Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Magharibi Kuanza Januari 2024

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Serikali imeeleza kuwa itaanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Magaharibi ifikapo mwezi Januari mwaka 2024

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalu, Zainab Katimba, aliyeuliza ni lini Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi itaanza kujengwa, Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ametoa majibu kuwa:

"Katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 5, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Magharibi ambapo ujenzi utaanza na jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD) ili litakapokamilika huduma zianze kutolewa.

Mheshimiwa Spika, ujenzi huu utaanza mwezi Januari 2024."
 
Back
Top Bottom