Kuwekeza kunahitaji zaidi ya yote kusoma nyakati, hasa mazingira ya kisera (policy environment) ya Chama Tawala na Serikali yake.
Rais Magufuli alipoingia madarakani anatimiza ahadi yake wakati wa kampeni kuwa nchi ni Tajiri ila fedha za Serikali zinaliwa/kuchezewa na wachache. Kauli yake ya kwanza alipoingia madarakani alisema wazi kuwa kuna watu wanafanya biashara kwa fedha za Serikali badala ya kufanya biashara kwa kwa fedha yao wenyewe inayozalishwa kibiashara.
Hoteli hiyo, naamini ilijengwa wakati shughuli nyingi za Serikali na Taasisi zake, hasa kubwa, zilifanyika Arusha, na ikawa ndiyo mahala pa Wakubwa kujinafasi.
Wakati ukuta, mwenye hoteli anapaswa kurudi kwenye meza ya mipango ajipange upya, kwa miaka 8 iliyobaki ya utawala wa Serikali inayoongozwa na Dr Magufuli.
Mwekezaji, wala mashabiki wa kisiasa wasije na lawama, kwa kuwa uamuzi wa kuwekeza ni wa mwekezaji na siyo Serikali. Serikali huweka mazingira rafiki ya uwekezaji.o