Rais wa Tanzania 2030, kipaumbele chako kiwe mipango miji

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Kusema kweli kwa asilimia 98 nina amini bila shaka kuwa Jamii kubwa ya Watanzania wana mtindio wa ubongo, yaaani hawawezi kuwaza na kufikiri vizuri.

Jambo kuu linalonifanya kuamini hivi ni kwa namna ninapotembea mikoa mbalimbali nchini na kuona jinsi wananchi wanavyojenga bila mpangilio na wala Serikali haipo serious kusisitiza mipango miji.

Sehemu kubwa ya Tanzania naweza kusema asilimia 75- 80 imejengwa bila kuzingatia mipango miji na kupangwa. Ukitembea mikoa mingi ikiwa sehemu zinazojulikana kama majiji mfano Mbeya, Mwanza, Dar es Salaam na Arusha sehemu kubwa imejengwa bila kuzingatia mipango miji pamoja na kupagwa hivyo kupelekea miji yetu kutopendeza na kuwa kama majalala ya takataka.

Kwa Rais ajaye wa 2030, awe yeyote yule naomba hotuba yake ya kwanza azungumzie jambo hili kama moja ya vipaumbele vyake vikuu.

Aje na mpango kabambe wa kubomoa na kujenga upya Majiji yote ya nchi hii ambayo yamejengwa vibaya bila mpangilio.

Kwenye hili kwanza aanze kwa kujenga nyumba mpya kwa mtindo wa flats kwenye maeneo mapya yaliyopangwa vizuri na kuhamishia wananchi walio katika maeneo yaliyojengwa vibaya/ hovyo kwa kutozingatia mipango miji. Wananchi hawa watakapohamishiwa katika nyumba hizo wawekewe mpango wa kulipia ili kununua hizo nyumba kwa kipindi fulani ili kurudisha gharama za ujenzi tu. Akimaliza kulipa anamilikishwa. Hata kama akifariki familia yake itaendelea kulipa na ikimaliza itamilikishwa.

Pili, kwa kundi la wale wanaojiweza, yapangwe na kupimwa maeneo ambayo watapewa viwanja bure kwa kujiandikisha na kupewa utaratibu wa kujenga. Hawa wajenge kutokana na plan ya eneo husika na wakimaliza kujenga wataanza kulipia gharama za viwanja vyao pamoja na kodi.

Tatu, kupangwe na kupimwa maeneo kwa ajili ya makampuni kujenga na kuuza nyumba za makazi na biashara. Kwenye maeneo haya makampuni yapewe bure, yajenge nyumba kwa standards tofauti na kuanza kuziuza. Kuwe na exemption ya kodi katika kujenga na kuziuza hizi nyumba.

Nina uhakika haya yakifanyika, ndani ya miaka 10-15 nchi yetu yote itakuwa imepangwa na kujengwa vizuri sana hivyo kuondoa hii aibu ya kuonekana kama nchi nzima ni majinga, hatuwazi wala kufikiri vizuri.

Tuna uwezo wa kufanya hivi na tukaendelea na shughuli nyingine za maendeleo bila shida kabisa.

Kupanga ni kuchagua. Rais wetu wa 2030. Naweka huu uzi inshallah nikiwa hai 2030 nitaufufua.
 
Mipango miji na mikopo ya IMF huo ni ujinga.
Kipaumbele ni nchi kumiliki maliasili Kama migodi bandari n.k Kwa asilimia kubwa au hata 100%
 
Mipango miji ihusishe Public Open Spaces(POS) na pia mipango ya mapema ya miondombinu, taifa linaingia hasara kubwa sana kubomoa lami na kufidia watu kila mara kujenga miondombinu mipya.
 
2030 ni mbali sana, Sehemu kubwa ya nchi itakuwa kama slums na makazi duni kama kupanga miji kutaendelea kuchelewa hadi wakati huo na itahitajika gharama kubwa zaidi kurudisha maeneo ya nchi katika hadhi ya binadamu kuishi.
Sahihi kabisa. Kusema kweli hili halihitaji 2030. Ikiwezekana tunaweza tukaanza sasa.
Swali langu ni Je kwa sasa tuna hiyo political will?
 
Na sheria hizi za kumuhudumia Rais na mwenza wake hadi wanakufa aibe ili iweje?
hiyo ya kuhudumiwa hadi afe pia ni wizi...kwani awezi kutumia mshahala wake kumake business hadi sisi tumuhudumie...

broh ebu inuka kuna wenye uhitaji haswa ila si marais wastaafu...😭😭😭​
 
Mipango miji ihusishe Public Open Spaces(POS) na pia mipango ya mapema ya miondombinu, taifa linaingia hasara kubwa sana kubomoa lami na kufidia watu kila mara kujenga miondombinu mipya.
Hyo bibi hata hana habari na hilo labda kununua magoli na kupomgeza team za michezo hilo ndo analoliweza
 
Kwa serikali makini kupanga miji ni kitu kidogo
Lakini kwa serikali ya CCM wanachozingatia wao ni kodi ya ujenzi wewe jenga popote
Kuna watu wamejenga mpaka kwenye hifadhi ya mto.
 
Back
Top Bottom