Hotuba ya Rais Magufuli Vs Freeman A. Mbowe

Hotuba ya Rais Magufuli Vs Freeman A. Mbowe

Wakati Mbowe analihutubuia Taifa na kulionya kuhusu janga linalotishia Taifa la corona

Raisi Magufuli alikuwa bize kulihutubia Kanisa na kuwashawishi waumini waachane na Mabarakoa ya kutisha tisha huku akitangaza ushindi mkubwa alioufikia kwa kuitokomeza corona
 
Tanzania mzima wanajua rais aliongea Jana Ila mbowe ni dar Arusha na dodoma labda huwez mfananisha mbowe na magufuli ki ushawish hata mapenzi kutoka kwa wananch mbowe mtu wa kawaida Sana juzi nimekutana nae maeneo ya town yupo tu Kama raia wa kawaida Tena baadh ya watu walionesha dalili za kuto kumjua fikiria kiongozi Kama mbowe alivyo mkubwa kwenye mitandao Ila mtaan anapanga folen Tena watu wanamkunjia bila kushtuka pia watu walikua hata hawajali alafu eti analendwa na watanzania mbowe lile tukio la juzi lilifanya niamin kwamba hata zile Ela mlizo sema mmechangiwa na wananch Sio kweli
Mbowe Kama atakataa nacho kiongea aje abishe apa Ila juzi tulionana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Elius Ndabila
0768239284


Jana sikupata muda wa kusikiliza hotuba ya Mh Mbowe, lakini leo nimeingia kwenye mitandao hususani mtandao wa twitter. Nikiwa ninapitia kwenye kurasa mbalimbali nimejaribu kuona baadhi ya twitter zilizonukuu hotuba ya Mh Mbowe na nikaona hata ukurasa wa CHADEMA ukiwa umeandikwa Mh Mbowe atalihutubia taifa(jana).


Makala hii fupi haita jikita kuchambua hotuba ya Mh Mbowe kwani sijaisikiliza zaidi ya kusoma twitter, nikisha sikiliza hotuba ya Mh Rais ndipo nitapata wasaa wa kumsikiliza Mh Mbowe. Lakini hapa ninahitaji kupata ufahamu wa pamoja ili kama kuna dhana ya upotoshaji tuikemee?


Ni kweli kuwa Mh Mbowe anayo anayomamlaka ya kulihutubia Taifa? CHADEMA wanapotosha ili kupata attention? Nani mwenye ligalilty na legitimacy ya kulihutubia Taifa?


Nijuavyo mimi, na ninadhani wabobevu wa humu jf mtanisaidia ni kuwa Mh Mbowe anayo mamlaka ya Kuzungumza na vyombo vya habari, Kuzungumza na wanaCHADEMA na kuzungumza na WanaHai lakini hana mamlaka(authority) ya kuzungumza na Taifa.


Mtu mwenye uwezo na mamlaka ya kuzungumza na Taifa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt John Joseph Pombe Magufuli. Huyu popote pale awapo anapozungumza anakuwa anazungumza na Taifa na inakuwa ni sauti ya mamlaka. Ndiyo maana chochote anachoagiza Rais ni sheria. Kwa mazingira hayo kama mwenye uwezo wa kuzungumza na Taifa ni Rais basi maamlaka anaweza kuwa nayo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wasaidizi mbalimbali wa Rais wakiwemo Mawaziri.

Viongozi wa vyama vya siasa hawana uwezo wa kuzungumza na Taifa wala maneno yao si utekelezaji kama alivyo Rais. Wao wanaweza kutumia vyombo vya habari kushauri au kukosoa lakini si KUZUNGUMZA NA TAIFA.

Kuzungumza na Taifa ni neno zito, si neno la mchezo mchezo. Ninadhani ilifaa kusema Mh MBOWE Mwenyekiti wa CDM atazungumza na vyombo vya habari na si kusema atazungumza na Taifa.

Mwisho tuendelee kujikinga na corona kwa kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu.

karibu kuwekeza Ileje. Tunayo ardhi ya kutosha yenye rutuba.

Haya subiri uteuzi
 
utafiti wako bado mwepesi sana. Angalau ungeangalia nani kaongea points juu ya suala zima la usalama wa wananchi
 
Viongozi wa vyama vya siasa hawana uwezo wa kuzungumza na Taifa wala maneno yao si utekelezaji kama alivyo Rais. Wao wanaweza kutumia vyombo vya habari kushauri au kukosoa lakini si KUZUNGUMZA NA TAIFA. Kuzungumza na Taifa ni neno zito, si neno la mchezo mchezo. Ninadhani ilifaa kusema Mh MBOWE Mwenyekiti wa CDM atazungumza na vyombo vya habari na si kusema atazungumza na Taifa.
Alisema atahutubia taifa, na si kuzungumza na taifa. Itakuwa ulimnukuu vibaya
 
Mkuu napata shida kukuelewa, unaongelea uwezo au mamlaka?
 
Na Elius Ndabila
0768239284

Mwisho tuendelee kujikinga na corona kwa kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu.
nimezungumza na mkuu wa idara ya kusifia na kuunga mkono juhudu pale lumumba. kasema kabla ya saa nane mchana, atakuwa tayari kashakuwekea buku7 yako kupitia namba ya simu uliyoambatanisha kwenye bandiko.
 
Baada ya kuona mh raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anawahutubia watanzania, mbowe nae kakurupuka kajaribu kuwahutubia misukule yake,kachekesha sana analialia kulalamika kutia huruma kuomba huruma za watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya magufuli ilikwenda live kwenye vituo vyote vya televisheni na redio,pia ilirudiwa tena saa moja usiku,pia utafiti wako haukugusa channel.ya ikulu mawasiliano.

Ya mbowe ilipatikana vichochoroni,ndio mana ukaona hao 1.3 wamejazana,ukute hao ni wote wa ughaibuni
Yaani katika watanzania milioni 55,unajivunia kutazamwa na watu milioni 1.3!
Mkuu kwenda Live unataka kujustify nini? Sawa wangapi walikuwa interested hizo mubashara? Wangapi baada ya kuona na kusikiliza baada ya dakika chache wakaendelea na shughuli zao.
Wangapi wanawezakuanfalia na kusikiliza hadi mwisho hizo speechi za rais hata wakiangalia You tube!!
 
Back
Top Bottom