snowhite
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,422
- 25,338
We Jibaba hukalii ma..i ! Ni kweli huyo ndiye malkia wa nyigu! But mwenyewe alishatupiiem zamani iwe siri! We ushamtangaza!
Ndiyo nini sasa?
ndo mi nashanga!
We Jibaba hukalii ma..i ! Ni kweli huyo ndiye malkia wa nyigu! But mwenyewe alishatupiiem zamani iwe siri! We ushamtangaza!
Ndiyo nini sasa?
Ya kazini nimeyatupa, jicho langu lilipokuona,
Uchovu wote umekatika, maudhi na hasira yote hakuna,
Wajua we ndo lulu, na mwengine hapa hakuna,
Karibu tujumuike sote, tuendelee kushikamana,
Kiwajibu na zaidi ,wapoteza yetu hali
Karibia mkekani ,nyoosha tua wako mwili
Ya kazini tia kapuni,ya kaumu tupa hewani
Karibu vya mkekani,ufunue vya kawani!
Duuh mineno hiyo! Mie hapa ni mijicho tu!
Bi' dada umenichuruzisha mimate an'nesesare ujue?
Imagine,
Haya, nimejitahidi nimefika huku nimeloa kiasi na kibaridi kikali,
Nafikia kwenye meza yenye chupa na vikombe vya kahawa nakuta patupu,
Khaa kumbe umeme umekatika na maji ya kahawa yanachemshwa na birika la umeme,
Haya sasa nimejikalia hapa na baridi,
Mbuzi yake kamba, niliwahi sikia hii,hasira zake mkizi,mwandamu huziwezi
raha wapewa kwa enzi,pokea kwa zake tenzi
sijitie kisirani,ulijaze lako tezi
mkekani kuna enzi,ipokee hala hala na machozi
mafiga yake ni chungu,sufuria haikaiMbuzi yake kamba, niliwahi sikia hii,
Japo siipendi sana, kwako nimefika sitanii,
Nimekuweka hapa mtimani, siku zote si tu jioni hii,
Nitapokuwa mbali nawe, sitaitamani Dunia hii
pole mwaya, wacha wajilie wenye meno yao.
hivi wajua mwenye kisu kikali ndo mla nyama??
Basi heri hutoa Maanani, maovu nduguye Shetani,mafiga yake ni chungu,sufuria haikai
kitanda mwenzake uvungu,hina hukoa kiganjani
Dunia wake wanadamu,kiwakosa hayawani
Hunikosi daima iwe dawamu,shaka rohoni la nini?
Basi heri hutoa Maanani, maovu nduguye Shetani,
Kila siku tupige goti, tupate heri ya yakini,
Katu lisiingie doa, kwenye mapenzi yetu makini,
Bishanga na wenzie wote, wakafie baharini,
Hiyo ilikuwa enzi za Musa na Harun. Enzi za sasa dawa ya baridi ni Chai ya iliki na mdalasini na vingine vya ki siku hizi
kaa kushoto!watu tupo kazini sa hz!
Hao bundi utakuwa umewaleta wewe,Khaa!
Nikidhani nitatupiwa jicho la imani, ukanikirimu japo kashata na kahawa mnywe wenyewe!
Imekua vya kunitimua !
Tena kushoto? Sikwambii kulia napo pia hola!
Haya bi dada, ila siku Bundi wakikutembelea utaujua umuhimu wangu.
La kuku halimpati mwewe,takaa usubiri sana!Khaa!
Nikidhani nitatupiwa jicho la imani, ukanikirimu japo kashata tu! na kahawa mnywe wenyewe!
Imekua vya kunitimua !
Tena kushoto? Sikwambii kulia napo pia hola!
Haya bi dada, ila siku Bundi wakikutembelea utaujua umuhimu wangu.