Kubenea shujaa akiichunguza serikali, akijichunguza ni uchwara. Ngoma bado mbichi

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
mhe :Kubenea mbunge Ubungo kupitia Chadema,jana kwenye gazeti lake mwanahalisi liliandika habari ya kupotea Ben Saanane hali hiyo imezusha hasira kali kutoka kwa BAVICHA walioko kwenye mitandao ya kijamii wengi wakipinga habari yake kuwa ni uongo na uzushi...

Pamoja na mashambulizi hayo ya BAVICHA kwenda kwà Kubenea bado wanakiri Kubenea alijizolea sifa kwa kuandika habari za uchunguzi.

MKUKI KWA NGURUWE, KWA BINADAMU MCHUNGU.

Chini ni maoni ya BAVICHA kupitia mtandao wa facebook

Na Daniel Ezekiel Daniel

SAED KUBENEA MBUNGE WA UBUNGO (CHADEMA) AKAMATWE NA KUHOJIWA

Leo siku yangu imeharibika kabisa kutokana na Gazeti la MwanaHalisi kuandika habari ya kitapeli kuhusu kikaratasi kilichoandikwa kwa mkono na kutupwa mlangoni mwa kampuni ya Hali Halisi Publishers kuhusu kupotea kwa Ben Ben-Rabiu Wa Saanane

Naita ni habari ya kitapeli mana Ni habari iliyotumika kurubuni wanunuzi ili kuwalaghai na kupata manunuzi kwa gharana ya maisha ya Mtu. MwanaHalisi limejipotezea heshima mbele ya umma.

Saed Kubenea akamatwe aeleze kwa kina Ben Saa Nane yuko wapi??? Inaonesha anajua alipo Ben Saanane. Utu wa mtu Ni muhimu na wa thamani Sana kuliko mauzo ya gazeti.

Nimejilazimisha Sana kutoandika chochote kuhusu hili, lakini nimeshindwa. KUBENEA akamatwe awekwe Chini ya ulinzi aeleze Ben yuko kijiwe gani cha kahawa.

BringBackBenAlive.

Na Respicius Francis

AIBU KUBWA KWA MWANAHALISI
1.Nimetoka kusoma gazeti la mwanahalisi lenye kicwa chabari 'Msaidizi wa mbowe kuibuka 'ambaye ni Ben saanane aliyetoweka kwenye mazingira ya utata.
Mwaandishi wa mwanahalsi anasema walipata habari kuwa Ben amejificha kwa marafiki zake baada ya mtu mmoja kuandika andiko lililoachwa kwenye lengo la gazeti hiyo kwenye mtaa kasaba maeneo ya kinondoni ,,,,
2.Mwaandishi wa mwanahalisi anasema mjumbe mmoja wa kamati kuu chadema [cc] aliwambia mwanahalisi kuwa ana wasiwasi kama Ben amepotea kweli kwasababu inawezekana ukawa mkakati wake kisiasa maana Ben amekuwa akionekana kutaka kukwea madaraka haraka nje ya utaratibu...
3.Maelezo mengine kwenye gazeti hilo ni longo longo tu,wala hiyo habari haina uchunguzi wowote wakina zaidi naweza kusema walilenga kuuza gazeti lao maana kichwa cha habari ni tofauti kabisa na kilichoandikwa ndani kwasababu amesema msaidizi wa Mbowe kuibuka lakini kwenye habari ndani hawajasema ataibuka lini zaidi wameishia kuandika longo longo sizizokuwa na uchunguzi wa kina ,
MY TAKE.
Kwanza niseme ukweli gazeti la mwanahalisi wametukosea sana na wamejishuka heshima mbele ya jamii kwasababu habari ambayo imepamba gazeti lao imejaa taarifa za kuunga unga ambazo hazina uchunguzi wakina wala utafiti wowote .
-Hivi unaweza kuamini kivipi ujumbe ambao unaukuta mlangoni kwako bila kufanya uchunguzi ?? yani mtu kuandika kikaratasi chenye maneno kuwa Ben yupo anaoneka kwa marafiki zake, Mwanahalisi bila kutumia akili au kuangalia familia yake inapata shida gani wanakuja kutuambia Eti Beni amejificha marafiki zake, chanzo cha habari kuwa Ben yupo kwa marafiki ni kikaratasi chanye ujumbe ambacho walikikuta mlangoni mwao,,,, Hakika hii ni aibu kwa gazeti kubwa kama mwanahalsi kuandika habari uchwara kama hii wakati tukioa hili linaumiza watu akili ??
-Mwanahalsi wanasema kuwa mjumbe mmoja kamati chadema ana wasiwasi kuwa Ben kupotea wake ni mkakati kisiasa kwasababu amekuwa anaonesha kutaka kukwea madaraka haraka bila kufuata taratibu, Hii ni aibu kwa mwanahalsi hivi katika sakata hili nyeti la Kupotea hivi utaandikaje habari za hisia?? maana huyu ambaye anajiita mjumbe wa kamati kuuu chadema hana uhakika na alichoangea ...Lakini gazeti la mwanahalsi ambalo hapo mwanzao lilpata sifa kwa kuandika habari za uchunguzi wametuaminisha kuwa Ben yupo kwa marafiki zake amejificha kupitia vyanzo vikuu viwli vya habari ambavyo ni
-Kupitia kikarati chenye ujumbe kilichokutwa mlangoni kwenye ya mwanahalisi kikisema Ben yupo kwa marafiki zake,
-Kupitia mjumbe wa kamati kuu Chadema ambaye alisema ana wasiwasi kuwa uenda Ben Saanane anafanya mkakati wa kisiasa lakini hakuwa uhakika moja kwa moja ...

Mwisho namshauri mmiliki wa Gazeti hilo Mhe:Kubenea alitazame upya gazeti lake haiwezekani gazeti la mwanahalisi likageuzwa kama gazeti ujumaa,kiu,Sani,,Hakika Kubene pamoja na gazeti lako umetutia aibu

Na Bob Chacha WangweNimesoma gazeti la Mwanahalisi kuhusu habari ya Ben. Sikupenda kusema chochote baada ya dokezo la last week kuhusu habari ile ya kuonekana kwa mwana mpotevu Ben.

Nilifanya vile baada ya kugundua andiko lile lilitoka kwa mwandishi wa siku nyingi Kubenea. Nimesoma makala ya leo lakini nimegundua mambo makuu matatu. Mosi, bila baadhi ya watumiaji wa mitandoa kulaani aina ya habari ile, huenda leo Mwanahalisi ingekuja na habari ya udaku zaidi. Pili, nimegundua pia kwanini, Mwandishi na mchambuzi wa siku nyingi ambaye ndiye mwandishi wa makala ya leo Mhe Kubenea hakuambatanisha jina lake (ametumia 'Na Mwandishi wetu') Hii ni kutokana na aina ya uandishi uliotumika(uandishi njano).

Tatu, habari ya Ben, ni business oriented. Iliandikwa kwa lengo la kibiashara. In short, hamna kitu kipya zaidi ya utunzi pengine unaongozwa na chuki.

Kubenea ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mwanahalisi, ni kati ya waandishi wachache nchi hii wanaofanya uandishi wa kiuchunguzi(investigative journalism) lakini katika hili la Ben ametuangusha sana.
Nachelea kusema, amefanya uchunguzi wa kiwango cha chini sana. Alipaswa kufanya uchunguzi zaidi.

Kwamba chanzo cha kwamba Ben anaonekana mitaani ni kikaratasi kilichoachwa katika ofisi za gazeti hilo. Kwamba Ben ni mtu mwenye kutaka kupata madaraka bila taratibu na maneno mengine ya aina hiyo yanayolenga kumchora kijana huyo kama mtu asiyekuwa mwaminifu yametoka kwa mjumbe wa CC na Makao Makuu. Inawezekana kabisa, hii ni mbinu ya kujiandaa kukabiliana na mkakati wowote muovu wa kisiasa unaoweza kufanywa na wanaohisiwa kuwa watesi wake, lakini kutumia taarifa za kuunga unga kwenye uhai wa mtu mwingine kwa lengo hilo na lengo la kibiashara, sio jambo la kiungwana hata kidogo.

Tunahitaji sana kupata habari za kiuchunguzi zinazohusiana na tukio hili la kupotea kwa huyu kijana ambaye siku zote amekuwa mstari wa mbele kulipigania taifa hili kwa namna mbalimbali. Nashauri uchunguzi uendelee kufanyika. Huu uchunguzi uliofanyika si sehemu ya investigative journalism. Ni uchunguzi uchwara.

Kama kuna kitu chochote cha kisiasa kitafanyika kwa lengo la kutuhujumu kama chama kitabainika tu. Nchi hii sio ya wajinga. Kama kuna mchezo wowote umefanywa na mtu au kikundi cha watu au pengine mwanampotevu mwenyewe, itabainika tu. Na ikibanika, operation itahamia kwa huyo au hao watakao kuwa wamefanya hivyo ili wachukuliwe hatua kali. Hofu ya aina yoyote tusiiruhusu iturudishe nyuma katikati ya mapambano ya kumtafuta ndugu, rafiki na mtanzania mwenzetu kwakuwa hatujui kilichomsibu. Ni hatari sana ku-draw conclusion kwa kutumia hisia au uchunguzi fyongo kama wa Mwanahalisi.

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]

©Bob Wangwe

Na Malisa GJ

TAARIFA ZA KUONEKANA KWA BEN, NA HEKAYA ZA "KIKARATASI" OFISI ZA MWANAHALISI.

By Malisa GJ,

Mwanahalisi waliweka kidokezo wiki iliyopita kuwa Ben anaonekana mtaani na kwenye vijiwe vya kahawa. Kisha wakamnukuu mjumbe mmoja wa kamati kuu aliyedai kuwa "Ben kajificha ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa"

Wakaahidi kwamba toleo la jumatatu ya leo Januaru 02, 2017 wangekuja na taarifa kamili. Kabla ya taarifa hiyo nilihoji mambo machache kuhusu kidokezo hicho cha habari. Nikahoji Ben ameonekana mtaa gani (vijiwe gani vya kahawa)? Lini? Akiwa na nani? Aliyemuona ni nani? Na mjumbe wa kamati kuu aliyesema Ben kajificha ni nani?

Baada ya kuhoji nikapokea maoni tofauti. Baadhi wakisema MwanaHalisi hawajui Ben alipo ila habari hiyo ni "kick" ya kuuza gazeti, na wengine wakasema tusihukumu kabla habari yenyewe kutoka. Tusubiri habari kamili ili tuweze kuhoji tukiwa na taarifa za kutosha.

Mhe.Kubenea alinitafuta kwa simu na tukaongea kwa kirefu kuhusu habari hiyo. Moja ya mambo aliyoniambia Kubenea ni kwamba, Kwanini sikusubiri habari hiyo itoke ndipo nitoe maoni? Nawezaje kutoa maoni kwenye kidokezo cha habari badala ya kusubiri habari kamili.

Hatimaye leo nimesoma habari kamili kwenye gazeti la MwanaHalisi kama ilivyokua ikisubiriwa na wengi. Kama ambavyo wengi tukitegemea gazeti la leo lingejibu maswali yote muhimu niliyouliza wiki jana. Yani Ben ameonekana mtaa gani? Lini? Alionwa na nani? Kwanini aliyemuona hakutoa taarifa polisi? Kwanini Ben ajifiche mtaani na kuiweka familia yake, chama chake na marafiki zake kwenye taharuki? Ben analindwa na intelijensia gani kiasi kwamba anaweza kujificha na Polisi wakashindwa kumpata?

Maswali haya nilitegemea yajibiwe kwa ufasaha kupitia MwanaHalisi ya leo. Lakini MwanaHalisi wameshindwa kujibu hata swali moja kati ya hayo. Yani wameongeza maswali badala ya kujibu maswali. Inaonekana ilikua mbinu ya kuuza gazeti.

MwanaHalisi wanadai taarifa za Ben kuonekana mtaani wamezipata kwenye andiko la mkono (kikaratasi) lilioachwa ofisini kwao mtaa wa Kasaba, Kinondoni na mtu asiyejulikana. Yani kuna mtu asiyejulikana alienda na kikaratasi akakiweka chini ya mlango ofisi za MwanaHalisi.

Kikaratasi hicho kinasomeka "Hamumfahamu Saanane. Sisi tunajua alipo. Wala hatuoni anayetishia maisha yake. Kuna wanaodai kauawa, ni waongo. Kuna kitu wanaandaa, kaa chonjo."

Kwahiyo eti wakatumia kikaratasi hicho kama source ya habari yao. Kikaratasi kilichowekwa na mtu asiyejulikana kinageuka kuwa credible source ya gazeti. Haya ni Maajabu.!

Yani gazeti kubwa lenye heshima kubwa kama MwanaHalisi linaacha kuamini vyanzo vya uhakika linakimbilia kuamini vikaratasi vilivyowekwa na mtu asiyejulikana? Hii ni aibu.

Mhe.Mbowe akiwa mkoani Mbeya alisema Ben ametekwa na hapendi kuongelea sana suala hilo ili watekaji wasije kumdhuru. Inaonekana MwanaHalisi hawakuamini taarifa hiyo ya Mbowe.

Lissu katika mkutano wake na wanahabari akasema inawezekana Ben anashikiliwa na dola kutokana na maandiko yake ya kukosoa serikali hasa elimu ya JPM. Lissu akafika mbali na kueleza kuwa anajua maeneo jijini Dar yanayotumika kutesa wakosoaji wa serikali, na akahofia huenda Ben yumo humo. Inavyoonekana MwanaHalisi pia hawakuamini taarifa za Lissu.

Waziri Mwigulu Nchemba nae akatoa tamko kuhusu Ben akidai ni rafiki yake, akisema anasikitishwa na taarifa za kupotea kwake na kwamba serikali inafanya uchunguzi. Lakini inaonekana MwanaHalisi hawakuziamini pia taarifa hizi.

Jeshi la Polisi makao makuu, kupitia kwa Kamishna Robert Boaz, December 21 mwaka huu lilitoa taarifa kuwa wanafanya uchunguzi juu ya taarifa za kupotea kwa Ben. Sikusikia MwanaHalisi wakisema kitu kuhusu hili.

Lakini cha ajabu wamekuja kuamini kikaratasi kilichowekwa na mtu asiyejukikana. Yani hawakuamini taarifa ya Mbowe, hawakuamini maelezo ya Lissu, hawakuamini taarifa ya jeshi la polisi, hawakuamini taarifa ya Mhe.Mwigulu, lakini wamekuja kuamini kikaratasi kilichowekwa ofisini kwao na mtu asiyejulikana. Ridiculous.!!

Yani taarifa ya kikaratasi zimepewa uzito kuliko taarifa iliyotolewa na Mhe.Mbowe, Mhe.Mwigulu, Jeshi la Polisi na Mhe.Lissu.?? Haya ni Maajabu ya kikaratasi. Kwanini MwanaHalisi waamini zaidi taarifa za kikaratasi kilichoandikwa na watu wasiojulikana kuliko kuamini taarifa rasmi zilizotolewa na vyombo vinavyoshughulikia suala hilo? Hivi kati ya kikaratasi kilichookotwa ofisi na Lissu nani anapaswa kuaminiwa?

Kikaratasi ambacho MwanaHalisi wamekitumia kama source ya habari yao kimeongeza maswali badala ya kujibu maswali ya awali. Kwanini kikaratasi hicho kipelekwe Mwanahalisi tu na sio media house nyingine kama Mwananchi, Majira etc? Kwanini waliokiweka wafiche identity zao? Kama kweli walimuona Ben mtaani kwanini hawakutaja hiyo mitaa?

Kama ofisi za Mwanahalisi zina walinzi usiku na mchana, iweje mtu aje na kikaratasi akiweke chini ya mlango bila kujulikana? Nadhani MwanaHalisi wanahitaji kujieleza vzr kuhusu ukweli wa kikaratasi hicho. Otherwise tutaamini kimeandikwa na watu wa humohumo ndani ili kupenyeza agenda yao kuhusu Ben, kisha kujifanya hawajui kilipotoka.

Nashauri Polisi wachunguze vizuri juu ya ukweli wa kikaratasi hicho. Huenda kuna mengi sana nyuma ya pazia kuhusu hicho kikaratasi.

Kwa ujumla habari ya leo kwenye MwanaHalisi kuhusu Ben imekua na impacts mbili kubwa.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]: imepunguza heshima ya gazeti mbele ya jamii. Wapo watu wameanza kulipuuza gazeti hili baada ya kusoma habari ya leo. Baada ya gazeti kutoa tuhuma kwamba Ben yupo mtaani, wengi walitegemea leo wapate majibu yko wapi, kwahiyo kitendo cha gazeti hilo kushindwa kudhibitisha madai yake, na badala yake wakaja na hekaya za kikaratasi na kujifanya kimetoka kwa watu wasiojulikana. Heshima ya gazeti imepungua.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; habari ya leo imefanya watu wahisi imeandikwa kwa msukumo wa chuki kutokana na tofauti ambazo zimewahi kuwepo kati ya Ben na Kubenea ambaye ni mkurugenzi wa gazeti hilo. Hii ni kwa sababu badala ya gazeti hilo kueleza Ben alipo, limeeleza mambo mengi negative kuhusu Ben ambayo hayakua na ulazima wa kuandikwa leo. Kwa mfano katika aya ya 8 &9 mwandishi ameeleza kuwa Ben aliwahi kumrekodi Dr.Slaa, na kutaka kumpa sumu Zitto Kabwe. Tuhuma hizi za miaka 8 iliyopita hazikua na sababu ya kuandikwa leo.

Kama agenda kuu ni kujua Ben alipo, kwanini wamechomekea mambo yasiyohusiana na agenda hiyo? Mara Ben alitaka kumuwekea sumu Zitto, mara Ben alimrekodi Dr.Slaa, so what?? Hayo yanahusiana nini na kupotea kwa Ben? Hivi watu wakisema habari hii imeandikwa kwa msukumo wa chuki binafsi MwanaHalisi watabisha?

Nashauri menejimenti ya MwanaHalisi ijitafari upya kuhusu siala hili. Tunalijua MwanaHalisi kama gazeti bingwa la habari za uchunguzi, sio MwanaHalisi ya udaku kama ya leo.

Tulitegemea habari ya leo ihitimishe mjadala wa Ben. Tulitegemea kupitia gazeti la leo umma wa watanzania ujue Ben amejificha wapi, kwanini ajifiche? Alionekana lini? Sio kutuletea hekaya za "kikaratasi" kilichoandikwa na watu wasiojulikana. Hii ni aibu.

Gazeti kubwa la uchunguzi lenye heshima kama MwanaHalisi kutegemea source ya vikaratasi kutoka kwa watu wasiojulikana, ni aibu kubwa. By the way kama mnakiri kikaratasi kimewekwa na watu wasiojulikana it means mmeshindwa kujua aliyeandika hicho kikaratasi hicho. Sasa je mtawezaje kumjua aliyemficha Ben, kama mmeshindwa kumjua mwandishi wa kikaratasi? Jitafakarini upya. Mmeanza kupoteza heshima yenu kubwa mliyoijenga kwa jamii kwa muda mrefu. Jisahihisheni. Acheni chuki kwenye mambo yanayohusu uhai wa mtu. Bado mna nafasi ya kujisahihisha, itz not too late yet.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!Na Joseph Alex

Nimesoma gazeti la mwanahalisi juu ya kupotea Ben Saanane.
Kubenea na Gazeti lake wameandika habari ambayo ilitakiwa iandikwe na magazeti Ujumaa,Kiu na sani lakini siyo mwanahalsi kama tulivyozea kuiliita Gazeti la uchunguzi..
Wakati tupo kwenye kipindi kigumu cha kumtafuta Ben gazeti kubwa ambalo linaheshimika kwa kuandika habari za uchunguzi wanakuja habari yenye 'kichwa cha habari chenye kuleta matumaini kuwa Msaidizi wa Mbowe kuibuka' lakini ndani ya gazeti wanatueleza udaku ambao tulizoe kuukuta kwenye magazeti ya Eric Shigongo,
Gazeti la Kubenea linasema kuwa Ben amejificha kwa marafiki zake kwasababu yupo mtu aliandika ujumbe wa maandishi na kuutupa mlangoni ofisni kwa Kubenea akisema Ben yupo isipokuwa amejifichwa kwa marafiki zake,Ni aibu kwa Gazeti kubwa kama Mwanahalisi kuchukua chanzo kimoja cha habari tena chanzo dhaifu kuaminisha umma kuwa Ben amejificha kwa Marafiki zake bila kufanya uchunguzi wa Kina ...Kisa wameamka asubuhi na kukuta kikaratasi mlangoni mwao kimeandikwa na mtu hasiyejulika kuwa Ben yupo amejificha kwa Mrafiki zake,
Gazeti la Kubenea linasema Mjumbe mmoja wa kamati kuu Chadema ana wasiwasi uenda Ben akawa anafanya mkakati wa kisiasa maana amekuwa akionekana kutaka kukwea madaraka haraka hata nje ya taratibu, lakini huyu mjumbe bado hana uhakika isipokuwa anaongea kwa hisia tu, Hapa Mwanahalisi wameonyesha udhaifu mkubwa maana kwenye tukio hili walitakiwa kuandika habari ya uchunguzi siyo habari za hisia .
Hakika lengo la gazeti la mwanahalisi kwa siku ya leo ilikuwa ni kibiashara ,Kueneza propanda, Kuonyesha chuki za wazi maana zipo taarifa kuwa mmiliki wa Gazeti hilio Ndugu Kubenea hana mahusiano mazuri ya kisiasa na Ben kwahiyo anatumia gazeti lake kumchafua Ben na kuandika habari ambazo hazina ukweli wowote..
Haiwezekani Mwanahalisi wanatumia vyanzo uchwara vya habari kuaminisha umma kuwa Ben amejificha kwa Mafiki zake bila kutuletea habari uchunguzi ..
Nitoe wito kwa Kubenea kuacha kuandika habari za hisia ambazo hazina uhakika ni bora ukabaki kimya zaidi ya kupotosha ummaNa Josephat Keraryo Nyambeya

Kubenea and his bullshit gazette MWANAHALISI have ruined my day. ..Ukanjanja wa kutafuta kiki ya kibiashara kwenye mambo serious ni zaidi ya ujinga ...Kimsingi mimi mmenipoteza hamtonipata tena kwenye hilo gazeti lenu . Sasa nimethibitisha ile chuki na uhasama uliopo kati ya Kubenea mhariri mtendaji wa Mwanahalisi na Ben Saanane , Mwanahalisi imetoa watu kwenye mstari for their own interests . Hili halipaswi kunyamaziwa
 
TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,876
2,000
Kambi ya Mbowe na Kambi ya Lissu zinaumana. Nasikia Lissu naye anautafuta uwenyekiti. Ben alikuwa anaelekea kuasi kuelekea kwa Lissu. Kubenea ni Team Mbowe+Lowassa. Hizo ni za chini ya carpet.
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,499
2,000
Ajabu ya filauni Lumumba kumpongeza Kubenea, endeleeni kuicheza ngoma ya Chadema mtakaposhituka kumekucha.
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,499
2,000
Kambi ya Mbowe na Kambi ya Lissu zinaumana. Nasikia Lissu naye anautafuta uwenyekiti. Ben alikuwa anaelekea kuasi kuelekea kwa Lissu. Kubenea ni Team Mbowe+Lowassa. Hizo ni za chini ya carpet.
Hata bila mikutano Chadema mtaitangaza wenyewe.
 
MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
5,260
2,000
Nanukuu
"Kuwa BAVICHA au UVCCM kindakindaki it's like someone who lost half of his/her brain "
Prof Shivji 15.07.2016
 
Sir Kite 2

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
554
500
Hivi ingetokea kubenua akaandika ben katekwa na serikali wangemshambulia kweli zaidi ya kumpongeza
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Hivi muanzisha Uzi ulitegemea kuzungumzia nini au majipu na viwanda uchwara huko Bongo ?
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,300
2,000
Hivi BAVICHA humu katika mitandao huwa wanakuja na kadi zao au hata wale Lumumba anaweza kuwa BAVICHA pia?
 
Ngapulila

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
757
1,000

Penye ukweli Giza hujitenga.Mkimaliza mtuambie Ben yupo wapi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom