Hizi siku nyingine hizi haaa!

Hizi siku nyingine hizi haaa!

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,119
Imagine,

Nimeamka asubuhi mvua inanyesha,
Kutoka kwangu mpaka kituoni ni kutembea kwa dakika tano,
Nimetafuta mwamvuli ndani sipati kwasababu haujawahi kuwepo,
Haya nimejitolea kuloa kwa hizo dakika tano mpaka kituoni,
Nimepanda daladala mara nalo siti zote zimejaa maji kwasababu nalo linavuja,
Kidogo mvua inaanza kwa kasi, daladala linaanza kuvuja na nalazimika kusimama,
Nafika ninapokwenda na sijui ntafikaje kwenye kaofisi kangu na mvua hii?

Haya, nimejitahidi nimefika huku nimeloa kiasi na kibaridi kikali,
Nafikia kwenye meza yenye chupa na vikombe vya kahawa nakuta patupu,
Khaa kumbe umeme umekatika na maji ya kahawa yanachemshwa na birika la umeme,
Haya sasa nimejikalia hapa na baridi, gizani na ka laptop kangu ka kichina kanakaa na chaji visaa viwili tu,

Kha siku nyingine hizi bhana!
 
Pole kiongozi! Ila nunua mwamvuli, usitegemee kumnenepesha Ng'ombe siku ya mnada.
Usisubiri masika ndy ununue mwamvuli ! Ununue kiangazi.
 
M'jr tabu ya nini? Tafuta mwanamke mwenye hela umuoe,we unafikiri Filipo hana akili?
Copy: marejesho
Hahahahaaa we ushauri wako hata siutaki asee kwasababu zifuatazo,

Sitaki kuamka asubuhi na kuanzakujiuliza kama nimsalimie habari za asubuhi au "SHIKAMOO"
Sitaki kubadilisha majina yangu kutoka yale niliyonayo sasa na kuitwa "MARIO" au "SERENGETI BOY"
Sitaki kuwa na mawazo ya kama leo atapata katoto zaidi na akaanza kufikiria MKATABA tulionao,
Na inakuwaje pale mi nitakapokutana na kale nitakakokadondokea?

Haya kwa ufupi ushauri wako siutaki baki nao mwenyewe.........

CC snowhite
 
Last edited by a moderator:

Mbona nasikia snowhite in real life ni 'malkia wa nyuki' na anaishi muscat?
 
Last edited by a moderator:
Mh! Kwanza pole sana mtoa mada na hii ni hali halisi ya maisha..
Bishanga naomba ushahidi tafwadhali...
 
Last edited by a moderator:
hayo ndo maisha yetu ya kila siku bongo
ila kwa leo pole sana.
 
Asante sana partner,

Niandalie za Nazi za karanga si unajua tabu yake?
Ntapitia partner ondoa shaka
ahahahahhaha acha uoga partner!
basi usijali!
ngoja niingie mtamboni!
 
Pole sana
Siku nyingine chukua tahadhari mapema.
 
partner achana na Bishanga!
pole kwa baridi!
pole kwa kukosa kikomba cha gahwa!
vipi,nikuandalie utapitia?
na kashata za nazi au karanga?
sijui naruhusiwa kumchagulia??
muandalie za karaga na kahawa ya tangawizi.
kisha umpe uji wa pilipili manga aitupe baridi mkono.

taa mnunulie kandili mtilie mafuta,
na kalaptop mwazime yako imliwaze ama si ndo upatna tena huu??
 
We nae gfsonwin,juu ya nini unapotea hivi?
 
Last edited by a moderator:
sijui naruhusiwa kumchagulia??
muandalie za karaga na kahawa ya tangawizi.
kisha umpe uji wa pilipili manga aitupe baridi mkono.

taa mnunulie kandili mtilie mafuta,
na kalaptop mwazime yako imliwaze ama si ndo upatna tena huu??
Mburaaaa!

Asee si umefanya sasa naansa hata kubadili mawa-mawaso..........hiyo mchanganyiko wako si unasidi hata Mtori? Nimeupendaje sasa!
 
Back
Top Bottom