Mkuu hapa kwenye wanaoenda nje hawakumbuki nyumbani si kweli hata kidogo.Ujamaa ulikuwa na faida nyingi sana kuliko unavyofikiri wewe. Hata kiswahili ni lugha inayotuunganisha. Tatizo hapa ni watu kukosa uzalendo. Hasa nyie mnaoenda nje ya nchi hamkumbuki nyumbani.
Nimekaa nje sana na ninaweza kukuhakikishia WaTZ ndiyo wanaokumbuka nyumbani kuliko waliotoka sehemu nyingine za Africa.
Tatizo kubwa sana ukishatua tu Dar, unaanza kunusa ubabe wa nchi.
Nitakupa kisa kimoja tu kilichomisibu rafiki yangu ambaye alitaka kuwekeza nchini kama miaka sita hivi illiyopita kwa kuanzia na tshs. 100mln. Akaenda Tanzania Invenstment TIC akazungumza na Bwana mmoja pale kuhusu nia yake. Akaelekezwa NHC, wakati huo wakiingia ubia na wananchi wenye nia ya kuwekeza na kima cha chini wakati huo ili kupewa support ya kuwekeza ilikuwa ni Mln 100 kwa Mtanzania. Walikuwa wanakupa kiwanja mahali penye jengo la zamani ili uweze kulibomoa na kujenga kitega uchumi. Kama sijakosea walikuwa wao wanachukua 25 ~ 30% ya mapato kama mambo yakishakubalika na kukamilika.
Alichagua mahali kutokana na orodha ya viwanja alivyoonyeshwa, na Arusha ndiyo mahali alichagua. Kabla ya kusaini mkataba ulitakiwa kuanza kutengeneza bussiness plan pamoja na michoro ya jengo. Ilimgharimu rafiki yangu fedha nyingi kufanya safari hadi Arusha kukagua eneo, kutengeneza bizi-plan na kuchora jengo. Alipofika kuwasilisha kama alivyotakiwa, mizengwe ikaanza. Wakubwa wakamwambia kwenye lile jengo akaongeze ghorofa mbili za kwao! Na hapo hawatodhubutu kujiandikisha wazi kuwa ni zao, watakuletea ndugu au mwanafamilia na kuwaandikisha kwenye mkataba.
yule Bwana ilibidi aachilie mbali, amekwenda kufanya mambo mengine kabisa.
Watanzania tunahitaji kubadilika na kuwapenda wenzetu waliobahatika na walio na nia kuja kuwekeza nchini siyo kuwakatisha tamaa.
Nimeona mengi sana kuhusu hili swala. Nikiamua kuyaandika hapa utadhani ninatunga. Kwanza kabisa watanzania na haswa viongozi, kuliko amsadidie mtanzania mwenzake kuendeleza au kuanzisha biashara yake ni afadhali amsaidie mgeni. Sijua huwaridhisha nini haswa ndani ya mioyo yao.
Binafsi niliwahi kwenda Wizara ya Hazina kwa mazungumzo ya aina hiyo tena baada ya kuomba appointment. Nilifika nikaingia ofisini kwa bwana mkubwa, nilipoingia tu akaanza kulalamika, Oh mama mkwe kafanyiwa operation nataka niende hospitali sasa hivi. Nikamwabia basi afadhali tupange siku nyingine nitakayoweza kukuona. Akasema hebu nileze kwa kifupi haswa nini ulikuwa unataka. Nikazidi kumsihi kuwa mazungumzo yatakuwa marefu kwani yalikuwa yanabidi apitie makaratasi fulani ili aweze kunielewa. Akaamka tukabidi tutoke tunaongea. Alipofungua ofisi akamwona kijana mdogo tu mwenye asili ya kiAsia. Akamsalimia kwa shangwe akarudi ndani ya ofisi, nilkaa pale nje ya ofisi kwa sekretari wake kama dakika nyingine arobaini ikabidi niondoke.
Hivi unafikiri uhusiano wa namna hiyo unajenga nia njema kwa walioko nje kuja kuwekeza?? Nadhani wapo wengi waliokumbwa na mambo kama haya na ni wakati umefika jambo hili likajadilliwa hata Bungeni. Wapo watanzania wengi sana nje ambao wangependa kuja kuwekeza lakini mambo kama haya yanakatisha tamaaa!.