Hotuba ya Rais Obama yawaliza wengi

Hotuba ya Rais Obama yawaliza wengi

Bure kabisa wewe.. yaani unajaribu kumtoa kuhusu Libya, halafu unasema issue aliikuta alichofanya yeye ni utekelezaji

Sasa utekelezaji wa nini kama si mauaji..!
Sorry mkuu kuna sehemu nimevuruga kidogo utaona ila ni makosa ya kiufundi
 
Kuna watu wanakuja na ushabiki maandazi Hapa eti alimuua Ghaddafi. Issue ya Ghaddafi aliikuta ule ilikuwa ni utekelezaji. Ni agenda ya Republicans. Mjaribu kusoma na kufuatilia international news mtajifunza mengi sio kukurupuka. Bush aliondoka watu hawakumlilia. Kuna baadhi ya watu wanataka aendelee kuongoza Marekani. Good Job Obama! The world will miss you! Kapumzike umeyafanya mengi mazuri hata kama yapo mabaya ni machache nawe ni mwanadamu una mapungufu. Great President in USA!
Hapo umenena! Amefanya mengi mazuri
 
Wewe uko nyuma ya dunia,sadam kafa lini?
Mangi Instagram simpati ana tatizo gani?

Rais Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa kama rais wa Marekani, huko Chicago hotuba ambayo ilijaa hisia kali na kupelekea kutokwa na machozi yeye pamoja na baadhi ya watu.
Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
"Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.
Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani".

Amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".
Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.
Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55.

Michelle Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi

Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.

Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake.

Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake.

Warmonger , monster bullshit kaiumiza mashariki ya kat alafu Leo anajitia kulia.

Nitasubiri utakapotuwekea clip hapa. Uwezo wa luninga kwa wengine una sua sua.
 
mkuu huna kaseti yake tusikilize?
 
Ah wapi,ameshindwa kututuliza sisi waislamu tunauana huku mashariki ya kati,Syria,lebanon,Iraq bali yeye anaenda kusulihisha nchi za kikristo na wakati anakua fika kabisa nchi zetu za kiislamu tukipata tatizo tunaomba Marekani watusuluishe.
 
Bibi nae binadamu, sijui kwa nini mnamuonaga kamamgumu fulani. Ni wa kike na mlaini wa moyo kama usowe!
Iwekeni hapa tusikilize, tuone kama na sisi tutalia. Mpaka Faiza Foxy Kalia? Duuh! Hakika ilikua ya Kugusa.
 
Hollywood kazini minafiki sana hiyo mijitu Obama ulishiriki kumuua Gaddafi bila kosa kapumzike ila najua tu Damu ya Gaddafi itakulilia hebu tazama Libya ulivyoigeuza kutoka mwamba mpaka imekuwa mchanga
simpendi kbsa huu jmaa na Clinton
 
JF inaharibika kwa sababu ndugu zetu waleee. . , wanachangia humu kwa "HISIA" ..., na sio kwa uelewa wa mambo dhahiri yaliyotokea na yanayotokea Duniani ... Ni aibu kukurupuka tuu na kusema mambo hasi ya nchi kama Marekani kwa vile eti umesikia tuu imaam, Sheikh au Padri wako amesema . . Kama unaijua lugha ya kimombo vizuri .., na umesikiliza hotuba ile ..., kwa kweli huna sababu ya kupinga kuwa ilikuwa ni hotuba nzuri sana, and it was so moving emotionally....
Kama imeweza kumtoa machozi dada yangu mgumu, mkorofi Faiza . . , unaweza kuhisi ilikuwaje . .

Obama ni Raisi atakayekumbukwa sana muda mrefu ujao na wamarekani wengi , hasa wenye akili . .
 
Mkuu, hayo unayoyaona makubwa yamefanywa na obama ndo yamesababisha trump kumpa uraisi kwa kuahidi kufuta yote, trump kwenye kampeni zake aliahidi kufuta mambo yote ya obama kuanzia "obama health care"-insurance. Pro-trump wanaamini huyo ndo "weakest president in american history".
 
Mkuu, hayo unayoyaona makubwa yamefanywa na obama ndo yamesababisha trump kumpa uraisi kwa kuahidi kufuta yote, trump kwenye kampeni zake aliahidi kufuta mambo yote ya obama kuanzia "obama health care"-insurance. Pro-trump wanaamini huyo ndo "weakest president in american history".

Waijua ObamaCare?
Mpango wa kupatia maskini wote bima/matibabu ya afya kwa gharama za matajiri.

Kumbuka Republican ni ya matajiri na Democratic ni wa kawaida.

Trump akisaidiwa na matajiri wa Matajiri wasiopenda 'weusi wengi 'ambao ni maskini wakasema kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe.

Sasa ndugu zangu hasa wale watoto wa 'Bwana yulee' kuleta mambo ya sjui kamiu nani,etc hamujielewi!
 
Back
Top Bottom