Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

Kwanza naona unajileta we mwenyewe.
Umesema Biblia inapatikana sehemu nyingi, hivyo bei ni tofauti. Dawa ya Babu inapatikana wapi na wapi???
Huko zinapotoka Biblia bei ni fixed au????
Unaweza ukatuletea sehemu ambayo Babu amesema alioteshwa hiyo 500/-??

Turudi kanisani.
Ni kweli sadaka sio lazima pesa, ni chochote, lakin unafahamu kwamba zile bahasha za kutolea sadaka zimeandikwa umetoa kiasi gani kwa pesa tu na sio vinginevyo???
Kama unafahamu kwamba kutoa sadaka sio lazima, je kutafuta tiba ni lazima????
Babu alisema ni lazima utibiwe na yeye???
Kuna mtu alikosa 500/- akaomba asaidiwe ikashindikana???
Huyu Mungu alisema NA ASIYEFANYA KAZI ASILE, je kutayakumbuka haya maneno kweli???
Wewe uliyekuwa na 100/- uliomba kusaidiwa na Babu au mtu yeyote ikashindikana???
Je ni kweli haiwezekani kusaidiwa???

Bado hujasema, tunapoambia tuchangie ujenzi wa kanisa ili ifike kiasi fulani sio fixed amount??
Sare za kwaya je?? Kitatakiwa kiasi chochote kuzipata???

Narudia tena babu alisema mwenyewe kuwa ameoteshwa atoze sh 500/-
nakuuliza swali na wewe, babu alishawahi kutangaza kuwa aliye na pesa chini ya 500/- aende akatibiwe?
 
Bikira ni heshima tunakubali. Lakini sio kuipigia tarumbeta all the time hata wakati usiohusu. Modesty inahusisha na kutozungumza vitu kama hivyo.

Huwezi kutangazia umma kuwa una figure namba nane kisha bikira ikisha tukufikirie kuwa na heshima. Huwezi kuanzisha thread inayofunza namna ya kutongoza inayohusisha kuwashika shika wanaume kisha utwambie una heshima kwa kuwa ni bikira.

Kuwa Bikra ni heshima sana Mungu akubariki na akupe haja ya moyo wako akupe Mume mwema kwenye maisha yako. Ukweli uko wazi na unaonekana una ufahamu mzuri wa maandiko, Babu anaweza kua sahihi au asiwe kwakuwa ni binadamu maana hata Musa aliambiwa auambie mwamba utoe maji yeye kaupiga mwamba mara mbili, babu anaweza kuharibiwa pia na watu maana mioyo hugeuzwa na watu.
 
.....zama za makuhani ndio hiyo 10% iliamuriwa na labda hili nalo lahitaji mjadala wake unaojitegemea.....

Mungu hana kigeugeu! Mungu ni yuleyule jana, leo, kesho na hata milele. Kama suala la zaka halipo sasa basi haikuwahi kuwapo!
 
Asante kwa majibu. Nimeanza kuelewa kwa kiasi.

Babu sijamsikia kutangaza kuwa asiye na 500 hatampa huduma. Lakini hiyo haimaanishi kuwa asiye nayo hatampa.

Kama ulivyosema Mungu anasema sadaka ni 10%. Lakini wasiyokuwa nayo wanasamehewa kutoa. Labda Babu anatumia theory hiyo hiyo. Kuwa huduma ni 500 lakini asiyekuwa nayo atampatia huduma vile vile.

Naamini kuweka bei fixed kumesaidia kutowafanya wenye nazo kummiliki fulani babu. Pata picha kina Rostam na Lowasa wangetoa pesa kiasi gani na kujifagharisha?

swali zuri sana.
Naomba niaze kujibu swali la pili.
Kwa mujibu wa baubu mwenyewe alisema ameoteshwa gharama ya matibabu ni SHILINGI 500/- hilo alilitamka yeye mwenyewe ene ameambiwana Mungu mpaka jinsi ya kuigawa hiyo 500/- inayopatikana.

Swali lako la kwanza naomba nikujibu kwa swali.
Kuna siku babu alishawahi kutangaza kuwa asiye na 500/- aende tu atatibiwa?
 
Sadaka/ Zaka ni 10% haijalishi zamani wala sasa.

Mungu hana kigeugeu! Mungu ni yuleyule jana, leo, kesho na hata milele. Kama suala la dhaka halipo sasa basi haikuwahi kuwapo!
 
kwanza tukubaliane, kutoa sadaka sio lazima yaani kama huna kipato sio lazima kutoa.
Na sadaka pia sio lazima kutoa pesa(nirekebishwe kama nimekosea)
na pia hiyo 10% uliyoitaja hapo nayo pia inategemea na kipato cha mtu(tunarudi pale palee)
kama kuna askofu, padri au mchungaji anayesema sadaka ni lazima utoe kiasi fulani huyo anakosea.
Kuhusu biblia;
kesi ya biblia hapa ni tofauti kabisa.
Wapo wanaouza biblia kwa bei ya juu, wapo wanouza kwa bei ya chini na wapo pia wanaotoa bure.
Hawa wote hawajaoteshwa na mungu.

Turudi kwenye tiba ya babu.
Mungu anapoagiza mtu anayetaka tiba yake ni lazma atoe sh 500/- ili apone na asiyekuwa nayo je?
Tiba iliyoelekezwa na mungu!!
Kama mimi uwezo wangu ni sh 100/- je inamaana nife? Mungu yupo fea kweli hapo?
Ndio maana hata kwenye kutoa sadaka mungu alielekeza kutoa kadiri ya uwezo wako, hakusema fixed amount.

10% wasn't it not fixed?
 
kuna post nyingi sana nimetoa majibu mengi sana tofauti. tatizo kuna mtu hukurupuka kuweka post bila kusoma zilizotangulia. kwa hiyo kama hoja fulani imejirudia na mimi nilishaijibu silazimiki kujijibu upya.

pia kuna wale wanaoniuliza wakinitaka nisemee mfano madhehebu yangu ya KKKT ama huduma zinazojitegemea kama za akina rwakatale, mwingira, kakobe, mwakasege, lusekelo nk, mimi si msemaji wa KKKT wala huduma nyingine yoyote ila nikiona kitu hakiendi kama maandiko yanavyosema mimi hufafanua namna maandiko yanavyotaka na si kusemea kanisa. hata huyu babu naye ni m-KKKT kama mimi, ninamkosoa kwa kuwa shughuli zake zina maswali mengi sana kwa mujibu wa maandiko.

kuna wengine wananishambulia mimi binafsi. naweza kuafafanua pale ninapoona kuna haja ya kufanya hivyo, vinginevyo naziacha tu hoja zao waendelee wenyewe.

halafu mmeona wengine wameanza kuchat na marafiki zao hapa kwenye thread kama wafanyavyo kwenye thread za jukwaa la MMU, sijui watu watabadilika lini!?

we jadili hoja nami nipo kufafanua hoja.

you are welcome.

kwa neema ya Mungu nitazikabili hoja zenu zote

Glory to God

Kwanza niseme kwamba, sikuwepo wakati uchangiaji wa hii post ulipoanza lakin nimepitia kila comment nimeona kuna mambo mengi umeshindwa kuyajibu, na hata sasa huelekei kwamba utayajibu.

Pili umesema wewe sio msemaji wa KKKT wala huduma nyingine yoyote (hivi unajua Babu anachofanya ni huduma??? Au wewe ni msemaji wa huduma ya Babu???), wala hao wenye huduma binafsi, then wakati huo huo unasema ukiona kitu hakiendi sawa na maandiko unakosoa!!!!!! Huoni hapa unajikoroga mwenyewe??? Hivi mnajua Babu ni binadamu na sio malaika??? Unafahamu hata watumishi wa Mungu nao wanahitaji kula na kupata malezi bora kama wengine???? Nani alikupa mamlaka ya kusemea huduma ya Babu mpaka utamke huduma yake NI SAWA TU NA WAGANGA WENGINE??? Au na wewe ulioteshwa maono umletee Babu???
Huoni hii unayoiita HOJA ni kumshambulia binafsi Babu na huduma zake???

Kwanini uwe mstari wa mbele kukosoa ya wenzako wakati ya kwako yana utata mwingi???
Nakukumbusha tena . . . . USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA

Kuhusu chat naona hii ni hoja ya kitoto zaidi.
Hivi kuna jukwaa hapa JF ambalo hakuna watu kuchati kabisa???? Au tunakukera tu kwa sababu zako binafsi?? MMU ndio sehemu ya kuchat kwani???
 
Asante kwa majibu. Nimeanza kuelewa kwa kiasi.

Babu sijamsikia kutangaza kuwa asiye na 500 hatampa huduma. Lakini hiyo haimaanishi kuwa asiye nayo hatampa.

Kama ulivyosema Mungu anasema sadaka ni 10%. Lakini wasiyokuwa nayo wanasamehewa kutoa. Labda Babu anatumia theory hiyo hiyo. Kuwa huduma ni 500 lakini asiyekuwa nayo atampatia huduma vile vile.

Naamini kuweka bei fixed kumesaidia kutowafanya wenye nazo kummiliki fulani babu. Pata picha kina Rostam na Lowasa wangetoa pesa kiasi gani na kujifagharisha?

Ndugu yangu usimsemee babu.
Kama aliweza kutangaza bei aliyo oteshwa pia angeweza kusema kuwa kwa wasionayo pia anawatibu.
lakini hakusema na amehojiwa mara nyingi tu na waandishi wa habari alakini hajasema.
 
Narudia tena babu alisema mwenyewe kuwa ameoteshwa atoze sh 500/-
nakuuliza swali na wewe, babu alishawahi kutangaza kuwa aliye na pesa chini ya 500/- aende akatibiwe?

Kuna mambo mengi sana hujayajibu ktk hoja yangu?
Tupe ushuhuda basi unaoonyesha mtu alikosa 500/- Babu akakataa kumpa dawa au watu wengine walio karibu wakagoma kabisa kumsaidia kukwepa hiyo GHARAMA KUBWA???!!
uNAMTAMBUAJE MTU/WATU WASIO NA UWEZO AMBAO WANAHITAJI MATIBABU BURE?? Tunaweza kuwa wakweli kwenye hili tafadhali???
Ukienda kwa babu hujiwezi atakunyima dawa kweli??? Tena kwa mtu aliyewahi kuwa mchungaji na kufanya kazi zaidi ya miaka 40 leo unathubutu kumfikiria hawezi kukusaidia endapo ukimweleza shida yako?? Unafahamu rekodi yake ya kusaidia watu ktk miaka yake 40 ya utumikiaji kanisani??? Unajua amesaidia angapi bure??? Leo eti kimshinde ki-500/-???
Huoni kwamba akisema bure basi kila mtu atataka anywe bure??? Atakula wapi na nini???

Mbona tunaongea kama vile Babu hakuwahi kutoa huduma bure au kama vile alitamka hatoi huduma bure????
Tanzania mna kazi sana!
 
Narudia tena babu alisema mwenyewe kuwa ameoteshwa atoze sh 500/-
nakuuliza swali na wewe, babu alishawahi kutangaza kuwa aliye na pesa chini ya 500/- aende akatibiwe?

Obviously asiyekuwa na TZS 500 kama si mkazi wa Loliondo hawezi kufika Loliondo. Taking into consideration nauli ya sasa kwenda Loliondo.
Nafuatilia majibu mengine ya huyu bwana kama hujajibu vile
 
Ndugu yangu usimsemee babu.
Kama aliweza kutangaza bei aliyo oteshwa pia angeweza kusema kuwa kwa wasionayo pia anawatibu.
lakini hakusema na amehojiwa mara nyingi tu na waandishi wa habari alakini hajasema.

Huu ni wivu wa kike.
 
Alaaaaaah! Kumbe sasa umeanza kuelewa!
Nenda kwa Babu, mwambie nimekuja kupata kikombe, sina 500/- naomba unisaidie halafu rudi hapa utupe ushuhuda wako wa alichokujibu.
Bahati mbaya amesema hairuhusiwi kunywa zaidi ya kimoja, lakini nina imani kubwa sana nae kiasi kwamba ana uwezo wa kukunywesha hata vikombe 6 wewe na familia yako. Ila kumbuka pia ni makosa makubwa kumjaribu mtumishi wa Mungu. Ukisema huna ionekane huna kweli na wala sio pretend, la sivyo huyo mtumishi akiyashinda majaribu yako utabaki matatani mbele ya Muumba wako
 
Kuna mambo mengi sana hujayajibu ktk hoja yangu?
Tupe ushuhuda basi unaoonyesha mtu alikosa 500/- Babu akakataa kumpa dawa au watu wengine walio karibu wakagoma kabisa kumsaidia kukwepa hiyo GHARAMA KUBWA???!!
uNAMTAMBUAJE MTU/WATU WASIO NA UWEZO AMBAO WANAHITAJI MATIBABU BURE?? Tunaweza kuwa wakweli kwenye hili tafadhali???
Ukienda kwa babu hujiwezi atakunyima dawa kweli??? Tena kwa mtu aliyewahi kuwa mchungaji na kufanya kazi zaidi ya miaka 40 leo unathubutu kumfikiria hawezi kukusaidia endapo ukimweleza shida yako?? Unafahamu rekodi yake ya kusaidia watu ktk miaka yake 40 ya utumikiaji kanisani??? Unajua amesaidia angapi bure??? Leo eti kimshinde ki-500/-???
Huoni kwamba akisema bure basi kila mtu atataka anywe bure??? Atakula wapi na nini???

Mbona tunaongea kama vile Babu hakuwahi kutoa huduma bure au kama vile alitamka hatoi huduma bure????
Tanzania mna kazi sana!

Kwani CPU, wewe unamwamini, kwa sababu tu alikuwa mchungaji??
What if asingekuwa Mchungaji wa KKKT akawa mchungaji wa TAG au padri wa Kikatoliki.
What if angekuwa Shekhe au mtumishi mwingine wa dini tofauti na Ukristo.
Mi sioni sababu za kumkubali kwa sababu ya historia yake ya uchungaji, tumkubali kwa sababu nyingine lakini siyo hiyo.
ILa mimi nasema Nitanyamaza kimya nitaomba, Cha Mungu Kitadumu, na kusimama tuuuuuuuuuuuu!!!
 
Ndibalema;

Mimi kwa nafsi yangu siamini dawa ya babu kwa sababu hakuna visibitisho vya kisayansi na sina imani ya kutosha ya kupona kwa kikombe kimoja (kwa kuwa hujiambia reasons milioni kadhaa za kisayansi na hivyo imani yangu kudidimia)

But still mambo ya Imani na Mungu huwezi kuyakatia fatwa tu kirahisi. Babu inaweza kuwa anakosea kwa kutotangaza kuwa atampa huduma yoyote anaeihitaji japo atakaekosa hiyo 500. Mimi na wewe hatujui kama atawapa huduma au la, lakini hatutaki hata kumpa benefit of the doubt kuwa atafanya hivyo.

Note: Si ajabu kukosea, hata Manabii walikosea pia enzi hizo. Mosses alimpiga mtu akafa.

Ndugu yangu usimsemee babu.
Kama aliweza kutangaza bei aliyo oteshwa pia angeweza kusema kuwa kwa wasionayo pia anawatibu.
lakini hakusema na amehojiwa mara nyingi tu na waandishi wa habari alakini hajasema.
 
Obviously asiyekuwa na TZS 500 kama si mkazi wa Loliondo hawezi kufika Loliondo. Taking into consideration nauli ya sasa kwenda Loliondo.
Nafuatilia majibu mengine ya huyu bwana kama hujajibu vile

Kwa maana ingine wale maskini wasiojiweza, na hawana uwezo wa kupata nauli wataendelea kuugua sio.
Huyu Mungu basi atakuwa na upendeleo, kwa sababu ukiangalia kwa haraka haraka, wanaohitaji hii tiba ni pamoja na lile daraja la chini kabisa, ambao hata kununua dawa za kinga/kurefusha maisha /kupunguza makali ya ugojwa, lishe bora nk ni shida kwao kupata.

Lakini hata nauli ya kusafiri kwenda huko ni hakuna, Matajiri na wenye uwezo ndio wanafanikiwa kwenda si ndiyo???
Huyu Mungu mwenye upendeleo namna hii mi simtaki!!!!
 
Kuna mambo mengi sana hujayajibu ktk hoja yangu?
Tupe ushuhuda basi unaoonyesha mtu alikosa 500/- Babu akakataa kumpa dawa au watu wengine walio karibu wakagoma kabisa kumsaidia kukwepa hiyo GHARAMA KUBWA???!!
uNAMTAMBUAJE MTU/WATU WASIO NA UWEZO AMBAO WANAHITAJI MATIBABU BURE?? Tunaweza kuwa wakweli kwenye hili tafadhali???
Ukienda kwa babu hujiwezi atakunyima dawa kweli??? Tena kwa mtu aliyewahi kuwa mchungaji na kufanya kazi zaidi ya miaka 40 leo unathubutu kumfikiria hawezi kukusaidia endapo ukimweleza shida yako?? Unafahamu rekodi yake ya kusaidia watu ktk miaka yake 40 ya utumikiaji kanisani??? Unajua amesaidia angapi bure??? Leo eti kimshinde ki-500/-???
Huoni kwamba akisema bure basi kila mtu atataka anywe bure??? Atakula wapi na nini???

Mbona tunaongea kama vile Babu hakuwahi kutoa huduma bure au kama vile alitamka hatoi huduma bure????
Tanzania mna kazi sana!
Kwahiyo mkuu unasema kuwa gharama ya dawa ni 500/- ila ukiwa na pungufu unatiwa?
Wewe unao ushuhuda kuwa mtu alienda bila ya pesa au alienda na pesa pungufu ya 500/- akatibiwa?
Kama ni hivyo mbona babu hajatwambia kuwa Mungu alimuotesha bei ya dawa ni sh 500/- ila kwa asiye na hiko kiasi pia anatibiwa? alishasema hivyo?
 
Kwa hiyo mlitakaje hata mjue kuwa ya Mungu?
Ahame Loliondo kwenye dawa ahamie Dar? na wa Mbeya jee? Mwanza?

Yesu alivyopoza alipoza wa dunia nzima au wale waliokuwa karibu yake tu? Duniani hakukuwa na wengine wagonjwa wakati huo?

Mungu kama humtaki endelea kutomtaka wakati wote, kwa sababu huduma inayotolewa Hospitalini inategemea kipato. Wenye utajiri wanapata huduma bora na wasio nazo hawapati huduma hata mbovu pengine.

Au huduma na dawa hizi za hospitali hazijaletwa duniani kwa uwezo wa Mungu? Watu wamezileta wenyewe kwa uwezo wao?

Kwa maana ingine wale maskini wasiojiweza, na hawana uwezo wa kupata nauli wataendelea kuugua sio.
Huyu Mungu basi atakuwa na upendeleo, kwa sababu ukiangalia kwa haraka haraka, wanaohitaji hii tiba ni pamoja na lile daraja la chini kabisa, ambao hata kununua dawa za kinga/kurefusha maisha /kupunguza makali ya ugojwa, lishe bora nk ni shida kwao kupata.

Lakini hata nauli ya kusafiri kwenda huko ni hakuna, Matajiri na wenye uwezo ndio wanafanikiwa kwenda si ndiyo???
Huyu Mungu mwenye upendeleo namna hii mi simtaki!!!!
 
Alaaaaaah! Kumbe sasa umeanza kuelewa!
Nenda kwa Babu, mwambie nimekuja kupata kikombe, sina 500/- naomba unisaidie halafu rudi hapa utupe ushuhuda wako wa alichokujibu.
Bahati mbaya amesema hairuhusiwi kunywa zaidi ya kimoja, lakini nina imani kubwa sana nae kiasi kwamba ana uwezo wa kukunywesha hata vikombe 6 wewe na familia yako. Ila kumbuka pia ni makosa makubwa kumjaribu mtumishi wa Mungu. Ukisema huna ionekane huna kweli na wala sio pretend, la sivyo huyo mtumishi akiyashinda majaribu yako utabaki matatani mbele ya Muumba wako

Kwa kigezo kipi??
 
Back
Top Bottom