Hofu ya CHADEMA ni kuogopa kusahaulika na sio kushindwa, kuratibu maandamano ni kuonesha uwepo wao. CCM fanyeni haya....

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Tofauti kubwa ninayoiona kati ya CHADEMA na vyama vingine vya upinzani mfano ACT Wazalenda ni kwamba CHADEMA wanaogopa kusahaulika na ACT wanaogopa kushindwa. Hofu hizo ndio zinazoendelea kuutafuna upinzani mpaka mifupa.

Kitendo Cha CHADEMA kuambulia mbunge wa kuchaguliwa na wabunge 19 wa viti maalumu kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 kwao ni kama ndoto mbaya ya kutosha na kinachowatia hofu zaidi na pengine wanajiuliza sana muda mwingi ,Je, huu ndio mwisho wetu? Je, tumesahaulika tayari? Lakini pia, ACT Wazalenda kufanikiwa kutoa Makamu wa Rais kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwao hofu yao kubwa Sasa ni kushindwa kuendelea kupata nafasi hiyo baadaye.

Hofu ya CHADEMA matokeo yake ni Hayati Magufuli na mpaka sasa wanaendelea kuwa na hofu zaidi na watu waliokuwa chini ya Magufuli na zaidi wana hofu na kutajwa Kwa jina la Magufuli. Kivuli cha Magufuli kinawatesa na kila mara wanaona kipo jirani yao na kadiri wanavyokiona karibu yao ndio wanapata hofu zaidi ya kusahaulika. Hayati Magufuli aliisahaulisha kabisa CHADEMA, watanzania walizoea kuishi bila upinzani ndio maana CHADEMA ikafunikwa 2020.

Baada ya kuondoka Hayati Magufuli CHADEMA waliamini kikwazo kimeondoka na Rais Samia atakuwa ni njia nyepesi kwao kujitibu kusahaulika kwao lakini haikuwa hivyo na zaidi wana hofu kubwa zaidi. Ni kweli CHADEMA imesahulika. CHADEMA waliamini kushindwa kwao ni kutokana na mfumo wa Tume ya Uchaguzi na hivyo Rais Samia kuamua kufanya maridhiano ili waone ni wapi penye changamoto parekebishwe. Na matokeo ya maridhiano hayo ambayo yatapelekea mabadiliko makubwa kwenye kwenye Sheria za uchaguzi na mageuzi kwenye mfumo wa Tume ya Uchaguzi bado yanapingwa na CHADEMA. Kwa nini?

Kwa sababu CHADEMA Kwa Sasa hakikubaliki na kwao wanaona mabadiliko hayo yataisaidia CCM kushinda zaidi ndio maana wamekuja na hoja ya maandamano. Kufanya maandamano ni kutafuta "attention" kwa watu ambao wamewasahau. Kwa kifupi maandamano ya CHADEMA ni attention seeking na sio kingine chochote. Tofauti yao na ACT ni kwamba ACT wametumia maridhiano kupanga mikakati ya ushindi.

Nini kifanywe na CCM ili kuusahaulisha upinzani kabisa?

Kwanza, hofu kubwa waliyonayo mpaka sasa CHADEMA ni Hayati Magufuli na Kwa kuwa Hayati Magufuli ameacha kukumbuka inayoishi Kwa watanzania na ni kumbukumbu iliyoisahaulisha CHADEMA basi CCM kitendelee kumtumia Hayati Magufuli popote pale. Mara nyingi nimesema na nitasema Hayati Magufuli akitumika vizuri 2025 kitapelekwa kuliko kikubwa mno upinzani.

Pili, Maandamano yao yaachwe ili watanzania waendelee kuuona upande wa pili wa CHADEMA unaotisha. Ni majuzi kama sikumsikia Katibu mkuu wa CHADEMA vibaya amenukuliwa akisema " wataendelea kufanya maandamano katika majiji na kama Serikali isipowasikiliza wataangalia utaratibu mwingine" ,tuendelee kuwa wavumilivu kama falsafa ya Rais Samia zinavyotaka na tutajua mengi makubwa.

Tatu, Mradi wa SGR uitwe jina la Magufuli, kama ambavyo tunaenzi kazi ya Wajerumani katika ujenzi wa Reli nchini mwetu Kwa zaidi ya miaka 100 Sasa hivyo naamini jina la Hayati litaenziwa Kwa miaka 100 na Kwa sababu CHADEMA wanamuogopa Hayati wataendelea kuogopa na kutishika zaidi na zaidi mpaka anguko lao litakapofika.

Imeandaliwa na mchambuzi wenu makini,
Karlo Mwilapwa.
mwilapwakarlo@gmail.com
 
Back
Top Bottom