comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Rais Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa kama rais wa Marekani, huko Chicago hotuba ambayo ilijaa hisia kali na kupelekea kutokwa na machozi yeye pamoja na baadhi ya watu.
Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
"Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.
Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani".
Amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".
Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.
Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55.
Michelle Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi
Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.
Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake.
Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake.