Hivi Wakenya wametushinda nini?

Hivi Wakenya wametushinda nini?

Kuna tofauti kubwa kati ya Wakenya na Watanzania lakini kubwa ni kwamba wenzetu wanachapa kazi, sisi tumelala. Niliwahi kufika mpakani mwa Tanzania na Kenya, Isebania (Kenya) na Sirari(Tanzania) usiku wa manane natokea Nairobi kuja Tanzania. Sikiliza kioja. Upande wa Kenya haukuwa na umeme, sijui siku hizi, lakini Maafisa Uhamiaji wa Kenya walitumia taa za kandili kutugongea haraka passport zetu tukaingia Tanzania. Loo! kufika Tanzania, kwenye umeme tukakuta miafisa uhamiaji yetu imelala, siyo ofisini, bali majumbani mwao na ofisi imefungwa. Tulilazimika kuyasubiri mavivu yetu yajivute wakati kumekucha kabisa, napo taratiiibu na tukagongewa passport zetu. Tulikaa upande wa Tanzania kwa saa 5. Je, unaweza kujiuliza kwa kutuchelewesha pale ni watu wangapi walichelewa katika biashara zao? Haya, wakati Kenya usiku ndo wanafanya biashara nchi nzima, maana usafiri unaendelea, ati Tanzania waliambiwa na Ziraili kuwa ikifika saa 4 usiku mabus yasisafiri kuna ajali. Utalinganaje na Kenya, wakati wao usiku wanafanya kazi, Tanzania wanalala, na huenda ndo nchi pekee duniani ambayo huzuia watu wake kusafiri usiku. Wanatuzidi kwa mengi, tena yaliyo chini ya uwezo wetu! Utadhani tumeshushiwa laana! Kipindi hicho ili ufike Mwanza, ilibidi upitie Kenya, maana yake tulikuwa tunawapelekea uchumi. Kisa, barabara. Sitaki kuendelea ntalia bure.....
 
Wanajamvi!
Tuseme ukweli Wakenya wametuzidi kwa mengi. Wanajituma kwenye kazi, zaidi si spenders kama sisi(kuanzia serikali mpaka mtu binafsi mfano kwao waziri anapanda PASSAT(saloon car),unaweza kukuta MKENYA tajiri mwenye majumba kila kona na makampuni kadhaa anatembelea TOYOTA PROBOX. tembea kenya hususani miji mikubwa (Nairobi, Kisumu, Mombasa) uhesabu investments kubwa kubwa REAL ESTATES,APARTMENTS,MAJENGO MAKUBWA,SUPERMARKETS,KAMPUNI KUBWA za Insurance, Constructions, Media Houses (TV stations, Publishing), Airlines, kampuni za Mabasi yanayosafiri ndani na nchi jirani kwa aslimia kubwa yanamilikiwa na WAKENYA WENYEWE na wameajiri wakenya wenzao(suala la kabila gani ndo wanaajiriwa usiniulize leo, mimi naanagalia wakenya ndo walioajiriwa). Sasa njoo Tanzania SERIKALINI matumizi ni makubwa kupitiliza MAGARI ya kifahari, watanzania wa kawaida ni SPENDERS mtu anatembelea TOYOTA LAND CRUISER V8 lakini hana investment ya maana. Zaidi watanzania ni wavivu kupitiliza, nenda hoteli hapa Tanzania ukimka asubuhi ya saa 12 ukiuliza chai unaambiwa bado. nenda kalale hoteli za kenya saa 12 kasoro chai tayari so unakunywa chai then kama unasafiri muda huo unaendelea na safari zako.

KUBWA KUPITA YOTE, KENYA WANATHAMINI ELIMU KULIKO VITU VYOTE (nikisema elimu simaanishi elimu ya vyuo vikuu tu) kuanzia shule ya msingi, sekondari na kuendelea) kwao mpaka mtu wa Saloon anasomea na ukienda saloon utaona tofauti na saloon za kibongo). LUGHA YA KIINGEREZA nayo imetufanya tujione wanyonge sana mbele yao. Wakenya ni wepesi kutafuta opportunities Hapa USA wakenya wamejaa, ukienda Uk ndo usiseme, Saudi arabia, South Sudan, TZ, Uganda, South africa ndo balaa na wakipata hela zao wanaenda ku-invest kenya. ndio maana MAKABURU (SOUTH AFRICA) wanashindwa/wanapata wakati mgumu kuinvest kenya maana competition kenya tofauti na TZ hakuna competition na waTZ hawathamini bidhaa za kwao(TZ).
 
Kina Mwigulu na Komba huwa wakiambiwa haya wanasema ni kwasababu Kenya was a Crown colony yani ma-settlers waliijenga Kenya wakijua ya kwamba hapo ni kwao! Hizi huwa ni hoja mufilisi za magamba after eating like gluttons and throw out shit!

Watanzania wanafanya kazi sana na wanakatwa mi kodi mikubwa tu katika mapato yao, lakini fedha hizi zinapelekwa wapi ni kitu moja na utilization ya resource zilizopo ni jambo la pili! Unafiki umewajaa viongozi wa nchi hii na as we see now our President is an imperialist love child ukijumlisha hii land grabbing inayoendelea hapa nyuma ya kina Pinda, Idd Simba & Co, usitegemee maendeleo ya aina yeyote!

Emerging leaders ndio hawa tena kina Le Mutuz what the hell do you expect?? Si vema kumlaumu Mwalimu Nyerere at least wakati wa uhai wake viwanda vilikuwepo na vilifanya kazi, na kimsingi kushindwa kwetu ni kwa kujitakia tu kwa kuwa hatma ya maisha yetu iko mikononi mwetu sisi wenyewe na ifahamike wazi tu kuwa dead people tell no tales!

Mnapoona katika Bunge la Kenya mijadala inakuwa mikali mpaka watu wanarushiana makonde mnafikiri ni kwa sababu gani?? Bunge letu limebaki kuwa rubber stamp ni kuletewa ma miswada na kuyapitasha bila utata wowote! Hata mitazamo ya baadhi ya wana JF kwa viongozi ni ya kustaajabisha!

Tukomae kwanza katika siasa kuwe na usawa kiasi kwamba watu wanaokuwa madarakani anzia katika halmashauri mpaka taifa wawe wanatimiza wajibu wao kikamilifu na si kuishi kwa kuamini kwamba nikiteuliwa tu kuwa mgombea wa ccm basi nashinda nafasi ya uongozi! Lazima zijengwe taasisi zenye nguvu kisiasa ambazo zitaweza kuwa washindani katika kuja na sera nzuri na zinazotekelezeka kuwaletea watu maendeleo, tukiendeleza ngonjera za chama kushika hatamu tumekwisha!
 
Tulishindwa kuweka misingi imara katika kila nyanja baada ya kupata Uhuru, kwa miaka 24 tumetawaliwa kidikteta nakila alichosema Rais tulilifata "blindly", maamuzi mengi yaliyofanywa wakati huo ndio yamekuwa chachu ya maporomoko ya kila kitu Tanzania.
 
Nimefanya kazi na Wakenya karibu miaka 10, ni wachapa kazi sana, na wanasimamia kazi (ambao ninyi mnaita Unyapara!). Moja ya maeneo wanayotuzidi ni upande wa utoaji huduma hasa hoteli. Ati waiter wa Kitanzania anamwendea mteja hotelini, tena akiwa amechoka utadhani katwishwa gunia la misumari, ataanza kwa swali la kijinga, bila hata salamu "Umeshasikilizwa? Kama kwamba lilikutumia mtu wa kukusikiliza! Meneja wa Hoteli Mtanzania ni meneja kweli. Aguse sahani ama kijiko? Huku Meneja wa Hoteli Mkenya ni vigumu kumtofautisha na wafanyakazi wengine, anachapa kazi kama waiter mpaka hoteli inachangamka. Li meneja la Kitanzania linakaa ofisini kucheza na simu, tutafika kweli? Sasa kiama chenu chaja. Hoteli karibu zote ukanda wa Kaskazini na Zanzibar mameneja na walio mapokezi sasa ni Wakenya. Sawa kabisa, mnalalamika nini kwa uzembe na kiburi chenu hiki utadhani mlichanjiwa!
 
Kiganyi,

Kwani wansiasa wamekukataza kufanya kazi kwa bidii ujipatie maendeleo yako binafsi?
 
Nimeishi na kufanya kazi kenya kwa muda mrefu kidogo but notion ya kuwa wako smart zaidi kutuzidi wambongo napingana nayo but ile SPIRIT OF DARING ndio inayo-set difference baina yetu.Mkenya hata ambaye hajaenda shule anaua kuthubutu kufanya mambo kwa maendeleo yake pasipo kusingizia kiwango cha elimu alicho nacho.Pia they are very proud na vitu vyao na nchi yao hawakwepi kodi ovyo.Nilifika maeneo ya mashambani hivi karibuni na kukutana na Wakenya ambao hata hawajawahi kufika Nairobi ila wakawa wananinsimulia Super Highway ilivyo na inavyorahisisha maisha kwao.Mpaka huu utawala wa kibwege uondoke ndipo watuwatabadilika mindset zao na kuanza kufikiri kwa kutumia akili zao.
 
wabongo hatujui kuchapa kazi kama wao..kila siku ya wiki asubuhi ukipita kwenye mabaa au pub utakuta magari yamejazana we jiulize hao watu pub asubuhi yote kwanini wasiwe makazini au kufanya shughuli za kuleta maendeleo...hii ndio bongo yetu...
 
Mi nimefanya kazi sana na wakenya hata wao wengi tu wavivu. Uvivu ni tabia ya mtu binafsi. WAkenya wengi ni vilaza ukija kwenye Technical point of view. Ila watanzania hawana tabia ya kujisifu.
Ujisifu na nini wakati huna cha kujisifia? I like the aggressiveness of the Kenyans!
 
Tofauti ni moja tu nayo ni watanzania wanaongozwa na kuwakilishwa na wajinga na wapuuzi wengi katika maamuzi ya msingi kwenye ngazi mbali mbali kuanzia shina hadi taifa wakati wakenya watu wa namna hiyo hawapewi nafasi!
Ujinga ninaoutaja hapa ni ule wa kutoweza kutumia mazingira, maliasili na rasilimali zingine zilizopo ikiwa ni pamoja na watu wasomi na wasiosoma kujiletea maendeleo.
Hatuhitaji elimu kubwa sana ya darasani ili kutumia vitu hivi kujiletea maendeleo. Inahitajika mindset tu kwa wote na hasa kwa viongozi. Tunaweza kufanya makosa makubwa tukianza kutukuza vyeti katika kuchagua viongozi kwani kuna wapuuzi wengi wenye Phd!
Nimefanya kazi na Wakenya na nimetembea kwao, wapo wanaojituma na wapuuzi pia wapo kama ilivyo kwa tz.
Na haya mawazo potofu ya kuwaona watanzania wako nyuma sana yaachwe mara moja, kuna tofauti kidogo tu ya kurekebisha na ipo kwenye siasa zaidi kwa kuwa siasa za Tanzania haziangalii faida za kijamii kwa ujumla.
Hata mzee ambaye hakuwahi kusoma darasani anajua hasara za maamuzi ya kipuuzi katika mambo ya msingi kabisa yanayofanywa na wachache wenye madaraka katika dola!
 
Ukikutana nao nje ya nchi wana confidence za kufa mtu. wakiwa kwao hawataki longo longo na kama hawaelewani watapigana mikwaju kisha wanadeliver

Tazama KTN au KBC picha ziko clear, news zimetulia, watangazaji wametulia

Soma gazeti la NATION au Standard...huwezi fananisha na lile gazeti la Michuzi (daily nyuz) au lile la copy and paste (guardian)

sisi tuna watu wengi zaidi, rasili mali nyingi zaidi, wanasiasa wengi zaidi, vyama vya siasa vingi zaidi, magazeti mengi zaidi, JF ndio zaidi, cabinet yetu kubwa kuliko ya kwao, katiba yao (na mahakama ya kadhi ndani) ndio walipitisha, sasa kwa nini hawa wana deliver na sisi hatuna kitu?

I've tried to hate them lakini nimeshindwa, cant hate their ambition esp based on their national interest.

Halafu wao kujenga li Superhighway kama hili ili iweje?

ahh sisi hata kuthubutu tunashindwa sijui kwa nini

7293527580_6750ff3295_b.jpg

Tatizo la Watanzania walio wengi ni wanafiki na mara zote wanachukua visingizio vilivyopitwa na wakati kuharalisha udhaifu wao. Kuanzia kwa Rais mstaafu Mwinyi yeye aliingia madarakani kwa kupora nafasi ya Salim Ahmed Salim akafikiri nchi ni kuongoza kama familia. Alikuta viwanda-basic industries vilivyokuwa vimejengwa na Mwalimu ili vizalishe bidhaa ya kutumika katika viwanda vingine. Akakuta viwanda vya nguo ambavyo kwavyom nchi nyingi ziliendelea. Sasa badala ya kuviboresha kwa nguvu zote na kuvilinda akafungua pandora box ya ajabu. Vidhaa hafifu ikashamiri soko letu kuanzia vijiti vy a kuchokonolea meno, nguo za mitumba, viatu vya kuendea kwenye sherehe uku unatembea unakilinda kiatu badala ya kukulinda wewe maana ukitembea kwa kishindo sole unaiacha hapohapo. Viwanda vyetu vya nguo ndio uliokuwa mwisho wake pamoja na viwanda vingine. Lakini kibaya zaidi ni kutokulipa kodi maana uchumi wetu unategemea sana mapato ya kodi. Serikali ya awamu ya pili ilikubali masharti toka mashirika ya fedha ya kimataifa moja ikiwa nikuacha kuwekeza kwenye elimu. Tulichovuna ni kushindwa kuwa na sustainable sucession system ya wataalamu. Vyuo vilivyokuwa vinawapika wataalamu kama Chuo cha TANESCO Morogoro, Bandari DSM, Posta na Simu Dar es Salaam, Chuo cha Maji na vingine vingi vikabaki maghofu ya kujifichia ngochiro, paka na nyoka.

Na alipoona hiyo haitoshi akaliua Azmio la Arusha na kuasisi Azmio la Zanzibar ambalo mpaka leo halikuwahi kuandikwa na yeye pamoja na viongozi waliofatia wanaona aibu kulitaja. Acha hayo yote wakati anaacha madaraka alituachia zigo la rada ya ndege ambapo kiasi cha pesa kilichalipwa, IPTL na madeni kibao ya nje na ndani, rushwa iliyokithiri, ubadhirifu wa mali ya umma, utoroshaji wa wanyama hai kwennye mbuga zetu na watu wasije wakasahau kuwa skendal ya twiga hai ya juzi ni jambo jipya na fragile social fabric ya mihadhara ya kashfa ya dini. Sijui wachambuzi watatausaidia legacy ya mzee Mwinyi ni dini katika nchi yetu.

Kingine alituachia kitu kibaya nacho ni intellectual dependence pale ambapo tunajiona hatuwezi kufanya chochote bila kuambiwa na wazungu. Tuna raslimali za kutosha lakini tunatembeza bakuri la ombaomba hata vitu vidogovidogo. Wenzetu wa Kenya wanajitegemea na raslimali za nchi zinatika koboresha uchumi. Uchumi wao unaadaliwa na Wakenya kakini sisi bajeti mpaka tuambiwe na watu wa nje kwa masharti ili wapate kuifinance. Kila jambo lina mwanzo na haya chanzo chake ni ruksa.

Marais waliomfatia wamerithi viatu vya ruksa. Rais Mkapa alijaribu kusahihisha ya makosa ya kushindwa kukusanya kodi. Akaunda mamlaka ya mapato japo ilikuwa ni maelekzo ya nchi wahisani lakini naye ameendeleza kaugnjwa ka riksa kwa kuwasujudu wageni kwa kigezo cha Foreign Direct Investment ambapo wawekezaji wa kigeni walikja wakachukua mashirika na mabenki kama njugu na wakasamehewa kodi zote. Na tax leave ikiisha wanabadilisha majina kwa kujifanya kampuni imenunuliwa na watu wengine ili waendelee kuenjoy tax holiday. Makampuni ya ya madini yanachukua madini yetu yalivyo bila auditing yoyote na kupelekwa nje tunabaki uambulia asilimia ya mrahaba. Ni aibu sana maana na hii inatoka na kile walichotangza kama faida ambapo hatuna uwezo kuaganlia vitabu vyao vya kihasibu kila siku. Tunaambulia kiduchu, tunaachiwa maandaki, uharibifu wa udongo, hewa, vyanzo vya maji mfano mto Tigeti. Ingawa Mkapa siye wa kwanza kuuza migodi ilianza na Mzee Mwinyi na MheshiwaKikwete akiwa waziri wa madini bado alikuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko lakini wapi.

Sasa mchezo wa kupokezana vijiti ukamkuta Rais Kikwete. Na yeye ameendeleza kile ambacho wenziwe walikiasisi-intellectual dependence. Hatuamini katika uwekezaji wa ndani bali wa kutoka nje na kusamehe kodi kwa wawekezaji hao. Kiasi kikubwa cha pesa kinaamishwa na wawekezaji hao kupitia faida, likizo, wataalamu toka nje na mengine. Lakini chini ya serikali hii safari za nje zimekuwa ni nyingi kwa kisingizio kuwa asiposafiri tutakula mchicha. Lakini hiyo mboga nzuri zaidi ya mchicha tumeshuhudia mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na huduma muhimu maana kwenye safari hizo tunaamisha fedha ya kigeni kupeleka huko nje.

Nchi zote duniani zimeendelea kwa kutumia elimu bora.Zimewekeza ktk elimu ya sayansi na ufundi. Chini ya serikali hii tumefanya vioja kwa kuanzisha sekondari kama uyoga za kata lakini tukazinyima walimu, vitabu, mahabara na maktaba. Wengine wanasema ni bomu la kulipuka, voda fasta, yebeyeba na majina kejeli mengi. Watawala wanazisifia lakini watoto wao nandugu zao wako ktk shule bora za ndani na nje ya nchi. Lakini wakineda kwa wafadhili wanawapa takwimu na wakipokea nishani wanakuja wanashangilia. Shule ambazo wanafunzi wanafika form IV hawajui kusoma na kuandika. Hawa ndio tunategemea waende vyuo vikuu tulivyovianzisha kwa fujo. Hivi ktk fragility hii utajenga flyovers? Kwa wizi na ubadhirifu unaofichuliwa kila uchao toka Buzwagi, Richmond, Meremeta,Loliondo, Utoroshaji wa twiga, kusamehe kodi, kuwepa kodi, kuua reli ya kati na Tazara na kuwapa waharabu tenda za kusafirisha bidhaa hata za umma utajenga uchumi imara wa kuwafaidi wananchi kama Kenya. Historia itasema
 
Wakenya hawa ni wenzetu tu hatutofautiani nao sana!

In 10 years to come uchumi wetu utawazi wa Kenya!

Tatitizo waTz ni Uswahili na Naneno mengi!

Tukipunguza meneno mengi... basi ni Take Off!!!
 
Wadau hebu tujaribu kuwa chachu ya mabadiliko kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja,familia na kuendelea sawa inawezekana viongozi wetu wakawa wanachangia kwa namna moja au nyingine kufanya mambo yaonekane hvyo yalivyo lakini sisi binafsi lazma tuwe ''agents'' wa mabadiliko hvyo kulalamika tu hakuwezi kutusaidia chochote ingawa sio mbaya kufanya hvyo mm ningeshauri kwakila mtu kwa nafasi yake afanye anavyotakiwa kufanya tutalalamika sana hapa kwenye vibao bofye(keyboards) vyetu hakuna kitakachobadilika.Ushauri ni kwamba hebu tufanye kitu kwajili ya nchi yetu hayo mengine ya viongozi wetu tuyaongee tukiwa tunafanya tunachokiongea.
 
Wanajamvi!
Tuseme ukweli Wakenya wametuzidi kwa mengi. Wanajituma kwenye kazi, zaidi si spenders kama sisi(kuanzia serikali mpaka mtu binafsi mfano kwao waziri anapanda PASSAT(saloon car),unaweza kukuta MKENYA tajiri mwenye majumba kila kona na makampuni kadhaa anatembelea TOYOTA PROBOX. tembea kenya hususani miji mikubwa (Nairobi, Kisumu, Mombasa) uhesabu investments kubwa kubwa REAL ESTATES,APARTMENTS,MAJENGO MAKUBWA,SUPERMARKETS,KAMPUNI KUBWA za Insurance, Constructions, Media Houses (TV stations, Publishing), Airlines, kampuni za Mabasi yanayosafiri ndani na nchi jirani kwa aslimia kubwa yanamilikiwa na WAKENYA WENYEWE na wameajiri wakenya wenzao(suala la kabila gani ndo wanaajiriwa usiniulize leo, mimi naanagalia wakenya ndo walioajiriwa). Sasa njoo Tanzania SERIKALINI matumizi ni makubwa kupitiliza MAGARI ya kifahari, watanzania wa kawaida ni SPENDERS mtu anatembelea TOYOTA LAND CRUISER V8 lakini hana investment ya maana. Zaidi watanzania ni wavivu kupitiliza, nenda hoteli hapa Tanzania ukimka asubuhi ya saa 12 ukiuliza chai unaambiwa bado. nenda kalale hoteli za kenya saa 12 kasoro chai tayari so unakunywa chai then kama unasafiri muda huo unaendelea na safari zako.

KUBWA KUPITA YOTE, KENYA WANATHAMINI ELIMU KULIKO VITU VYOTE (nikisema elimu simaanishi elimu ya vyuo vikuu tu) kuanzia shule ya msingi, sekondari na kuendelea) kwao mpaka mtu wa Saloon anasomea na ukienda saloon utaona tofauti na saloon za kibongo). LUGHA YA KIINGEREZA nayo imetufanya tujione wanyonge sana mbele yao. Wakenya ni wepesi kutafuta opportunities Hapa USA wakenya wamejaa, ukienda Uk ndo usiseme, Saudi arabia, South Sudan, TZ, Uganda, South africa ndo balaa na wakipata hela zao wanaenda ku-invest kenya. ndio maana MAKABURU (SOUTH AFRICA) wanashindwa/wanapata wakati mgumu kuinvest kenya maana competition kenya tofauti na TZ hakuna competition na waTZ hawathamini bidhaa za kwao(TZ).

MKUU,
Umesummarize andiko la kukupatia PHD......umeongea ukweli kuliko nadharia....makubaliana na wewe 100%
 
Watanzania mabingwa wa pesa za MICHORO, wizi na ujanja-ujanja mwingi. Wanataka wafanye kazi kidogo tena za kutegea, zisizo na kiwango pamoja na wizi humo humo kwa malipo makubwa. Taabu kweli kweli!
 
Wanajamvi!
Tuseme ukweli Wakenya wametuzidi kwa mengi. Wanajituma kwenye kazi, zaidi si spenders kama sisi(kuanzia serikali mpaka mtu binafsi mfano kwao waziri anapanda PASSAT(saloon car),unaweza kukuta MKENYA tajiri mwenye majumba kila kona na makampuni kadhaa anatembelea TOYOTA PROBOX. tembea kenya hususani miji mikubwa (Nairobi, Kisumu, Mombasa) uhesabu investments kubwa kubwa REAL ESTATES,APARTMENTS,MAJENGO MAKUBWA,SUPERMARKETS,KAMPUNI KUBWA za Insurance, Constructions, Media Houses (TV stations, Publishing), Airlines, kampuni za Mabasi yanayosafiri ndani na nchi jirani kwa aslimia kubwa yanamilikiwa na WAKENYA WENYEWE na wameajiri wakenya wenzao(suala la kabila gani ndo wanaajiriwa usiniulize leo, mimi naanagalia wakenya ndo walioajiriwa). Sasa njoo Tanzania SERIKALINI matumizi ni makubwa kupitiliza MAGARI ya kifahari, watanzania wa kawaida ni SPENDERS mtu anatembelea TOYOTA LAND CRUISER V8 lakini hana investment ya maana. Zaidi watanzania ni wavivu kupitiliza, nenda hoteli hapa Tanzania ukimka asubuhi ya saa 12 ukiuliza chai unaambiwa bado. nenda kalale hoteli za kenya saa 12 kasoro chai tayari so unakunywa chai then kama unasafiri muda huo unaendelea na safari zako.

KUBWA KUPITA YOTE, KENYA WANATHAMINI ELIMU KULIKO VITU VYOTE (nikisema elimu simaanishi elimu ya vyuo vikuu tu) kuanzia shule ya msingi, sekondari na kuendelea) kwao mpaka mtu wa Saloon anasomea na ukienda saloon utaona tofauti na saloon za kibongo). LUGHA YA KIINGEREZA nayo imetufanya tujione wanyonge sana mbele yao. Wakenya ni wepesi kutafuta opportunities Hapa USA wakenya wamejaa, ukienda Uk ndo usiseme, Saudi arabia, South Sudan, TZ, Uganda, South africa ndo balaa na wakipata hela zao wanaenda ku-invest kenya. ndio maana MAKABURU (SOUTH AFRICA) wanashindwa/wanapata wakati mgumu kuinvest kenya maana competition kenya tofauti na TZ hakuna competition na waTZ hawathamini bidhaa za kwao(TZ).

Unazo sifa zote za mtanzania! Kuthamini vya wageni na kudharau vya wenyeji. We ni mtumwa hujui tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom