Na Elius Ndabila
0768239284
Jana sikupata muda wa kusikiliza hotuba ya Mh Mbowe, lakini leo nimeingia kwenye mitandao hususani mtandao wa twitter. Nikiwa ninapitia kwenye kurasa mbalimbali nimejaribu kuona baadhi ya twitter zilizonukuu hotuba ya Mh Mbowe na nikaona hata ukurasa wa CHADEMA ukiwa umeandikwa Mh Mbowe atalihutubia taifa(jana).
Makala hii fupi haita jikita kuchambua hotuba ya Mh Mbowe kwani sijaisikiliza zaidi ya kusoma twitter, nikisha sikiliza hotuba ya Mh Rais ndipo nitapata wasaa wa kumsikiliza Mh Mbowe. Lakini hapa ninahitaji kupata ufahamu wa pamoja ili kama kuna dhana ya upotoshaji tuikemee?
Ni kweli kuwa Mh Mbowe anayo anayomamlaka ya kulihutubia Taifa? CHADEMA wanapotosha ili kupata attention? Nani mwenye ligalilty na legitimacy ya kulihutubia Taifa?
Nijuavyo mimi, na ninadhani wabobevu wa humu jf mtanisaidia ni kuwa Mh Mbowe anayo mamlaka ya Kuzungumza na vyombo vya habari, Kuzungumza na wanaCHADEMA na kuzungumza na WanaHai lakini hana mamlaka(authority) ya kuzungumza na Taifa.
Mtu mwenye uwezo na mamlaka ya kuzungumza na Taifa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt John Joseph Pombe Magufuli. Huyu popote pale awapo anapozungumza anakuwa anazungumza na Taifa na inakuwa ni sauti ya mamlaka. Ndiyo maana chochote anachoagiza Rais ni sheria. Kwa mazingira hayo kama mwenye uwezo wa kuzungumza na Taifa ni Rais basi maamlaka anaweza kuwa nayo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wasaidizi mbalimbali wa Rais wakiwemo Mawaziri.
Viongozi wa vyama vya siasa hawana uwezo wa kuzungumza na Taifa wala maneno yao si utekelezaji kama alivyo Rais. Wao wanaweza kutumia vyombo vya habari kushauri au kukosoa lakini si KUZUNGUMZA NA TAIFA.
Kuzungumza na Taifa ni neno zito, si neno la mchezo mchezo. Ninadhani ilifaa kusema Mh MBOWE Mwenyekiti wa CDM atazungumza na vyombo vya habari na si kusema atazungumza na Taifa.
Mwisho tuendelee kujikinga na corona kwa kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu.
karibu kuwekeza Ileje. Tunayo ardhi ya kutosha yenye rutuba.