Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
HOSPITALI mpya ya Rufani mkoani Shinyanga iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga haina jengo la kuhifadhia Maiti, pamoja na kukabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yudas Ndugile amebainisha hayo jana kwenye ziara ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mkoani humo.

Alisema hospitali hiyo ilianza kutoa huduma za matibabu Novemba mwaka jana na kwamba serikali ilitoa Sh.bilioni tisa ili kuikamilisha, bilioni tano zilitumika ujenzi wa majengo na bilioni nne ununuzi wa vifaa tiba, lakini hadi sasa haina jengo la kuhifadhia maiti.

“Hospitali hii ina hudumia wagonjwa 150 hadi 200 kwa siku na tunalaza wagonjwa 60 hadi 80 kwa siku moja ya changamoto ambayo tunayo kwenye hospitali yetu hatuna jengo la kuhifadhia maiti,” alisema Dk. Ndugile.

—————
Serikali imetoa ufafanuzi: Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu ukosefu wa Jengo la Kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa Shinyanga
 
HAKUNA UJINGA MKUBWA KWA TAIFA KAMA HUU, ndio yale yale ya mwekezaji wa mgodi kuambiwa awajengee shule wanakijiji..kweli Viongozi na akili zenu timamu unataka kumpa dezo ya bandari mwekezaji kwa masharti pia akujengee mochuari? Hivi sisi WATANZANIA ujinga wa fikra wa kafanyiwa kila kitu na mwekezaji hata vitu ambavyo tunaweza kufanya utaondoka lini vichwani .Miaka 60 ya uhuru bado vitu kama shule ,hospital, etc kweli mwekezaji aje kufanya?
 
Back
Top Bottom