Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

 • Ndio

  Votes: 13 15.5%
 • Hapana

  Votes: 71 84.5%
 • SIJUI

  Votes: 0 0.0%
 • Sina jinsi

  Votes: 1 1.2%

 • Total voters
  84
 • Poll closed .
Unfortunately hotuba zote mbili naziona karai tu; hakuna yenye quotable quote ingawa kidogo Mkapa alitumia sentensi stronger kuliko Kikwete, labda kwa vile yeye alikuwa mwandishi wa habari.

Mtemi wao kwenye hotuba alikuwa ni Nyerere tu ambaye kila hotuba yake ilikuwa na elements za philosphy kiasi kuwa alikuwa hakosi kuacha quotable quotes. zaidi zaidi alikuwa hasomi labda iwe na mahali kama umoja wa mataifa amabao wanataka kopi ya hotuba in advance.
 
An intellectual is a person who is fascinated by ideas. Mkapa was (and still is) an intellectual while JK is not. It is unfair (to JK) to compare him with Mkapa.

We owe it to ourselves, as a nation, to give JK an intellectual who will write his speeches. It is not good enough for a couple of friends to do his speeches for him. Presidential speech writing is too important to be left to friends.

Augustine Moshi
 
I agree with you Moshi by 100%. I only need to add that making a great speech requires intensive and extensive reading. This guy, as far as I am aware, never reads serious stuff, and so are many of his aides. Without reading where can he get ideas? Hata hao wasaidizi wake wanaomwandikie speech wameshajua boss wao anapenda speech za uswahili uswahili basi wanamuandikia ki-uswahili uswahili hivyo hivyo!
 
JK ana hitilafu, siku ya uhuru alitoa hotuba mbovu kabisa niliyowahi kusikia toka kwa kiongozi wa nchi. Haonyeshi kama mtu mwenye uelewa wa mambo.

Ile hotuba aliotoa wakati wa ufunguzi wa bunge nadhani aliandikiwa na akakarishwa vizuri,maana baada ya hapo amekuwa akichemka tu. Fikiria ile hotuna aliyozungumzia Darwin's nightmare, akaja kupia ile aliyo zungimzia real madrid(akizungumza na wahariri) hii ya uhuru funga kazi. Alafu alimalizia kwa kusema Kidumu chama cha Mapinduzi! Sidhani kama alikuwa analihutubia taifa.

Na shaka sana na uwezo wa raisi wetu.
 
nikimnukuu mtangazaji Mambo Mbotela, HIVI HUU NI UUNGWANA JAMANI!! JK ameutafuta, na kujiandaa kwa, Uraisi tangu mwaka 1995, halafu unakuja ku-perfrom vibaya kiasi hiki?!

kutoa hotuba ndiyo jambo rahisi kupita yote ktk kazi za raisi. na hotuba niliyowaletea hapa ni hotuba ya kujitambulisha, ambayo ndiyo rahisi kupita zote. lakini tunaona jinsi jk anavyochukulia kazi yake kimzahamzaha.

Dr.Moshi,
nasema hapana kwa maoni yako hapo juu. kila jk anapokosea mnadai ameshauriwa vibaya, mnaleta kila aina ya visingizio. wakati umefika kwa jk kubeba msalaba wake mwenyewe.

jk, alikuwa akijulikana tangu aanze uongozi kwamba si mtu makini hata kidogo. hakuwa mtu aliyependa kujisomea au kujifunza. akiwa waziri alikuwa na tabia ya kuchelewa hata ktk miadi ya kikazi. wakati huo atleast alikuwa na wakubwa wa kazi wa kumsukuma sukuma. sasa hivi yeye ndiye mkuu wa kazi, na matokeo yake ndiyo haya.

mwanasiasa, ongara,
.....ukisoma hotuba aliyotoa kigali, halafu ukafuatia na ile ya kampala, unaweza kulia kama mtoto mdogo. yaani ni uoza mtupu.

ukiendelea mpaka hotuba ya majuzi kwa makamanda wa jeshi uganda utajua kwamba jk anatoa hotuba kwa kusikiliza mambo ya vijiweni, na siyo kufanya utafiti. s
 
Jamani ebu nipeni darasa hapa.
JK kachemsha wapi? na BM kazungumza lipi lenye uzito zaidi. Maana ke kwangu hotuba zote mbili zinafanana kwa aina fulani, tofauti ni wakati na mission yenyewe. Wote wanashukuru kwa chakula, ujirani na undugu.... Sioni kinachompa sifa BM kabisa kwa sababu hizi zote ni sifa za ugeni kumsifia mwenyeji wake. Kitu gani hasa alitakiwa JK kukizungumzia ambacho kimewavutia ktk hotuba ya BM.
 
Jamani ebu nipeni darasa hapa.
JK kachemsha wapi? na BM kazungumza lipi lenye uzito zaidi. Maana ke kwangu hotuba zote mbili zinafanana kwa aina fulani, tofauti ni wakati na mission yenyewe. Wote wanashukuru kwa chakula, ujirani na undugu.... Sioni kinachompa sifa BM kabisa kwa sababu hizi zote ni sifa za ugeni kumsifia mwenyeji wake. Kitu gani hasa alitakiwa JK kukizungumzia ambacho kimewavutia ktk hotuba ya BM.

Afadhali Mkandara tusaidiane huu mzigo.

Mimi naona kabisa hotuba zote mbili ni za aina moja. Tofauti ni kuwa sentensi za Mkapa ni structurally stonger zaidi ya zile za JK. Hata hivyo hotuba zote mbili hazina philosophical lesson yoyote ndiyo maana zinakosa quotable quotes. Kama zingekuwa ni term papers, labda ningewapa makarai kwa kudemand kuwa wawe wanakuwa philosophical kidogo katika hotuba zao.

Inawezekana kuwa kwa kuchanganya hotuba zote alizowahi kutoa JK na na zile za BWM kuna upungufu sana katika hizi za JK: kwa mfano kudai kuwa Tokyo kuna majambazi wavunja nyumba inaonyesha kuwa hafanyi research yoyote wakati wa kutayarisha hotuba zake. Sikusikia hotuba hizo nyingine za Uganda, Uhuru na za wanajeshi, lakini hizi za Kigali hazionyeshi tofauti yoyote kabisa, kumbuka kuwa wote walikuwa mbele ya msosi.
 
Eti Mkapa ni what? Wewe Moshi lazima ni Mchagga, yaani ndugu ya mke wa Mkapa, I mean in your eyes MkAPA is almost an-angel? WHY?

Mkapa anakuwaje intellectuall, alipotutanganzia kuwa atapigana na rushwa to the core, akampa kamati rafiki yake Warioba kuchunguza rushwa, kamati ilipomkabidhi akaanza kugombana na wabunge waliotaka waliotajwa wawe prosecuted, leo Mkapa na Warioba ni maadui wakubwa mno maana Warioba, anasema Mkapa ni mla rushwa namba moja,

Again, kamati ya bunge ikasema Idd Simba, amekula rushwa kwenye hela za sukari za jeshi, Mkapa akagoma kabisa kumuwajibisha, na alipolazimishwa na kina Dr. Mzindakaya, akawatukana ile mbaya na hasa Dr. Mzindakaya kuwa ni wapumbavu,

Waandishi wa habari wa bongo ni wapumbavu as far as Mkapa is concerned, maofisa wote wa foreign Affairs hawajui kuandika English as of Mkapa, isipokuwa Mchagga Palangyo, maji ya Mtera yameisha under his watch,

leo ni the private analia kama mtoto, akiwalaumu Kikwete na Lowassa kuwa hawawezi kazi, juzi bila kuitwa aliposikia rais yuko Massasi naye akaja na kummiminia sifa kibao mbele ya public,

Halafu mnasema huyo Mkapa, ni intellectual, mtu si unakuwa intellectual kutokana na maneno na matendo yako, au? Kwa hiyo mtasema Mwalimu ni intellectual so is Mkapa naye? Yaani hiyo sio kumvunjia heshima baba wa taifa? Yaani huyu Mkapa hata nyumba kwao Massasi hana, anaishi kwa Mapadri akija huku, lakini kajenga Lushoto karibu na kwa mke, eti mnasema huyu ni intellectual?

Hebu tusaidiane kuelewa ndugu zangu?
 
Mzee Es,

Afadhali umeyasema wewe!...
Binafsi nimefurahishwa sana na kipande hiki cha hotuba ya Lowassa bungeni.
Uongozi una maeneo mengi, lakini moja na la muhimu ni sifa zinazomuwezesha kiongozi kukubalika kwa anaowaongoza. Aidha, uwezo wa kufikiri, uwezo wa kujieleza, uwezo wa kuimudu kazi yake na kuelewa matokeo ya maamuzi anayoyafanya na jinsi yatakavyopokelewa na wanaoongozwa. Kuwa kiongozi mzuri inasaidia kuwa mtawala mzuri pia. Mwandishi mmoja Robin Sharma aliandika kuhusu alichosema Woodrow Wilson kuhusu viongozi, nanukuu:
"You are not here to merely make a living. You are here in order to enable the world to live more amply, with great vision, with a finer spirit of hope and achievement. You are here to enrich the world, and you impoverish yourself if you forget the errand".

maelezo safi lakini sidhani kama huyu msera ni intellectual!...
 
Mzee Bob,

Ninakusikia, yaani watu kama Mahatma Ghandi, Nelson Mandela ninaweza nikaelewa kuwa ni intellectuals, kutokana na maneno yao na vitendo vyao, na waliweza kuyabadili mazingara waliyoyakuta, kutokana na maneno yao na vitendo,

Watu kama Martin Luther King kule US, kina Malcom-X waliojifunza kusoma wakiwa jela, wakatoka na kufanya vitu vikaonekana, yes, lakini kutumia hela za nji yetu kwafurahisha wafadhili, halafu ukiaacha urais wanakupa fadhila ya wema wako kwa kutumia hela za walipa kodi, kwa kukupa kazi huko nje, yaani kwao wazungu, huku nyuma umeacha wananchi hawana umeme wewe unaruka tu majuu, halafu unakuwa intellectual!

Mkapa sio intellectual, tusiharibu maana ya maneno ya watu jamani!
 
Tusichanganye mambo.
Kuwa 'intellectual' na kuwa kiongozi mzuri ni mambo mbalimbali.
'Intellectual' haina maana mtu si mpokea rushwa. Tuseme 'intellectual' anaweza kuwa na uwezo mzuri wa kuyachambua mambo na kuyawasilisha; kwa mfano kwa kutoa hotuba zenye nasaha. Kwa hiyo tupime u-intellectual wa viongozi wetu hawa kwa mantiki ya hotuba zao walizozitoa, na sio kwa kigezo cha uzuri wa uongozi wao.
 
Kwa hiyo kama ninakuelewa, Mkapa ndiye riais wa kwanza duniani aliyewezakuwa shujaa wa hotuba lakini akashindwa kuzitekeleza, lakini anapaswa kuwa intellectual, maana alikuwa shujaa wa hotuba tu?

Anyway hotuba za rais Mkapa zilikuwa zikiandikwa na nani? Yeye au Kalaghe?
 
Ndg Wanabodi,Nimefurahi kuona kuwa kumbe kuna wengi wanaoona ukweli!.,Awamu hii ya Nne iliingia kwenye madaraka kwa ahadi nyingi na kubwa kubwa,lakini sasa inaonekana kile walichokisema wanashindwa kukitekeleza na wanakuwa wakali na majibu ya kihuni. Hapa nanukuu "Tatizo la umeme tumeliridhi kutoka kwa awamu zilizopita",au kutoa kauli za uongo kama."Hata Tokyo kuna majambazi wavunja nyumba,kwa hiyo ujambazi Tanzania si kitu cha ajabu" au "Huko New York kila dk kuna mtu anauawa na wahalifu/majambazi".Jamani Mtukufu Rais, ukiombwa statistics unaweza kutoa?Bado sijajua nani ni washauri na waandishi wa speeches za huyu Bwana,najua Kallaghe yupo hapo na juzi tu Bwana Kilumanga Chabaka kaenda kwenye timu hiyo.Nitasikitika sana kama kweli Januari Makamba ni mmoja wa waandishi wa karibu wa JK,kwa sababu naamini wazi kuwa Uandishi si kujua English tu, inabidi kujua mambo mengi kitaifa na kimataifa,na kumfanya JK kuwa comfortable kwenye mazingira yoyote anayotoa hotuba kutokana na viwango mbalimbali vya Elimu vya wapokea hotuba hiyo!Kupiga Bla Bla kama ktk hotuba aliyotoa kigali kunapunguza heshima ya nchi.Imefika kipindi sasa kinachosemwa kifanyike na sio kutoa Hotuba zisizokuwa na ukweli ili kupata umaarufu kisiasa."Huwezi kusema kuwa nikipata Urais nitaanzisha Mahakama za kiislamu kwenye Taifa lenye dini zaidi ya mbili" Nataka kujua hapa inakuwaje ikiwa Rais anapoteza uwezo wa kuongoza?kwa nini kusiwe na impechment?Watanzania lazima tuamke, na tusiwe watu wa kuishi kwa hopes za hawa Wababaishaji,wanaokuja kutafuta uongozi ili kutunisha mifuko yao.
 
Better put this way:
JKN: Alikuwa Intellectual + Had charisma
BWM: Intellectual - minus Charisma
JK: Kwa muda mfupi aliokaa hapa IKULU hana vyote! Ni kweli mtoto wa mjini.
 
Mzee Bob,

Ninakusikia, yaani watu kama Mahatma Ghandi, Nelson Mandela ninaweza nikaelewa kuwa ni intellectuals, kutokana na maneno yao na vitendo vyao, na waliweza kuyabadili mazingara waliyoyakuta, kutokana na maneno yao na vitendo,

Watu kama Martin Luther King kule US, kina Malcom-X waliojifunza kusoma wakiwa jela, wakatoka na kufanya vitu vikaonekana, yes, lakini kutumia hela za nji yetu kwafurahisha wafadhili, halafu ukiaacha urais wanakupa fadhila ya wema wako kwa kutumia hela za walipa kodi, kwa kukupa kazi huko nje, yaani kwao wazungu, huku nyuma umeacha wananchi hawana umeme wewe unaruka tu majuu, halafu unakuwa intellectual!

Mkapa sio intellectual, tusiharibu maana ya maneno ya watu jamani!


you get my full support on this note. Inaelekea watu tumeanza kutia maji sifa ya intellectualism; haitokani na kukaa shuleni tu, na wala haitokani na wingi wa wapiga debe. Sifa hii inatokana na jinsi mtu anavyotumia intellect yake katika mambo anayofanya, ikiwa ni pamoja na kwenye mikataba ya serikali. Mikataba aliyoacha Mkapa haionyeshi kama alikuwa anatumia intellect yoyote katika kuifanyia maamuzi. Kama Mkapa ni intelectual kweli basi viongozi wote waliokuza uchumi wa nchi zao ni intelectuals including Tony Blair na George Bush. Acheni utani jamani.
 
Kama maana ya intellecual ni hii "a person who uses the mind creatively"
basi kumwambia Mkapa kama rais alikuwa intellectual ni kupoteza maana ya neno lenyewe. Labda Mkapa kama Mwandishi wa habari alikuwa na hizo sifa.

Mtu kuwa intellectual lazima kile anachokifanya kiwe na lengo la kuwa na faida kwa jamii. Huwezi kumwita mwizi kwamba alikuwa intellectual hata kama
amefanikiwa kuiba mara nyibgi bila kukamatwa.

Tukija suala la JK nafikiri tatizo ni lile lile la uvivu wa akili kama walivyosema baadhi ya wajumbe. Kuto kujiendeleza kwa kusoma vitabu na makala mbalimbali. Hata uwe na waandishi wazuri kiasi gani, hotuba nzuri ni zile ambazo mtoaji anajua anaongelea nini. JK lazima aelewe anataka kuongelea nini na hapo ndipo hao waandishi wazuri wanaweza kumsaidia. Pia kwasasa TZ kuna hili la kupeana ulaji, kwasababu ni mtoto wa fulani basi anasogezwa karibu na mzee. Mwandishi wa rais wala sio lazima hata awe mfanyakazi wa Ikulu na badala yake kuna Watanzania wengi sehemu mbalimbali ambao wangeliweza kuwa sehemu ya hao waandishi na mara moja moja wanaombwa kusaidia na kisha rais na wasaidizi wake wa karibu ndio wanaamua hotuba ipi inafaa.

JK inabidi atoke kwenye box na akubali kufanya kazi na watu ambao hawana mizizi ya CCM huko nyuma. Nina maana watu ambao sio lazima baba zao au kaka zao au ndugu zao walikuwa na vyeo ndani ya CCM. Lazima ajitahidi kutafuta uwanja wa kuwapata watendaji wake. watu wa namna hiyo
wanaweza kuleta fresh air kwenye serikali ya JK.
 
Wanabodi ,

Mimi siku zote naamini ya kuwa uandishi ni art . Speech za JK ni nzuri lakini sio katika level ya Rais . Ni kweli kwamba ukiangalia kwa undani speech yake na mkapa zina ujumbe sawa ila ujumbe ulivyowakilishwa ni tofauti kabisa . Wakati ile ya mkapa inaonekana ya kuwa mwandishi alikaa chini na kuiandika ya kikwete inaonyesha mwandishi akufanya hivyo.

Lakini hata hivyo tatizo sio la mwandishi peke yake kwani hata yeye Jk azireview hizi speech na kuzirekebisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom