Ikiwa wenye PhD feki wana manufaa na uchungu kwa nchi yetu, basi tunawataka waongoze nchi yetu

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Wahasimu wa Hayati JPM wanaendelea kutuaminisha kuwa, JPM hakuwa Mtanzania pia PhD yake ilikuwa feki.

Licha ya hayo yote, wanaungana na wengi kuduwaa jinsi PhD feki ilivyo tofauti na PhD original.

PhD original tulizonazo hapa Tanzania, hazitusaidii na hazijawahi kutatua matatizo yetu kama nchi.

Jiji kubwa kabisa hapa Tanzania na maeneo karibu yote ya mikoa ya Pwani hakuna maji, na PhD original zipo, hazina majibu. Jamani, tujivunie PhD original kweli?

Jambo hilihili lingetokea kipindi cha JPM mrundi na mwenye PhD feki, tusingelikuwa hatuna maji Kwa majuma haya yote.

Nachotaka kusema ni kwamba, ikiwa wenye PhD feki wanauwezo Mkubwa kiasi hiko, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupatie kwa wingi hawa watu kulikoni walio na original PhD, hawa watu ni sawa na ziro (0) kabisa vichwani mwao.

Jambo lingine ni kwamba, ikiwa ni kweli Hayati Magufuli hakuwa Mtanzania, na licha ya yeye kutokuwa Mtanzania amewafanyia mengi mazuri na ya kushangaza Watanzania, basi tunawahitaji Warundi wengi kwenye nchi yetu ili wawe maraisi wetu na hatimaye tuondokane na huu umasikini wa watu wetu Kwa sababu wazawa wa nchi hii wamekalia kuiba rasilimali zetu tu na hakuna la maana.

PhD feki ya Kirundi moja, sawa na PhD orijinal 200 za Kitanzania.

PhD original za Kibongo ni Hovyo sana!
 
Daah! . mmebadirisha maneno ya heading

Mmeupozesha Uzi huu wakuu hadi siku yangu tayari ishaharibika aisee
 
Back
Top Bottom