Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Kama kuna jambo linalonifanya kila siku niseme inawezekana nchi yetu tulilaaniwa ni namna ambavyo nchi yetu imejengwa vibaya bila mpangilio. Yaani namna watu wanavyojijengea hovyo hovyo tu bila mpangilio na kupangwa.
Kila siku tumekuwa tukiandika humu na kusema humu huku titicaca Serikali ichukue hatua ila kwa muda ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa.
Kwa namna Waziri Jerry Silaa alivyoanza kulishughulikia hili jambo napenda kumwambia kwa akili zangu zote kuwa ametufurahisha sana watu wenye akili tuliokuwa tunalipigia kelele hili jambo.
Najua watanzania wanapenda sana uholela na najua kwa wengi kuishi eneo lililopangwa na kupimwa vizuri wanaona ni kama kitu kigeni na cha kitajiri sana hivyo kutopenda.
Nichachopenda kuwaambia watanzania kila mtu ana haki na kustahili kuishi katika eneo lililopangwa na kupimwa vizuri. Hii sio haki ya watu wachache kama wanavyodhani hivyo ili nchi yetu kuwa na mpangilio mzuri ni lazima sasa waiunge mkono Serikali kuhakikisha nchi yetu yote inapimwa na kupangwa vizuri ili tuondokane na takataka za ujenzi holela.
Mwisho kwa Jerry Silaa naomba usiishie kutoa matamko tu. Sasa uje na mpango na utekelezaji wake katika kuhakikisha nchi yetu yote inapimwa na kupangwa vizuri. Weka fedha, weka mfumo tuondokane na aibu za kuishi kama wadudu na nchi yetu kuwa ya hovyo. Unaenda vizuri na kuanzia sasa nitazidi kukuombea ili usiondolewe katika Uwaziri wa Ardhi na tutimize ndoto ya nchi yetu kupimwa na kupangwa yote.