bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,166
- 2,839
KILA RAIS WA MAREKANI LAZIMA AONDOKE NA KICHWA KIMOJA
Unapokuwa rais wa nchi yoyote ile ni kwamba unafuata kile ambacho watu fulani wanataka ukifuate, unaweza kuja na mipango yako na isifanye kazi.
Unawekewa mkakati kwamba tunakuweka wewe ila tunataka ufanye hili na lile, unatakiwa kufuata hata kama hutaki. Hii ipo kila kona duniani.
Sasa kwa Marekani, unakuwa rais shujaa kama kwenye uongozi wako uliondoka na kichwa cha mtu mmoja. Tangu zamani ipo hivyo ila nikianza kwa George W. Bush utaona kwenye uongozi wake aliondoka na Saddam Hussein.
Akaja Barack Obama, naye hakutaka kuondoka kinyonge, ilikuwa ni lazima uonyeshe kwamba wewe una nguvu sana, akaondoka na Osama na Gaddafi.
Baada ya hapo akaja Trump. Mara nyingi muongo wa pili ndiyo huwa na tukio la kuondoka na kiongozi mmoja kwa Waarabu, kabla hajafika hiyo hatua ya pili, watu wakamtoa, wakamleta Joe Biden.
Huyu pamoja na kuwa mgonjwa, ila akajitahidi kuwafurahisha Wamarekani kwa kuondoka na kiongozi wa Islamic State, Abu Ibrahim al-Hashimi na kiongozi wa Al-Qaeda, Ayman Al Zawahiri.
Baada yake amekuja Trump. Naye anajua kabisa ana miaka minne hivyo ilikuwa ni lazima kufanya kama wanavyofanya marais wengine, naye akaondoka na Ali Khamenei.
Hivi ndivyo wanavyofanya na hata ukifuatilia marais wa zamani wa Marekani huwa ni hivyohivyo. Kwenye tawala zao waliondoka na watu wengi walioonekana kuwa wasumbufu kwenye mitikasi yao.