Fanya Mambo aya kabla ya usahili

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi
Idadi ya watu ambao wanaomba kazi , kila mwaka imekuwa ikiongezeka mwaka Kwa mwaka , na kila mwaka vyuo vinatoa wataalamu WA Aina mbalimbali


Watu wengi awajui kwamba nafasi ya ajira ni fursa ya Mungu au miungu kutawala ofisi usika, umewai kusoma habari za Daniel , alipoitwa interview aliitwa pamoja na wachawi kwenye interview ,kuna watu wanaweza kusema ni maneno yangu soma habari hii

Daniel 1:20 Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.

Katika interview ya Mfalme Nebukadreza majibu aliyokuwa nayo Mfalme yalikuwa Daniel na wenzake walikuwa Bora mara 10 ya waganga na wachawi walioko kazini , Kwa hiyo Ile interview ilikuwa inawaondoa wale waganga kazini? Unafikiria wale waganga walifuraia kufutwa kazi na kina Daniel ??

Kuna watu wamekwenda interview na interview lakini hawapati , shida sio kwamba hawana sifa sio kwamba hawana uwezo shida wanategemea Sana vyeti na ujuzi walionao au watu wanao wafahamu kuliko kumtegemea Mungu?

Kuna tofauti ya kumuamini Mungu na kumtegemea , Mungu unaweza kuwa na muamini mzuri Sana WA Mungu lakini linapokuja kwenye swala la Maisha yako ya kila siku haumtegemei Mungu

Kama sio kwanini unakwenda Kwa watu kuomba connection ya ajira au unatoa rushwa upate ajira kama kweli unamtegema Mungu ?

Kuna nafasi za kazi ambazo connection haitakusaidia , vyeti havitakusaidia wala ujaja ujaja wako havitakusaidia , itaitajika mkono WA Mungu kuwa pamoja nawe

Kuna watu tangazo Tu la ajira kikitokea Tu wanakwenda Kwa Mganga kutengeneza mazingira ya kupata ajira, kuna wengine kukitokea tangazo la ajira wanakwenda kuonanana na wakubwa kutoa rushwa ili wapate ajira lakini wewe unakaa Tu unategemea Tu kwamba utashinda kwa urahisi Tu , unaamini Mungu atakusaidie wakati haumtegemei Mungu?


Fanya Mambo yafuatayo:-

Jambo la kwanza

Tangazo la ajira ni lango, watu wengi wanakosa kuitwa kwenye interview Tu kupitia tangazo la ajira, unapopata tangazo la ajira , tenga muomba WA kuomba tangazo ili, achilia Damu ya Yesu kwenye hilo tangazo ,Damu ya Yesu ikanene Kwa ajili yako kwenye kazi hiyo


Jambo la pili

Unapo andaa nyaraka zako za kuomba kazi , kabla ya kuzituma, bandika mikono Kwa Imani, ambatanisha maombi yako pamoja na Bwana Kwa Damu ya Yesu, mahali nyaraka zako zitakwenda Yesu Kristo akawe mdhamini wako katika wale wadhamini weka Jina la Yesu Kwa imani kama Mdhamini Kwa Damu ya Yesu

Jambo la tatu

Kwenye interview , mara nyingi ofisi nyingi kuna interview Zaidi ya moja, kuna interview ya mitihani ( written interview) na ya Kwa mahojiano ( oral interview) hakikisha kila interview unakwenda na Yesu, sema Nina kwenda kwenye interview ya kampuni flani pamoja na Bwana Kwa Damu ya Yesu , Yesu akutetetea Yesu akufungulie mlango, Yesu akupe kibari mbele za wasimamizi WA mitihani , mbele ya panel ya interview , Yesu akufundishe namna ya kujibu na majibu ya kujibu kwenye interview ,

Mambo mengine muhimu
1. Ombaea chumba cha mitihani ili Bwana Yesu atawale , ombea ufalme WA Mungu uje kwenye chumba cha mitihani/interview

2. Ombea WA simamizi WA mitihani wasimamie katika haki wasitumike kutoa nafasi yako Kwa wengine , ombea fikra Zao , teka mawazo Yao yapate kutii ya Kristo

3. Ombea maamuzi yao iyawe upande wa Bwana

4. Sikiliza maelekezo ya Roho mtakatifu na Mungu atakusaidie

Tukutane kazi na Jina la Bwana lipate kutukuzwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom