSTEAD THEY ARE FULL OF DESTRUCTIVE IDEAS AND DEEDS!
 
Jambo Forum ndio ulikuwa moto wa kuotea mbali sasa hivi sioni hivyo tene wanabodi imekuwaje? Naomba ufafanuzi?
 
Wambwanda,
Maneno yako mazuri lakini kidogo sioni uhusiano wake na intellectualism.
Jokakuu alipotuwekea hapa hii mada nadhani alitaka tuzipitie hotuba za hawa watu na kuona tofauti zao...kwa maana ya kusema - Mbingu na Ardhi, lakini mjomba nimeziona kuwa zote ni hotuba za kawaida zilizoandaliwa kulingana na shughuli yenyewe... Hapa sikuona Constructive ideas zozote. Sasa ikiwa zipo hotuba ambazo zinaonyesha tofauti ya hawa watu nadhani itakuwa bora sana tuzione hizo hotuba.
Kisha, mara nyingi unaweza soma hotuba zikavutia sana lakini mtoaji hotuba zenyewe akachemsha kutokana na body language yake kuwa mbaya.
Nimegundua, hawa marais wetu ukiwaondoa Nyerere na Mwinyi, mara nyingi wanapotoa hizi hotuba huwa hawapo huru na mwili wao. Hawafahamu jinsi ya kutumia mikono yao kusisitiza issues, na husimama sehemu moja kama vile askari mlinzi wa Queen. Nyuso zao zina mchecheto kama sii ujeuri. Hii nimeshuhudia wakati wa Mkapa (ujeuri) na JK (mchecheto) - lakini wote huwa wame freeze jukwaani.
Kifupi, ni rahisi kugundua kuwa Mkapa na JK wamekariri hotuba zao na wanatumia nguvu nyingi kukumbuka waliyoyahifadhi kichwani badala ya kuwa huru na mwili wao wakati wakihutubia. Pia, Nyerere na Mwinyi walikuwa mabingwa kwa utumiaji wa hekima na busara ktk kuwakilisha hotuba ili ziwafikie wananchi bila kuwachosha. Tofauti na hawa wajomba wetu.Mkapa alikuwa zero kwa hili, watu huomba saa ngapi atamaliza watu wakijikate.
Kwa hiyo kuna mengi sana ambayo kila mmoja wao ana upungufu (JK vs BWM). Na tunaporudi ktk constructive ideas - BWM alieleweka vizuri kwa wasomi na sio walalahoi. Alikuwa akiongea lugha ya UDSM ama niseme O'bay hali wahutubiwa wengi ni watu wa Kariakoo. Ndio maana hiyo MIKUKUTA na sijui MIKURUKUTA ni vitu visivyoeleweka kabisa....Uwekeshaji bomu kwa hotuba na bomu kweli kiutendaji!... je, alieleweka vizuri?
Mwisho, kama nilivyokwisha sema ktk baadhi ya mada -Tanzania leo hii pamoja na kuwepo na wasomi wengi bado kabisa tunashindwa kuzipeleka message zetu kwa raia walio wengi. Mambo mengi tunaweza kuyazungumza kwa lugha ya kiingereza na mazingira ya Ulaya lakini tunashindwa kuyatafsiri kwa wananchi ktk lugha wanayoifahamu na kuyahusisha na mazingira yetu.
Mathlan, majuzi nilikuwa namfahamisha mtu bongo kuwa rafiki yake mahututi kapelekwa Emergency Department!. Akaniuliza Emergency ndio wapi?.... Ikabidi wife aingilie kati na kunambia - mwambie Casuality!
Hapo hapo nikaanza kufikiri, hivi kiswahili hiki kitengo kinaitwaje?... Dharura!... Je, mkulima wa huko Nzega asiyefahamu hiyo casuality, nikisema Dharura ataelewa msisitizo wangu ama atachukulia dharura kama kitu cha haraka lakini sio muhimu.
Kazi ipo!
 
Mandela, Mahatma Ghandi, Martin Luther King, na Malcom-X, ninaamini ni intellectuals, can you fit Mwalimu kwenye hilo kundi ndiyooooooooooooo!

Je unaweza kumuweka Mkapa hapo kwenye hili kundi, as per Mwanasiasa na IO, na Moshi!


Mzee hapo juu,

Jambo forum ni safi na tunaendelea, tuna-deal na issues as they come, hapa sio Mlimani, au kituo cha polisi, hapa ni Bulogu ya burudani tu na sio mtihani wa form six, na tunaendelea na kumkoma nyani!
 
Mzee Es,
Nyerere anaweza kuitwa mwana-falsafa kama Ghandi, na Martin Luther, kutokana na mchango wake ktk falsafa ya ujamaa na kujitegemea.

Intellectual, mimi naamini ni mtu yeyote yule anayependa kutafiti na kujifunza na ambaye ametoa mchango binafsi wa kitaalamu ktk fani fulani[elimu,mazingira,uhandisi,diplomasia,...]

Mkapa, kwa mtizamo wangu anaingia ktk kundi la intellectual kutokana na tabia yake ya kutafiti, kujifunza, na uandishi. Mkapa ni mwandishi wa vitabu, na makala mbalimbali za masuala ya diplomasia, akiwa Raisi, na kabla ya kuwa Raisi.

NINAJILAUMU kwamba katika kuanzisha mjadala huu wa hotuba za JK nimemlinganisha na predecessor wake BM. Mara nyingi jambo kama hilo huzua MABISHANO, badala ya MAJADILIANO, kutokana na kuingiliwa na WAPAMBE wa kambi mbili husika.

Ninachojaribu kusema ni kwamba hotuba za JK hazifanyiwi utafiti wa kina.Sasa hata kama hukuzifanyia utafiti basi unapaswa kuwa MBUNIFU,CREATIVE, katika kuziandika na kuziwakilisha. Hayo ndiyo mapungufu ya hotuba za JK. Kwa mawazo yangu hazistahili hadhi ya raisi wa jamhuri.

tatizo la BM kutokueleweka kwa walalahoi linatokana na ukweli kwamba mara nyingine hotuba zake zilikuwa za kisomi mno, too intellectual!!! vilevile, BM hakuwa mwanasiasa wa ndani, na hili la kuzungumza mbele ya walalahoi ni suala ambalo alikuja kujifunza akiwa raisi.

JK amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa muda mrefu kuliko wote tanzania. pamoja na uzoefu wote huo, kwanini jk anashindwa hata kutoa hotuba fupi, yenye ubunifu, katika hafla ndogo kama dhifa ya taifa?
 
Jokakuu,
BWM alikuwa akitumia sana kitabu, ELIMU yake badala ya uwezo wake wa kujieleza kama rais na MBUNIFU. Ubunifu sio kuiga elimu ya darasa ktk mazingira tofauti hiyo haiwezi kuwa intellectual..
Nyerere aliweza kutumia Elimu ktk lugha ambayo mwananchi wanaielewa, matani na ubunifu ambao mlalahoi aliweza kuona mwanga mbele anakokwenda. tatizo la Nyerere lilikuwa ukamilishaji wa hayo malengo.... mfumo ulikuwa bomu na sera zke bomu hazikulingana na mazingira yetu pamoja na kwamba alieleweka vizuri.
 
Mkandara,
mimi nadhani ungekuwa sahihi zaidi kama ungesema BWM hakuwa mwanasiasa. yaani mara nyingi, katika hotuba zake, alishindwa ku-connect na wananchi wa kawaida.

BWM ni intellectual hilo halina ubishi. mchango wake katika uandishi wa vitabu, na majarida mbalimbali ya foreign relations unajulikana. katika uandishi huo huwa anaandika kwa kuzingatia utafiti.

kwa upande mwingine, naomba tuangalie CONTENT ya hotuba za JK. kwa mtizamo wangu hayuko creative kwa kutumia misamiati yenye kuongeza MSISITIZO, UZITO, MVUTO, na USHAWISHI, katika yale anayoyazungumza.

mambo hayo manne, na muhimu mno katika hotuba za kiongozi yeyote yule.
 
Jokakuu: Huyu ulimwelezea hapo juu ni academic rather than an intellectual. Intellectual is an academic who dicusses ideas in a public arena and for the benefit of the public. An academic is someone who undertakes academic activity for scholarship and academic purposes such as promotion, etc. Yaani tunaweza tukawa na academics (wanataaluma) wengi, lakini intellectuals (wasomi) mara nyingi ni wachache sana. Kwa mfano pale UDSM tuna maprofesa chungu nzima lakini tuna intellectuals kiduchu sana. Mfano wa intellectuals ni kama kina Chachage Marehemu), Haroub Othman, Baregu na Shivji. Yaani, ni mtu anayependa kujadili (debate) ideas zina manufaa kwa jamii. Ndio maana Nyerere ana-fit vizuri katika hili. Kwa maana hiyo watu kama Mkapa, Kikwete na Mwinyi watoe haraka sana katika kundi la intellectuals. Wote hawa walikuwa na ni woga sana wa kujadiliana. Yaani wanaogopa debate mno.

Ila kutoa hotuba nzuri na inayovutia sio lazima uwe intellectual japokuwa kuwa intellectual inasaidia sana kutoa hotuba nzuri. Tuendelee na mjadala.
 
Wanabodi,

1. Naona wengi mmeuona huu upungufu wa hotuba za JK kama nilivyowahi kuchangia huko nyuma na kumshauri atafute Mwandishi mwingine mahiri au yule aliyepo "ajifue zaidi" (ndiyo maneno niliyotumia).
BTW, ninavyokumbuka mimi, mwandishi wa hotuba wa BM alikuwa Balozi Tuvalo Manongi (alipelekwa UN na BM kabla hajaondoka madarakani-kama ni shukrani sijui! Kama pia alivyompa hadhi ya ubalozi Bw Kallaghe mwisho mwisho wa madaraka yake).

2. Huenda mifano ya hotuba za kwenye dhifa si mizuri sana kwani kwa kawaida, na inafahamika na hata kufundishwa hivyo kwenye diplomasia au uhusiano wa kimataifa, kuwa kwenye dhifa za kitaifa huwa ni "maneno maneno ya kusifiana, ili msiharibiane hamu ya kula na kunywa"; naweza kusema hapo blah blah inaruhusiwa. Hivyo huwa hakuna ujumbe mzito; hapo si mahala pake. Hata hivyo, pamoja na muktadha huo, binafsi ningependa kusikiliza hotuba yenye kuvutia na kuchangamsha; isiwe kavu, iwe na misemo miwili mitatu, na hakika ikiwezekana ikumbukwe siku zijazo, hata kama ilitolewa kwenye dhifa ya kitaifa.

3. Kama taifa, tuangalie uwezekano wa kuingiza kwenye mfumo wa elimu yetu namna ya kuwajengea uwezo watu wetu (wanapokuwa wanafunzi) namna ya kuongea kwenye hadhira mbalimbali (public speaking) kwa kujiamini. Tuliosoma zamani nakumbuka mambo ya "debate" mashuleni. Siku hizi ni shule chache tu wanafanya hivyo, sana sana hizo "academy" au "international schools" za Bongo. Kwa ujumla, binafsi naona tuna tatizo kubwa sana la "effective public speaking", kuanzia kwa wengi wa wahadhiri wetu mpaka hao wanasiasa. Kwa mtazamo wangu, hata mapadri na wachungaji wengi siku hizi hawana hotuba/mafundisho ya kuvutia kama ilivyokuwa zamani.

4. Binafsi, namuona BM kama "intellectual" (japo halikuwa lengo la mchokoza mada kujadili hili, lakini maadam limetokea ngoje tutoe hisia zetu!). Hii ni kutokana na hotuba zake hasa zile za kuandikwa rasmi. Bila shaka ndiyo maana alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Uandishi (Doctor of Letters) pale Open University of Tanzania. Nina mpango wa kukusanya hotuba zake ambazo zilichapishwa kama kitabu ili niwe nazipitia tena na hata "kuzifanyia shule".

Nimewahi kuwasikia baadhi ya maprofesa wa hapa Dar pia wakikiri kuwa BM ni "kichwa", msomi, na hazina kubwa ya taifa. Bila shaka ndiyo maana jamaa wa nje wanamtumia.

Nimewahi pia kuhudhuria hafla wakati BM akihutubia. Hakuwa mkavu sana; hakika alichekesha/kufurahisha hadhira kwa maneno yake. Na hapo alikuwa tofauti na hotuba alizokuwa anasoma za kila mwisho wa mwezi. Nyingi ya hizo zilikuwa kavu sana. Kwa ujumla pia nadhani BM alibadilika na akawa mahiri zaidi kadri alivyokaa madarakani. Huenda JK naye atakuja kuwa hivyo.

Pamoja na kumuona BM kama "intellectual" sina hakika kama alikuwa kiongozi mzuri. Sana sana alikuwa mtawala Mpaka sasa naamini kuwa mtu anaweza kuwa "intellectual" lakini asiwe kiongozi au mwanafalsafa. Wachache wanajaaliwa vyote, na hao ndio kina Nyerere na Ghandhi.

Mwisho, kama nilivyomshauri JK huko nyuma, aachane na ufunguzi wa mikutano na makongamano na warsha na semina "ndogo ndogo". Ahudhurie ambazo ni za muhimu kisera au kimkakati, ambazo kwazo, atatoa ujumbe mzito kwa taifa au jumuiya ya kimataifa. Vinginevyo ndiyo maana atakuwa anaishiwa maneno, anaonekana mwepesi.
 
Mwanagenzi,
Naafiki kabisa para yako ya mwisho. JK aachane kabisa na haya ya ufunguzi wa shoprite za Ubungo na warsha ndogo ndogo. Awatume mawaziri wake wafanye hiyo kazi. Pia atumie muda wake mwingi akisoma kama alivyofanya Mkapa. Angefanya hivyo asingepata ile aibu ya kuhoji "Darwin's Nightmare" wakati hajaiona hata filamu yenyewe. Aaachane na cheap populism.
 
Jasusi: Umenimaliza, hivi kumbe huyu bwana alikuwa hata hajaiona ile picha ya Darwin's nightmare? Basi bwana..
 
Jokakuu,

Ukisema BWM ni intellectual na hakuna ubishi basi mshikaji sina zaidi kwani hapa tuna tofauti ya tafsiri. Kuwa mwandishi wa habari haihusiani kabisa na intellectual nadhani Mwanasiasa katupa picha nzuri zaidi.
Kisha kumbuka kule Bsctimes wakati wa uongozi wake sote tulikuwa tukisema BWM hana vision... na mtu asiyekuwa na vision mara nyingi hawezi kuwa mbunifu.... Kifupi kila kitabu alichoandika BWM ni maelezo ambayo yanapatikana ktk vitabu vya elimu. Hawezi kabisa kuongea kitu nje ya kabati na akibanwa huwa mwepesi wa kuchukia kwani hana explanation zaidi ya zile zilizoandikwa kitabuni.
Mwisho, nadhani hapa tusipotee na kufananisha watu wala isije eleweka kuwa nampaka BMW na kumfagilia JK.
JK simjui hivyo ktk hotuba zake zaidi ya kumwona siku ile pale sokoni akiuza nchi yetu. Nilichogundua ni kuwa alikuwa na mchecheto kasimama kama askari, body language yake mbovu pia majibu yake yalikuwa mepesi sana kuwavuta wawekeshaji ambao wanaogopa kuwekesha Afrika acha mbali kuwa huku wengi hawaifahamu Tanzania.
Mkapa namfananisha sana na Karamagi, wasomi wazuri wanaoweza kutumia kitabu kuonyesha uuwiano fulani tofauti kabisa na mtu kama Maghembe (Mali asili na Utalii) ambaye anaweza kuchanganya lugha ya mtaani na darasani kuwapa picha zinazofanana.
Hawa wote kiboko yao ni Freeman kwani mshirika huyu hajambo anaijua kazi yake.
 
Mkapa, hawezi kuwa intellectual wakati yeye alikuwa muandishi wa habari wa magazeti chama kinachotawala, katika enzi za utawala wa chama kimoja, yeye alikuwa akiandika propaganda za akina Sozigwa, tu na sio maoni yake hata siku moja!

Sasa anakuwa rais waandishi wanapoandika maoni yao binafsi, anaita wote wapumbavu, na kwamba ni waandishi wa upinzani, hivi kweli this makes the man intellectual? Mkapa amebuni nini? kutuletea viongozi mabomu kuliko yeye na kuwaomba mapadri watuambie kuwa rais ni nabii wa Mungu?

I mean hivi ndugu zangu mara ya mwisho mliondoka lini bongo? Maana Mkapa amebuni nini? Halafu hebu tuwekeeni the best hotuba yake hapa, ili tuichanganue na kui-relate na maisha yetu bongo jinsi alivyoyakuta na alivyoyaacha, tuone huu u-intellectual wake unaingilia wapi na kutokea wapi?

Wabongo tunaendelea kulala kwenye giza, viwanda havifanyi kazi, wanachi ajira inazidi kupungua maana viwanda havifanyi kazi, Mkapa yuko huko majuu anazunguka tuuuu, juzi alikuwa Tunisia, leo yupo Geneva anatoa hotuba tuuu za "u-intellectual",

ametuachia viongozi bomu ambao wanathubutu hata kusema hadharani eti wamebeba matatizo yaliyoaachwa na awamu zilizopita, na masikini ya Mungu hatuna waandishi wa habari wa kuwauliza mbona Lowassa alikuwa waziri wa maji, na Jk alikuwa waziri wa nishati wa awamu zilizopita wanazozilaumu, sasa wao si ndio walipaswa kuwa na majibu, maana hayo ndio maneno Mkapa anyasema in private, kuwa si wao ndio walikuwa mawaziri wa hiyo sehemu wanalia nini, yeye Mkapa na hawa viongozi wapya wote wasaniii na hakuna intellectual kati yao, angalau Sokoine ninaweza kusema alikuwa intellectual,

Biblia inasema maneno bila matendo ni bure mbele ya Mungu!
 
Nadhani JK bado yupo kwenye "Learning curve". Ile hotuba aliyoitoa kwenye miaka 45 ya uhuru ni uchafu mtupu. Kwa kawaida hotuba inatakiwa iwe na utangulizi ambao unaandaa hadhira kusikiliza nini utasema. Pili unatoa kile hasa unachotaka kusema halafu unahitimisha. Ili kuepuka kukosa hayo wengi wa viongozi makini huandika na kusoma hotuba zao. Hotuba za JK hazina mtiririko, unaweza kusikiliza mwanzo hadi mwisho huwezi kupata anataka kusema nini. Anahitaji mwandishi mzuri na mahiri na aachane kuimbisha watu nyimbo kwenye mikutano ya serikali, anatakiwa atofautishe CCM na Serikali.
 
Back
Top Bottom