Hivi Wakenya wametushinda nini?

Hivi Wakenya wametushinda nini?

aliyewaroga alifariki mwaka 1999 na mlimzika kwa mbwembwe!

yeye alikalia ukombozi wa afrika wakati kwake kunaoza. Alifunga mpaka na kenya baada ya kuvunjika ea community wakati hatukuwa na viwanda tukawa hatuna hata sabuni za kuogea.
 
Walianza kama sisi' Walikuwa na Mafisadi wengi tu, wakawashitaki kwa kuwapeleka Mahakamani na kutaka pesa zilipwe au

Waende Jela, wakasafisha Ufisadi na sasa ni Wasafi sasa wameanza kuipenda Nchi yao Kimaendeleo; Sisi tutaweza lakini

Sio kwa CCM kuwapa uongozi Vijana kwa Manufaa ya Kikwete's Prince apatiwe Uongozi na hao Vitoto vilivyo pandikizwa

Madaraka haraka haraka na Rais Kikwete; Ujanja huo una uwalakini sababu hautainufaisha nchi itaturudisha nyuma.
 
sisi watanzania na wao ni wakenya wala usitulinganishe nao unachotakiwa kujadili ni jinsi gani tuendeleze nchi yetu. vitu vingine havina maana yoyote hapa.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Wakenya na Watanzania lakini kubwa ni kwamba wenzetu wanachapa kazi, sisi tumelala. Niliwahi kufika mpakani mwa Tanzania na Kenya, Isebania (Kenya) na Sirari(Tanzania) usiku wa manane natokea Nairobi kuja Tanzania. Sikiliza kioja. Upande wa Kenya haukuwa na umeme, sijui siku hizi, lakini Maafisa Uhamiaji wa Kenya walitumia taa za kandili kutugongea haraka passport zetu tukaingia Tanzania. Loo! kufika Tanzania, kwenye umeme tukakuta miafisa uhamiaji yetu imelala, siyo ofisini, bali majumbani mwao na ofisi imefungwa. Tulilazimika kuyasubiri mavivu yetu yajivute wakati kumekucha kabisa, napo taratiiibu na tukagongewa passport zetu. Tulikaa upande wa Tanzania kwa saa 5. Je, unaweza kujiuliza kwa kutuchelewesha pale ni watu wangapi walichelewa katika biashara zao? Haya, wakati Kenya usiku ndo wanafanya biashara nchi nzima, maana usafiri unaendelea, ati Tanzania waliambiwa na Ziraili kuwa ikifika saa 4 usiku mabus yasisafiri kuna ajali. Utalinganaje na Kenya, wakati wao usiku wanafanya kazi, Tanzania wanalala, na huenda ndo nchi pekee duniani ambayo huzuia watu wake kusafiri usiku. Wanatuzidi kwa mengi, tena yaliyo chini ya uwezo wetu! Utadhani tumeshushiwa laana! Kipindi hicho ili ufike Mwanza, ilibidi upitie Kenya, maana yake tulikuwa tunawapelekea uchumi. Kisa, barabara. Sitaki kuendelea ntalia bure.....

Hamia Kenya Mkuu, unasubiri nini????
 
Wekeni utaifa mbele, Acheni kujidharau na kujidhalilisha. Hili ndio linalotuua.

Kufungia ukweli nje hakutatusaidia kitu, kuna mambo inabidi tujifunze kwa wakenya. Mf. mwishoni mwa 2011 walikuwa na inflation mbaya kuliko sisi, lakini walipoamua kupambana nayo imeshuka kwa kasi kuliko matarajio ya wengi. Hapa hm watu wanavuana magamba, running up and down like headless chicken, hakuna kinachoendelea.

Mkuuu wa kaya ana majukumu makuu matatu, kuteua, kusafiri na kuahani misiba, hatuwezi kuendelea namna hii.

Culture pia inatusumbua, wakenya hujipeleka mbele kwa kila jambo kitu ambacho hapa kwetu ni kitu kibaya tuinata kiherehere. Lakini hicho "kiherehere" kinawasaidia wakenya kupata ajira, position kubwa, business deals kubwa kubwa n.k. lazima tuige haya
 
Yote tisa, kumi ni kwamba:
1. Nyumba usiyolala hujui kunguni wake,
2. Utamu wa ngoma ingia ucheze mwenyewe,
3. Usoweza kuukata ubusu,
4. Ukiona ambari zinduna iko nyuma,

Nawe ongeza zako zinazoonyesha kwamba eidha;
i. Umetambua udhaifu wetu, au
ii. Unatamani mabadiliko toka rohoni, au
iii. Umekiri kwamba wakenya wametuzidi, au
iv. Umesifia/kudharau Kenya na wakenya kwa kujua/kutokujua kwa usahihi kilichoko nyuma ya pazia, au
v. Uko tayari kuhakikisha unaifikia TANZANIA TUITAKAYO!:israel:
 
Hakuna mfumo mbaya duniani kama UJAMAA kwa watu wasio na fikra thabiti....kwa watu hawa ujamaa humaanisha kula kutokana na uwezo wa kupiga porojo....wakati wa ujamaa watu walipata hela lakini kujenga mh..full kula bata.....ujamaa ni kuwa na uhakika serikali itakupa hata kama umelala....watoto watasoma na kula.
Kwa waliopitia ujamaa baada ya kuwa na mfumo wa ubepari wao ni tofauti na sisi (hatujafika hata slavery) eti ujamaa.
Kenya maisha yao hayategemei zaidi serikali....kula na kuishi hakutegemei uswahiba,ukuwadi na porojo...labda ukabila (wakikuyu)....Mkenya akipata nafasi hasa marginalised groups (wajaluo,wanandi,wakamba) hufanya kweli...wapo kibao nchi za watu wakijituma kwa bidii....kupata ardhi nairobi ni sawa na kununua nyumba masaki....hata kupanga westlands,harnington,huruma,estates,embassy n.k ni issue kwa nini wasijitume.
Mtu uswahiba na mtoto wa Rais tayari mkuu wa wilaya kwa nini usibweteke......pia wao ni visionary,angalia hata banks&supermarket zao with branches in Tz (why not us?).
 
7293527580_6750ff3295_b.jpg

Don, picha nzuri hii, naomba niicopy please! Ili hata kama sitaenda Nairobi (7bu fly overs ze2 hazitafanana hii), niseme nshawahi kuiona.
 
Godfrey Mwampembwa aka GADO ni Mtanzania ambaye amekuwa tajiri kupitia Kenya

Je waweza kumfananisha na Masudi Kipanya?

Je ingekuwa Masudi Kipanya ni Mkenya na anachora magamba vile angekuwa wapi now?

Julizeni hii Jamii forum ingekuwa owned na wakenya hali ingekuwaje? au tuseme JAMII MEDIA ingekuwa ni ya wakenya zile monthly press conference za serikalini waandishi wa jamii media wangekuwaje?

Hivi mnajua UAE kuna wakenya wangapi wanafanya kazi kule?

baloz wa UAE Tanzania aliwahi kulalamika kuwa nafasi za kazi zikitangazwa Emirates watanzania eidha ni hawaombi na wanaoomba hawawezi kushindana na waKenya

Jiulizeni kwa nini International Organisations nyingi zimeweka base Nairobi?

Tazama sasa wana commuter railway mjini Nairobi



AuDWM9QCIAEnUEM.jpg:large
 
Last edited by a moderator:
siasa ya ujamaa ukichanganya na joto la dar imechangia sana kuharibu akili zetu
 
Mkuu kenya wanatumia ENGLISH kama lugha ya taifa, unajua kiswahili kimeturudisha nyuma sana
 
kinachotufanya watanzania tusiendelee ni uthubutu hatuna.Magufuli akitangaza kung'oa nyumba za barabarani mnamuona hana huruma,ndio maana hii nchi inabidi tupate raisi dikteta kwa maslai ya vizazi vijavyo.sio kauli za akina pinda kutukatisha tamaa kwamba ukiwachukulia hatua mafisadi inchi itayumba.!
 
Kuna sifa moja kubwa ya wabongo mmeisahau 'STEALING' ktk hili tumekubuhu.
 
ITV kuna program inaitwa "SHAMBA SHAPE-UP SAFARI"..........

Ukikiangalia utaona intergration ya mashirika mbalimbali ya kilimo ya Kenya au ya kimataifa jinsi yanavyofanya marketing..

Tatizo letu........... lol.......

Kila Mtanzania anauwezo wa kueleza tatizo la Mtanzania......
 
Godfrey Mwampembwa aka GADO ni Mtanzania ambaye amekuwa tajiri kupitia Kenya

Je waweza kumfananisha na Masudi Kipanya?

Je ingekuwa Masudi Kipanya ni Mkenya na anachora magamba vile angekuwa wapi now?

Julizeni hii Jamii forum ingekuwa owned na wakenya hali ingekuwaje? au tuseme JAMII MEDIA ingekuwa ni ya wakenya zile monthly press conference za serikalini waandishi wa jamii media wangekuwaje?

Hivi mnajua UAE kuna wakenya wangapi wanafanya kazi kule?

baloz wa UAE Tanzania aliwahi kulalamika kuwa nafasi za kazi zikitangazwa Emirates watanzania eidha ni hawaombi na wanaoomba hawawezi kushindana na waKenya

Jiulizeni kwa nini International Organisations nyingi zimeweka base Nairobi?

Tazama sasa wana commuter railway mjini Nairobi



AuDWM9QCIAEnUEM.jpg:large


Kama unaakili timamu ni ngumu sana kuwachukia Wakenya......!

Mwenye kubisha aweke picha za Tazara na TRL (hadi kichefuchefu kuyataja)
 
Last edited by a moderator:
Kivipi mkuu?

mkuu ndyoko, we fikiria ukitaka kusoma vitabu vya kingereza kwanza unaanza kubadilisha neno kwenda kiswahili ndio ulielewe, we angalia wakenye wangapi wanafanya kazi kwenye english speaking countries ukifananisha na waswahili. Yote haya ni kwa sababu ya NYERERE, we unaleta so called "lugha ya taifa" kwa linchi masikini kama letu ukajifananishe na wachina?
 
Last edited by a moderator:
Ni rahisi sana kusifia kitu ukiwa mbali. Mleta mada naomba aishi Kenya kwa mwezi mmoja tu alafu atuletee report.
 
inawezekana viongozi wetu wa think small

mimi ht sijui sababu

ni nchi ya ajabu kuwa wananchi wameunganishwa lakini hakuna mwenye kujua hati za huo muungano ziko wapi...including Attorney General
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom