Mi bado sijashindwa bado napambana labda wewe wamekushinda
Nakuunga mkono.
Mi bado sijashindwa bado napambana labda wewe wamekushinda
Sisi tumewazidi kufisadi na uvivu.
Nchi yetu imetoa kipaumbele kwa siasa na wanasiasa toka zamani!! Na siasa ikachukuliwa kama longo longo na uswahili mwingi. Unafiki ni wa hali ya juu TZ na siasa iliyokuwa inasisitiza kuwa serikali italetea maendeleo watu wake! bila kujibidisha. Hiyo mentality imekuwepo hadi leo. Kenya toka zamani ulikuwa uchumi huria na ukicheza kidogo unakufa njaa. Hakuna urafiki wa kusaidiana wala kuoneana huruma. Niko kwao kikazi na hadi sasa sijui jirani yangu wa nyumba ya karibu anafananaje mwaka wa pili huu!! Hakuna kuombana chumvi hapa. Usipohangaika unakufa kweli hakuna utani. Hapo nyumbani tunaelekea huko toka tuingie uchumi huria. Dalili zote zipo wazi. Chama tawala bado kinataka wananchi wasifanye uchambuzi!! lakini njaa inapozidi wote wataamua kufanya kazi siyo mchezoUkikutana nao nje ya nchi wana confidence za kufa mtu. wakiwa kwao hawataki longo longo na kama hawaelewani watapigana mikwaju kisha wanadeliver
Tazama KTN au KBC picha ziko clear, news zimetulia, watangazaji wametulia
Soma gazeti la NATION au Standard...huwezi fananisha na lile gazeti la Michuzi (daily nyuz) au lile la copy and paste (guardian)
sisi tuna watu wengi zaidi, rasili mali nyingi zaidi, wanasiasa wengi zaidi, vyama vya siasa vingi zaidi, magazeti mengi zaidi, JF ndio zaidi, cabinet yetu kubwa kuliko ya kwao, katiba yao (na mahakama ya kadhi ndani) ndio walipitisha, sasa kwa nini hawa wana deliver na sisi hatuna kitu?
I've tried to hate them lakini nimeshindwa, cant hate their ambition esp based on their national interest.
Halafu wao kujenga li Superhighway kama hili ili iweje?
ahh sisi hata kuthubutu tunashindwa sijui kwa nini
Ukitaka kuendelea lazima uwe na roho mbaya. Wametuzidi roho mbaya na utu hawana kabisa, Pesa mbele utu nyuma.
Kuna tofauti kubwa kati ya Wakenya na Watanzania lakini kubwa ni kwamba wenzetu wanachapa kazi, sisi tumelala. Niliwahi kufika mpakani mwa Tanzania na Kenya, Isebania (Kenya) na Sirari(Tanzania) usiku wa manane natokea Nairobi kuja Tanzania. Sikiliza kioja. Upande wa Kenya haukuwa na umeme, sijui siku hizi, lakini Maafisa Uhamiaji wa Kenya walitumia taa za kandili kutugongea haraka passport zetu tukaingia Tanzania. Loo! kufika Tanzania, kwenye umeme tukakuta miafisa uhamiaji yetu imelala, siyo ofisini, bali majumbani mwao na ofisi imefungwa. Tulilazimika kuyasubiri mavivu yetu yajivute wakati kumekucha kabisa, napo taratiiibu na tukagongewa passport zetu. Tulikaa upande wa Tanzania kwa saa 5. Je, unaweza kujiuliza kwa kutuchelewesha pale ni watu wangapi walichelewa katika biashara zao? Haya, wakati Kenya usiku ndo wanafanya biashara nchi nzima, maana usafiri unaendelea, ati Tanzania waliambiwa na Ziraili kuwa ikifika saa 4 usiku mabus yasisafiri kuna ajali. Utalinganaje na Kenya, wakati wao usiku wanafanya kazi, Tanzania wanalala, na huenda ndo nchi pekee duniani ambayo huzuia watu wake kusafiri usiku. Wanatuzidi kwa mengi, tena yaliyo chini ya uwezo wetu! Utadhani tumeshushiwa laana! Kipindi hicho ili ufike Mwanza, ilibidi upitie Kenya, maana yake tulikuwa tunawapelekea uchumi. Kisa, barabara. Sitaki kuendelea ntalia bure.....
Hamia Kenya Mkuu, unasubiri nini????
Wametushinda vingi ikiwemo jana kupitisha sheria kwamba wabunge lazima wawe na angalau degree ya kwanza ili waweze kutoa hoja zenye mashiko badala ya jazba!
Natamani Bunge hili mwaka ujao lipitishe sheria kama hiyo ili wabunge wenye wasiokuwa na angalau shahada ya kwanza waende shule kwanza.
Ikipitishwa naona kama makundi kwa makundi ya wabunge wakienda kusoma BBA jioni pale UDOM!
Nyie wavivu sana kufanya kazi, nenda kwenye mashirika yenye wakenya hapa Tanzania utakuta wabongo wanalia lia eti wanaonewa! mmekalia uvivu tu
ndio mana nimejiunga nao kukamilisha ule usemi wa "IF YOU CANT BEAT THEM JOIN THEM".nakwenda nao sambamba aye for an aye,tooth for a tooth.[h=3][/h]Ukikutana nao nje ya nchi wana confidence za kufa mtu. wakiwa kwao hawataki longo longo na kama hawaelewani watapigana mikwaju kisha wanadeliver
Tazama KTN au KBC picha ziko clear, news zimetulia, watangazaji wametulia
Soma gazeti la NATION au Standard...huwezi fananisha na lile gazeti la Michuzi (daily nyuz) au lile la copy and paste (guardian)
sisi tuna watu wengi zaidi, rasili mali nyingi zaidi, wanasiasa wengi zaidi, vyama vya siasa vingi zaidi, magazeti mengi zaidi, JF ndio zaidi, cabinet yetu kubwa kuliko ya kwao, katiba yao (na mahakama ya kadhi ndani) ndio walipitisha, sasa kwa nini hawa wana deliver na sisi hatuna kitu?
I've tried to hate them lakini nimeshindwa, cant hate their ambition esp based on their national interest.
Halafu wao kujenga li Superhighway kama hili ili iweje?
ahh sisi hata kuthubutu tunashindwa sijui kwa nini
sisi mbona kazi tunafanya sana tuuu au?