Hotuba ya Rais Obama yawaliza wengi

Hotuba ya Rais Obama yawaliza wengi

Okey...nimekuelewa mkuu.
.....halafu mbona siku hizi hautupii vile vitu pendwa jukwaa lile historia
Hata hivyo hawa wanaonipa pesa ya mkate wa kila siku wamenibana kiaina ninaingia JF kwa machale mkuu majukumu ni mengi.
 
Sky Eclat said:
Mbona leo tu nimeweka hitoria ya dhifa (banquet).
My bad...sijatembelea leo mkuu...nimekurupuka tu na kulaumu...same he Mara saba sabini mkuu
 

Rais Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa kama rais wa Marekani, huko Chicago hotuba ambayo ilijaa hisia kali na kupelekea kutokwa na machozi yeye pamoja na baadhi ya watu.
Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
"Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.
Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani".

Amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".
Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.
Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55.

Michelle Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi

Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.

Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake.

Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake.
Mbona Mimi haijanitoa machozi wandugu
 
Kuna watu wanakuja na ushabiki maandazi Hapa eti alimuua Ghaddafi. Issue ya Ghaddafi aliikuta ule ilikuwa ni utekelezaji. Ni agenda ya Republicans. Mjaribu kusoma na kufuatilia international news mtajifunza mengi sio kukurupuka. Bush aliondoka watu hawakumlilia. Kuna baadhi ya watu wanataka aendelee kuongoza Marekani. Good Job Obama! The world will miss you! Kapumzike umeyafanya mengi mazuri hata kama yapo mabaya ni machache nawe ni mwanadamu una mapungufu. Great President in USA!
Usidanganye watu nani anae taka aendelee kuongoza ile ni nchi ya ki democracy ukiisha mda wako unampisha mwengine kuhusu kulia tazama kwenye mkutano mzima alie lia ni yeye na makamu wake wa rais na bintie binafsi naona anawalilia maelfu ya watu aliyo wauwa Iraq na Syria a.k.a is a.k.a daesh Bila kusahau Libya na Yemen
 
Binafsi nilimpenda ila alipojiingiza LIBYA na akajuta lakini akajiingiza SYRIA kwa kuwasapoti Magaidi ya IS ambayo yamefanya unyama wa kutisha na lengo ilikua kumuua Rais wa SyRia Assad Nilimdharau sana isingekua PUTIN tungekua tunaona habari nyingine Syria za ajabu kabisa Nampongeza PUTIN kwa kumuondoa Bibi Kizee Yule Clinton maana Akili zake zilikua ajabu sana zaidi ata za OBUMA....
 
Hajajutia kumuua Ghadaf katika hotuba hii, nilitegemea atuombe radhi Waafrika kwa kutuvamia na kumuua kiongozi wetu, amesababisha madhila mengi kwa raia wa Libya..hatakua na Amani atateseka sana moyoni kwa ukatiri ule waliofanya Libya...Mungu amlaze Pema kamanda Muamar Ghadaf...
 
Hollywood kazini minafiki sana hiyo mijitu Obama ulishiriki kumuua Gaddafi bila kosa kapumzike ila najua tu Damu ya Gaddafi itakulilia hebu tazama Libya ulivyoigeuza kutoka mwamba mpaka imekuwa mchanga
Na bado huko syria.
 
Kuna watu wanakuja na ushabiki maandazi Hapa eti alimuua Ghaddafi. Issue ya Ghaddafi aliikuta ule ilikuwa ni utekelezaji. Ni agenda ya Republicans. Mjaribu kusoma na kufuatilia international news mtajifunza mengi sio kukurupuka. Bush aliondoka watu hawakumlilia. Kuna baadhi ya watu wanataka aendelee kuongoza Marekani. Good Job Obama! The world will miss you! Kapumzike umeyafanya mengi mazuri hata kama yapo mabaya ni machache nawe ni mwanadamu una mapungufu. Great President in USA!
Bure kabisa wewe.. yaani unajaribu kumtoa kuhusu Libya, halafu unasema issue aliikuta alichofanya yeye ni utekelezaji

Sasa utekelezaji wa nini kama si mauaji..!
 
Back
Top Bottom