Uchaguzi 2020 Hongera sana ITV kwa kurusha habari kwa usawa kwa vyama vyote

hayaland

JF-Expert Member
May 4, 2012
692
500
Nimekuwa nikifatilia habari mbalimbali hususani habari za UCHAGUZI KUU NA WAGOMBEA WAKE. nimegundua ni ITV pekee wanaorusha habari sahihi zisizo elemea upande wowote ule(sijui azam).ukikosa habari ya itv inakulazimu kutumia mitandao ya kijamii kupata habari zenye uhakikia zaidi.Baadhi ya vituo vya television sitapenda kuvitaja wao wamejikita katika habari za vijijini zisizo na mvuto hata kidogo.

Napenda kuwahasa kwa sasa ni kipindi cha uchaguzi ni muhimu sana kutoa habari za kampeni kwa vyama vyote bila kubagua. Ukiangalia STAR TV habari zao utadhani wako enzi za karne ya 20.Naamini wao katika mlengo wa chama fulani ila kuna haja ya kurusha habari za vyama vyote.Ukiangalia hawarushi habari za MH TUNDU LISSU na hawana mwandishi huko ila kampeni zinafanyika sana.

Tunakoelekea nguvu ya mitandao ya kijamii itakuwa kubwa sana kuliko kutegemea habari kutoka katika vituo vya televisions mbalimbali.Na baadhi ya vyama vya siasa wamebadili upepo wao wao badala ya kutumia zaidi tv sasa wammejikita zaidi katika mitandao ya kijamii.

Hongera sana MABELE MAKUBI kutupa habari za MH LISSU kwa uhakikia na mvuto wa hatari
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,258
2,000
Kwakuwa tu umewapa sifa ITV kwa kurusha habari za "wasiyempenda" siku chache zijazo utasikia wamefungiwa kwa siku 7.

Tanzania itarejea kwenye misingi ya Uhuru na umoja jiwe akiondoshwa 28/10/2020. Na ndipo tutaanza kupata Maendeleo.
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,570
2,000
Dawa inawaingia sasa wanaanza kujitambua taratibu tutaelewana tu
 

Kalpana

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
6,501
2,000
Shida ni kusifia tuu na hasa ukisifia wasiolipenda . Maana nakumbuka Tundu Lisu aliwasifia polisi baada ya hapo alipata kichapo cha mabomu
 

REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
2,780
2,000
ITV wanazidi kusoma alama na nyakati, wameshapima (check and balance) na kuona maji yanaenda kuzidi unga, so inabidi warudishe Imani' kwa audience wao kwa kuanza 'kubalance' habari za kampeni.
 

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
492
1,000
Kwasasa chombo pekee kilicho mahiri katika kurusha habari kwa kina bila ubaguzi ni Azam Tv ( UTV)

Unapata coverage ya kutosha kila angle ya nchi wapo, watangazaji mahiri kina Charles Hillary, Ivona, Burhan Muhuza, Fatma Nyangasa etc, wachambuzi mahiri wa siasa wanaoalikwa ktk session ya habari kama kina Said Msonga, na pía ung'aavu wa picha (HD) na usikivu vyema kabisa vinanifanya niwe fully satisfied ktk upataji wa habari..!!!

Tunasemaga mpira wa pasi nyingi ni mpira biriani, basi Azam News (UTV) ni habari biriani
 
Aug 7, 2020
28
75
Washachelewa sana, toka waanze tabia ya uoga na kukumbatia serikali walishapunguza sana watazamaji nikiwemo mimi, Naona mzee aliondoka na ITV yake.

Sasahivi hakuna kimbilio la kupata habari za uhakika zaidi vyombo vya nje, hapa ndani watu wanaangalia tamthilia tu za azam walau.
 

torosi

JF-Expert Member
Aug 12, 2020
372
1,000
Nakumbuka hawa ITV mwaka 2015 siku ya kupiga kura, walikuepo chato

Wakiwa live mwandishi wa habari akamuuliza Jiwe baada ya kutoka kupiga kura, Je akishindwa atakubali matokeo.? Nakumbuka jinsi jiwe alivyomkata jicho na lile swali alikataa kujibu. Baada ya kama dakika 15 jamaa wakakata matangazo huko Chato

Ile clip sijawahi kuiona tena hata Youtube
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom