- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Hii picha inayosambaa mitandaoni ikionesha nyumba za bati na kuelezwa ni za jeshi la polisi, imekaaje wadau?
- Tunachokijua
- Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano ya amani tarehe 23/09/2024 na Mara baada ya maandamano hayo imekuwepo picha ya nyumba za mabati inayosambazwa Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikidai kuwa nyumba hizo ni za maaskari wa Jeshi la Polisi Tanzania
Fungua kutazama wanaodai nyumba hizo ni za Jeshi la Pilisi Tanzania (Hapa, Hapa, hapa na hapa)
Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa nyumba hizo Si za Jeshi la Polisi Tanzania bali ni za Jeshi la Magereza Tanzania, ambapo Zilikuwa zinatumiwa kama makazi na Jeshi la Magereza, Katika Gereza la Keko, kwa kutumia Google Reverse Image Search, JamiiCheck imebaini Mnamo Desemba 1, 2016 Kituo cha Clouds Fm kupitia mtandao wa Instagram kilichapisha taarifa kuhusu nyumba hizo kuwa ni za Jeshi la Magereza ambazo walikuwa wanazitumia kutokana na kukabiliana na uhaba uliokuwepo wa Nyumba za Maaskari.
Aidha, kwenye tovuti ya Jeshi la Magereza Mnamo Novemba 30, 2016 walichapisha nyumba hizo kwenye tovuti yao wakielezea ukaguzi wa eneo uliofanywa na Kamishna Jenerali wa Magereza - CGP. John Casmir Minja, eneo ambalo lingejengwa nyumba za Maaskari wa Jeshi la Magereza huku wakibainish kuw nyumba hizo za mabati zimekuwa zikutumiwa kama makazi na Maaskari wa Jesho hilo wa Gereza la Keko Dar Es Salaam kwa kile walichoeleza ni uhaba wa nyumba za kuishi Maaskari.
Aidha, chanzo chetu cha kuaminika kimetujulisha kuwa kwa sasa nyumba hizo hazipo baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za Maaskari ndani ya Gereza la Keko.