Hivi Wakenya wametushinda nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Wakenya wametushinda nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Don Draper, Jun 1, 2012.

 1. D

  Don Draper Senior Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukikutana nao nje ya nchi wana confidence za kufa mtu. wakiwa kwao hawataki longo longo na kama hawaelewani watapigana mikwaju kisha wanadeliver

  Tazama KTN au KBC picha ziko clear, news zimetulia, watangazaji wametulia

  Soma gazeti la NATION au Standard...huwezi fananisha na lile gazeti la Michuzi (daily nyuz) au lile la copy and paste (guardian)

  sisi tuna watu wengi zaidi, rasili mali nyingi zaidi, wanasiasa wengi zaidi, vyama vya siasa vingi zaidi, magazeti mengi zaidi, JF ndio zaidi, cabinet yetu kubwa kuliko ya kwao, katiba yao (na mahakama ya kadhi ndani) ndio walipitisha, sasa kwa nini hawa wana deliver na sisi hatuna kitu?

  I've tried to hate them lakini nimeshindwa, cant hate their ambition esp based on their national interest.

  Halafu wao kujenga li Superhighway kama hili ili iweje?

  ahh sisi hata kuthubutu tunashindwa sijui kwa nini
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,052
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Nyie wavivu sana kufanya kazi, nenda kwenye mashirika yenye wakenya hapa Tanzania utakuta wabongo wanalia lia eti wanaonewa! mmekalia uvivu tu
   
 3. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  ​Hivyo vya Blue ndo walivyotushinda.
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 46,445
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  aliyewaroga alifariki mwaka 1999 na mlimzika kwa mbwembwe!
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,123
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Leo wanasherekea madaraka day wanajivunia kuwa wakenya harambeeee! (listening to Jomo Kenyatta speech spoke better Swahili than most Kenyan Leaders how come?)
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,530
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Wako kikazi zaidi na si wavivu wa kufikiri kama Wabongo wengi tulivyo, hawaruhuru watu wengine wafikirie badala yao. Bora umeliona hilo!!!
   
 7. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kuendelea lazima uwe na roho mbaya. Wametuzidi roho mbaya na utu hawana kabisa, Pesa mbele utu nyuma.
   
 8. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mi nimefanya kazi sana na wakenya hata wao wengi tu wavivu. Uvivu ni tabia ya mtu binafsi. WAkenya wengi ni vilaza ukija kwenye Technical point of view. Ila watanzania hawana tabia ya kujisifu.
   
 9. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,730
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Wanajiamini. Wanathubutu hata kama wengine wana uwezo mdogo katika mambo. Lakini nafikiri zaidi ni suala la malezi: wamelelewa katika mfumo wa kibepari - mfumo wa ushindani. Kwa hiyo wao wanachowaza ni kufaulu, kuwa mbele, kuwazidi wengine, nk. Kila mmoja anakuwa na bidii na nia ya maendeleo.
   
 10. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na wewe unakiri kushundwa??. yaani huna confidence, una longo longo huwezi kudeliver??. Hakuna watu wenye longolongo kama wakenya,.
   
 11. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wekeni utaifa mbele, Acheni kujidharau na kujidhalilisha. Hili ndio linalotuua.
   
 12. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bora yako wewe umeongea point kidogo.
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,836
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Mi bado sijashindwa bado napambana labda wewe wamekushinda
   
 14. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  fikra za ujamaa na uswahili mwingi. Maendeleo hayaji kwa lelemama, yanahitaji kujituma. Lets be serious, otherwise ni aibu tupu. Hivi nchi hii Mungu ametupa kila kitu tunaweza kumlaumu nani kwa umaskini na aibu hii. Nipo nje ya nchi na ninapokutana na watu ukiwaambia umetoka tz, they associate it na umaskini, what a shame. Leaders ndio kila wakati kuzurura kuombaomba wakati sisi ndio tungetakiwa kuombwa.

  Kinachotokea tanzania ni kwamba kutakuwa na tabaka la wale walio matajiri kutokana na juhudi zao, na lile la umaskini wa kutisha ambao wataendelea kulaumu kila mtu kwa hali zao. And then there will be a fight between. Kwakuwa tabaka la juu litakuwa na nguvu, wajipanga kujihami kama ilivyo marekani, mabunduki kila mahali
   
 15. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Ujamaa ulikuwa na faida nyingi sana kuliko unavyofikiri wewe. Hata kiswahili ni lugha inayotuunganisha. Tatizo hapa ni watu kukosa uzalendo. Hasa nyie mnaoenda nje ya nchi hamkumbuki nyumbani.
   
 16. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Labda kinachowasaidia kingine ni ukabila, hakuna kabila linalokubali kuwa chini ya mwingine kenya, hata huyo raisi wao na waziri mkuu wao ni ukabila tuu ukasababisha mauaji makubwa!
   
 17. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kweli unaweza kuchukulia mfano wa China!
  Sema sisi hatujiamini kuwa tunaweza, Unamkuta mtu ni mtaalamu kwelikweli but hajiamini!
   
 18. D

  Don Draper Senior Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unapambana kwenye giza kaka?

  maana hata Che Guevara alipokuja Africa (Congo) na kukuta akina Kabila wavuvu ilibidi aachane nao maana hawakuwa serious

  sasa hebu niambie unapambania nini hasa? na so far umefikia wapi kwenye mapambano hayo?
   
 19. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 823
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Tatizo letu ni ubishi na kujiona wajuaji wa kila kitu, hivyo kukwamisha mipango mingi, kila kitu tz ni kulindana sasa maendeleo yatakuwepo kweli mazingira ambayo nchi imefika mahali inaonekana kama haina mwenyewe.
   
 20. rugumisa

  rugumisa Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini na wewe muandishi wa huu uzi umepotosha kidogo.Kutoka gazeti la East Africa la wiki hii na iliyopita liripoti kuwa hiyo highway imejengwa kwa msaada wa nchi ya moja ya kiasia ambayo ni china.na miradi mingi ya kijenga miundombinu ya kenya ni misaada ya China na Japan (kupitia JICA).kwani na sisi tunashindwa kutopa hela china?na kwa hiyo hawajajenga highway kutoka mapato ya ndani-kodi.
   
Loading...