benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Baada ya uwekezaji na uwezeshaji mkubwa kutoka Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inatarajiwa kuingia katika historia tarehe 13/04/2023 kwa kuwa miongoni mwa Hospitali zinazotoa huduma ya kupandikiza Figo hapa nchini Tanzania.
Awali Hospitali hiyo ilikuwa ikitoa huduma ya Kusafisha damu (Dialysis) pamoja na kutoa huduma ya matibabu ya kuvunja mawe kwenye Figo na mfumo wa mkojo kwa njia ya mawimbi mshtuko/mtetemo bila kumpasua mgonjwa ambapo mgonjwa anaweza kutibiwa wa siku moja akisubiria mawe hayo yapasuke na kutoka kwa njia ya haja ndogo.
Hapa nchini Hospitali kadhaa ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili-Dar es Salaam na Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ni miongoni mwa Hospitali zinazotoa huduma ya kupandikiza figo.
Pia Hospitali hiyo ya Muhimbili-Mloganzila ipo katika hatua za mwisho katika kuanza kutoa huduma ya kupandikiza Kizazi na Ini.