Home workout special thread (Uzi maalumu wa Mazoezi unayoweza kufanyia nyumbani)

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,563
Salaam Wakuu,

Natumai nyote mpo salama. Nimeleta uzi huu kama sehemu ya kujihamasisha mimi na kuwahamasisha wengine kufanya mazoezi Soma: Umuhimu wa kufanya mazoezi

Natambau wengi wetu tunatamani kuwa wafanya mazoezi, lakini kwa sababu mbalimbali tumekuwa tunakosa muda kwenda uwanjani au sehemu za mazoezi,

Uzi huu umezingatia sana ratiba ya watu. Hivyo, nitakuwa nikiweka clips fupifupi zikionesha mazoezi rahisi ambayo mtu yoyote anaweza kufanyia nyumbani kwake.

Kama unayo clip pia weka hapa uzi huu ni wetu sote.

Katika kila clip ntayoweka fanya zoezi hilo kwa sekunde 30.

PIA SOMA: SoC 2021 - Afya: Unataka uanze kufanya mazoezi? Fuata hatua hizi...

 
Tengeneza shape na stamina ya miguu yako ukiwa home. Mazoezi simple kabisa. Fanya raund 16 kila zoezi. Utaongeza idadi kadri siku zinavyosonga.


No pain no gain
 
Mazoezi simple ya tumbo unayafanya mwenyewe home. Anza na raud 15 kila zoezi. Ongeza idadi kadri siku zinavyosonga.

 
Nina kila saa moja ya mazoezi kila siku. Mazoezi yangu nayafanyia chumbani kwangu muda mwingine. Au kwenye chumba cha mazoezi.Hata nikiwa nimesafiri hotel nitakayofikia nahakikisha room ninanalitaka lina nafasi fulani ya kunitosha.

Naanza mazoezi ya chini,yaani miguu. Naanza kwa kuruka kama kamba japo nakuwa sina kamba. Naruka kama dakika 1 mpaka 2 nabadiri naruka ile kijeshi unanyua kwa kuukunja kijeshi,hiyo dakika 1. Nabadiri miguu kama nakimbia mikono ikigusa kisigino chap. Hiyo dakika 2. Narudi kwenye kamba. Nakuja kichura sekunde 40. Mchanganyiko wa mazoezi hayo mpaka dakika 30. Nastop,navuta pumzi dakika kama 2. Nakuja mazoezi ya push-up. Kwenye push-up hapo kuna ile unanyoosha mikono mbele kama push-up za kawaida ila hii utofauti wake na zingine hii inafanya kazi nyingi. Unanyoosha mikono mbele ukiwa umeikutanisha. Nyoosha sana,hapo unaenda kama kwa kupiga push-up lakini kwa kuiendea mikono mbele na kurudi nyuma,unaifuata na kurudi nyuma. Hii inakaza tumbo,mikono kuanzia kwenye kifua mpaka mwisho wa mikono. Hizo napiga 5 mpaka 10 nainunuka navuta pumzi. Nabadiri napiga kawaida pc 40. Naruka ya mwanzo. Kwa ujumla naenda mara 10.

Nakuja za tumbo. Nalala chali nikiwa nimenyooka. Miguu naivalisha uvunguni kwa kitanda kwenye mwamba. Nikiwa nimenyooka hivyo hivyo mikono nimeikutanisha kisogoni nanyanyuka,narudi chini bila kufika chini. Naenda hiyo pc 30. Napumzika sekunde 15 kuvuta pumzi. Narudi tena. Nabadiri naenda nikishuka nashika mkono wa kushoto upande wa kulia chini,nanyanyuka,narudi chini mkono wa kulia unagusa chini upande wa kushoto. Hizo Jumla yake 30 mara 10. Mpaka hapo saa moja kamili inakuwa imekata.

Nimeanza haya mazoezi tangu nikiwa na umri wa miaka 22 mpaka sasa miaka 40+ nimo tu
 
Mazoezi ya kuimarisha kifua na mikono. Jitahidi anza na raund 20 kila zoezi
 
Nina kila saa moja ya mazoezi kila siku. Mazoezi yangu nayafanyia chumbani kwangu muda mwingine. Au kwenye chumba cha mazoezi.Hata nikiwa nimesafiri hotel nitakayofikia nahakikisha room ninanalitaka lina nafasi fulani ya kunitosha...
Safi sana kwa commitment hiyo ndugu yangu. Tutumie uzi huu kuhamasishana na kufundishana mazoezi mbalimbali.

Ukipata demo tupia hapa huenda ikasaidia kuwaamsha na kuhamasisha wengine
 
Mazoezi simple kwa ajili ya tumbo. Ukifanya hili kwa uhakika utapata matokeo mazuri kwa haraka, Kila zoezi fanya kwa sekunde 30 unapoanza.


 
Back
Top Bottom