Pikipiki ya sh 500,000/= nayo ni pikipiki?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Wakuu, sijaidharau, ila nimeshangazwa na bei yake. Nimeona mtandaoni pikipiki zinazouzwa Dar Es Salaam kwa bei ndogo sana. Zipo za kuanzia laki tano mpaka sh 1.8m. Zote ni used.

Sikuwahi kumiliki pikipiki. Lakini nilipoziona leo mtandaoni, kwa jinsi zilivyo bei "chee", nimepata wazo la kuinunua moja niipeleke shambani iwe inatumika kwa safari za "hapa" na "pale" zinazohusiana na shamba.

Shamba lipo mbali na zilipo huduma muhimu za kijamii. Linahudumiwa na "wafanyakazi" watatu. Usafiri wanaotumia kwa sasa huko shambani ni baiskeli.

Je! Hizo pikipiki za bei rahisi zinazouzwa Dar Es Salaam zinaweza zikafaa?

Japo zipo mpaka za laki tano, lakini ninafikiria niwachukulie ya kuanzia laki saba.

Haitapakizwa mizigo mizito, labda vitu vidogo vidogo kama unga kilo ishirini n.k.

Hizo zinazotangazwa mitandaoni zinafaa? Namaanisha hizo za bei rahisi ambapo zingine zinauzwa mpaka shilingi laki tano!

Zinafaa?
 
Zinafaa Endapo ukazifanyia service pia.

Ushauri kumiliki pikipiki mbovu ni bora kuwa na baiskeli mpya.

Ikikupendeza na ukapata PESA utawanunulia pikipiki mpya ambayo sio hela nyingi Ina-range 2M .4

Ikiwa unalipenda shamba lako hakikisha unawapenda na wafanyakazi wako usiwanunulie vitu vibovu walee Kwa mfumo ambao sio tu watapata PESA Ila watapata maarifa ya Wao kufika hatua uliyofika wewe.
 
Mimi nna ngalangala yangu moja nlikua naendea pori.
Ukiiona tu kwa nje inaonekana marehemu kabisa, lakn masta nakwambia ni jino moja tu chuma hewani, mafuta inanusa na hao wenye mpya mpya hua nawaacha mbali na inakula shimo sio poa. Kila kitu mang'anyu. Nlikua nauza 500 akaja hopeless mmoja ananiambia anipe 300. Nmeitunza stoo.
Nataka nije niikate iwe kama zile za "cafe racer" maana sa hv naendesha DT.
To be honest, pikipiki ni engine. Hayo mengine ni ufwala. Kama chuma iko ngaa, chukua kaweke shockup mpya peleka pori waungwana waoshee jina
 
Piki Mpya Dukani ni million 2.9 na sasa hivi zimefika usajili Namba E
Kwa uwiano huo wa bei mimi sishangai piki piki Namba B au A kuuzwa laki tano ujue ni nzima mimi piki piki ikiwa inauzwa laki 2 na nusu

Hapo lazima nishtuke hata ikiwa Namba A lazima nijue nanunua mkangafu au nikute piki piki Namba c inauzwa laki tano mh lazima nijue hapo nauziwa Namba na sio piki piki.

Kwa soko la piki piki sasa hivi lilivyo kwa laki 5 unapata piki piki Namba A au B Iliyo nyooka sio MIKANGAFU Ila kama huzijui ni vizuri ukaenda na fundi wako pia.
 
🙏🙏🙏
 
Zinafaa Endapo ukazifanyia service pia.

Ushauri kumiliki pikipiki mbovu ni bora kuwa na baiskeli mpya.

Ikikupendeza na ukapata PESA utawanunulia pikipiki mpya ambayo sio hela nyingi Ina-range 2M .4

Ikiwa unalipenda shamba lako hakikisha unawapenda na wafanyakazi wako usiwanunulie vitu vibovu walee Kwa mfumo ambao sio tu watapata PESA Ila watapata maarifa ya Wao kufika hatua uliyofika wewe.
Jamaa yangu aliinunua yake sh 800,000/= mwaka Juzi lakini mpaka sasa bado ipo porini inapiga kazi. Yeye kaniambia pikipiki ni "bodi". Kama bodi ni nzima, hivyo vingine vibarekebishika kwa bei ndogo.

Sikuwa na mpango wa kununua pikipiki mkuu, na wao hawatarajii nifanye hivyo. Baiskeli ipo na wameridhika nayo. Lakini baada ya kuziona za bei rahisi, nimepatapata wazo la "kuwaboreshea" chombo cha usafiri.

Ninawajali sana wafanyakazi wangu mkuu. Ndiyo maana nimefikiria kuwaongezea chombo cha usafiri.

Si unajua kuihudumia pikipiki ni gharama zaidi kuliko baiskeli?🤣
1. Mafuta!
2. Service!
3. N.k.
 
Piki Mpya Dukani ni million 2.9 na sasa hivi zimefika usajili Namba E
Kwa uwiano huo wa bei mimi sishangai piki piki Namba B au A kuuzwa laki tano ujue ni nzima mimi piki piki ikiwa inauzwa laki 2 na nusu

Hapo lazima nishtuke hata ikiwa Namba A lazima nijue nanunua mkangafu au nikute piki piki Namba c inauzwa laki tano mh lazima nijue hapo nauziwa Namba na sio piki piki.

Kwa soko la piki piki sasa hivi lilivyo kwa laki 5 unapata piki piki Namba A au B Iliyo nyooka sio MIKANGAFU Ila kama huzijui ni vizuri ukaenda na fundi wako pia.
Nashukuru sana mkuu. Niwe tu mkweli! Baada ya kuziona za laki tano, nilipata mashaka kuwa huenda zikawa si "pikipiki". Ndicho kilichonifanya niupandishe huu uzi. Nilitaka nipate mawazo ya wazoefu.

Nashukuru. Mpaka sasa nimeshashawishika! HATA PIKIPIKI ZA SH 500,000/= NAZO NI PIKIPIKI!🙏
 
Domo la mamba cc150 bei kuanzia million 3.3. Hizi nyingine zinaanzia 2.8m. Hiyo hela ni ndefu. Nunua used zingatia engine ubora wake. Marekebisho mengine ni kawaida. Katika hiyo bei ya kununulia weka laki 2 ya kuipeleka gereji kuiongezea ubora
Sitaki mpya mkuu.

Na siyo kwamba nina aleji na mpya, ishu ni bei.

Kama kuna mpya ambayo bei yake haizidi milioni moja mbona nitaichukua haraka sana🤣
 
Mimi sijui sana kuhusu vyombo vya usafiri, lakini mtoa mada unaweza kuangalia minada ya vyombo vya moto vilivyotelekezwa polisi, huwa inafanyika unaweza pata chombo safi kwa bei ya kutupa, japo zile nzuri nzuri wanakuwaga wameshazichukua wao…. (Sorry kama hizi ni siri zenu)

Kwa kupitia huu uzi wenye taarifa zaidi wanaweza kukupatia.
 
Hizi zinachomolewa sana vitu na kuwekwa vibovu
 
Back
Top Bottom