Hivi Wakenya wametushinda nini?

Tatizo tunalo na sisi waTZ, hatuna uzalendo wa nchi yetu. Siku moja niko sehemu pembeni yangu wako wadada 2 wakenya. Mmoja anamsimulia mwenzie eti TZ hakuna shule wala vyuo vizuri,elimu hovyo etc. Nikaingilia maongezi yao. Akastuka akasema yeye anaishi USA haijui TZ ilakaambiwa na rafikize wa TZ. Nikampa ukweli akasema tatizo ni ninyi waTZ hamsemi mazuri ya kwenu. Tubadilike nasi!
 
Wakenya wamefanikiwa kuzima simu feki,sisi wachina ndo wanatuzia hizo simu feki
 
watu wa tz wamezidi kuwa wachawi.....wavivu....wanafiki....na mwisho si wazalendo......ukijumlisha haya yote utampata mtanzania......matatizo yooote ya mtanzania yanajengwa na madhaifu haya aliyonayo....jamii yote ya mtanzania imeathirika na mambo haya...
 
Lakini na wewe muandishi wa huu uzi umepotosha kidogo.Kutoka gazeti la East Africa la wiki hii na iliyopita liripoti kuwa hiyo highway imejengwa kwa msaada wa nchi ya moja ya kiasia ambayo ni china.na miradi mingi ya kijenga miundombinu ya kenya ni misaada ya China na Japan (kupitia JICA).kwani na sisi tunashindwa kutopa hela china?na kwa hiyo hawajajenga highway kutoka mapato ya ndani-kodi.
Our God must be crazy
 
japo inauma,ni vizuri kuukubali ukweli kwamba wenzetu wamepiga hatua kubwa kimaendeleo, hii itatusaidia na sisi kuchukua hatua za makusudi za kuiletea nchi yetu maendeleo. Viongozi wao wanadhamira za kweli kushrikiana na wananchi kutimiza ahadi zao. huku bongo tunao mafisadi wa kutoa ahadi hewa
 
Wekeni utaifa mbele, Acheni kujidharau na kujidhalilisha. Hili ndio linalotuua.

Tatizo lenu watz penye ubovu mnabadilsha kuwa kweli, mfano ufisadi umefikia wapi? mumehalalisha, hivyo lazima mkubali rangi ya mkaa ni nyeusi lakini mnafanya rangi ya mkaa kuwa nyeupe
 
Tatizo tunalo na sisi waTZ, hatuna uzalendo wa nchi yetu. Siku moja niko sehemu pembeni yangu wako wadada 2 wakenya. Mmoja anamsimulia mwenzie eti TZ hakuna shule wala vyuo vizuri,elimu hovyo etc. Nikaingilia maongezi yao. Akastuka akasema yeye anaishi USA haijui TZ ilakaambiwa na rafikize wa TZ. Nikampa ukweli akasema tatizo ni ninyi waTZ hamsemi mazuri ya kwenu. Tubadilike nasi!

hatuna mazuri yoyote, matokeo ya mitihani ni mabaya siku zote, hamtaki kutafuta sababu, mnabadilisha mifumo, wakati siyo solution, migomo ya chinichini aka baridi ni mibaya sana.
 
aliyewaroga alifariki mwaka 1999 na mlimzika kwa mbwembwe!

That's poor defence mechanism ambayo haikupeleki popote. Wewe jiangalie ni wapi unashindwa. How do you use your education on critical and critique basis? Lakini kama ndivyo unavyojenga hoja hivi kama ulivyofanya hapa unakuwa mtumwa wa mzimu ule unaosukumia zigo. Hivi huyo alifariki 1999 ndiye alimwambia waziri wenu mzuri na baba yake Mwinyi wahasisi mrahaba wa 3% kwa mapato ambayo huwezi hata kuyahakiki? Waliwaambia njoo chimba gesi ahalafu mtuuzie sisi wakati wengine 50:50? Alisema uzeni Loliondo,tausi hadi za Ikulu, jimirikishieni Kiwira, fungua shule za kata na utegemee kupata competitive engineers au professionals. Yeye alisema bomoa mfumo wa elimu hasa vyuo amabavyo vilikuwa incubators- Bandari Temeke, Posta na Simu Kijitinyama, Tanesco Morogoro, Benki Iringa na vingine vingi. Alsiema uzeni viwanda vyenu halafu watakaonunua wavifanye viwe maghala ya bidhaa toka nje. Be serious mwanangu and think big. This is a sensitive thread that needs deep thinking. Mmabo magumu na majibu mepesi waachie wengine
 
Mi nimefanya kazi sana na wakenya hata wao wengi tu wavivu. Uvivu ni tabia ya mtu binafsi. WAkenya wengi ni vilaza ukija kwenye Technical point of view. Ila watanzania hawana tabia ya kujisifu.

hatuongelei technical, kwani wakenya wamejisifia nini? nafikiri walikofikia na wanayoendelea kuyafanya yanajisifia yenyewe.
 
Mi nimefanya kazi sana na wakenya hata wao wengi tu wavivu. Uvivu ni tabia ya mtu binafsi. WAkenya wengi ni vilaza ukija kwenye Technical point of view. Ila watanzania hawana tabia ya kujisifu.

Wewe hukufanya kazi na Wakenya bali Watanzania wanaojifanya Wakenya. Wakenya ni wabunifu, hawana cha hivyo kwa mapenzi yakekuzungukazunguka na kusifia kisichokuwepo. Shule wameenda na hawajachakachua elimu kama tulivyofanya hapa kwetu. Usitegemee kupata engineers, doctors, lawyers, accountants, na wataalamu wengine ambao wako confident and knowledgable. Si rahisi ili uwe confident hata mentor wako au mwalimu anatakiwa awe confident lakini kama ni mwalimu wa voda fasta huwezi kuwa na skills na delivery kama yule alifundishwa na mwalimu ambaye amekuwa hivyo kwa mapenzi yake na akaendelezwa na kujienedelza kipaji chake na mwisho akalipwa vizuri. Badilisha mifumo yetu na kuwaenzi wataalamu. Wape nyenzo na kipato kizuri na kuwa na viapaumbele enedelevu lakini sio kuendekeza safari za nje halafu hata kile kidogo kilichopo kinaishia kule mnaona wenzenu wanapaa halafu mnasema wana roho mbaya. Hesabu safari za Kibaki nje ya nchi na za kwenu halafu angalia profit and loss na utasema mwenyewe
 
Jibu la swali lako ni swali lako!,... namaanisha walichokushinda ni wewe kuanza kuwadiscuss wakati wenzako hawana muda wa kupoteza kukudiscuss wewe!,.... hakuna walichokushinda, fanya kazi be proud of who you are and what you have!....
 
watu wa tz wamezidi kuwa wachawi.....wavivu....wanafiki....na mwisho si wazalendo......ukijumlisha haya yote utampata mtanzania......matatizo yooote ya mtanzania yanajengwa na madhaifu haya aliyonayo....jamii yote ya mtanzania imeathirika na mambo haya...

Sema kuwa Tanzania tunaongozwa na uswahili, lakini Kenya uswahili uko Mombasa peke yake. Angalia wakuu wetu wa mikoa wakuu wa wilaya au wabunge, uone kama ni watu wanao-qualify. Angalia serikali yetu yote ilivyo uone kama kweli inajaribu kufanana japo na Rwanda, sio kenya, Rwanda tu. Uswahili, uswahili, uswahili...that is the cancer of Tanzania.
 
Tatizo tunalo na sisi waTZ, hatuna uzalendo wa nchi yetu. Siku moja niko sehemu pembeni yangu wako wadada 2 wakenya. Mmoja anamsimulia mwenzie eti TZ hakuna shule wala vyuo vizuri,elimu hovyo etc. Nikaingilia maongezi yao. Akastuka akasema yeye anaishi USA haijui TZ ilakaambiwa na rafikize wa TZ. Nikampa ukweli akasema tatizo ni ninyi waTZ hamsemi mazuri ya kwenu. Tubadilike nasi!

What did you tell them so as to bellitle them? Which University in Tanzania can you now put forward as a benchmark from which others to learn? Na kama unasema tunacho chuo cha aina hiyo wahitimu wamefanya nini? Tunajenga barabara hazina viwango kama ile ya Kilwa. Haingii akilini kuwa wakati inajengwa civil engineers wetu hawakuwepo na hasa wanaotoka wizarani na TANROADS. WHY did not no raise the alarm. Wakati sasa hivi nchi yetu inaongoza kwa kuwa na mikataba mibovu ya madini na wizi unaotokea kwenye mbuga zetu wasomi wa sheria si wapo? Hivi elimu ni vyetu vizuri kabatini au ni jinsi unavyoitumia? Kitila Mkumbo anasema elimu hata unaweza kuipata chini ya mti as long as ina ubora. Hatuna cha kujisifia sisi wenzetu wametuacha na sisi tunahitaji kubadilika
 
Mkuu kenya wanatumia ENGLISH kama lugha ya taifa, unajua kiswahili kimeturudisha nyuma sana

Wahindi wanatumia kihindi.
Wakorea wanatumia kikorea.
Wajapani wanatumia kijapani.
Je hao ni masikini kama sisi? Lugha ya taifa si sababu ya sisi kuwa masikini. Tafuta sababu nyingne.
 
wametuzidi kila kitu,halafu walim wao waligoma wameongezewa mshahara ndo wamerudi kazini
 
Don Draper,
Wakenya hawajatushinda chochote, labda wametushinda kwa kuwatelekeza masikini wao (Wakenya) vibaya sana kiasi ukienda uswahilini kwa Wakenya utashangaa umasikini ulivyikithiri na tusibabaishwe na kibarabara hicho cha Athi Road ''super highway' chenye viji- by-pass na urefu wa hiyo highway haizidi kilometa 40.

Tizama jinsi masikini wanavyopigika Kenya:

31418.jpg

a fire broke out in Deep Sea settlement, Nairobi, destroying 80-90% of their housing structures. According to the Kenya Red Cross, up to 10,000 people may have been affected by the fire – a majority of who have been made homeless, and dozens reportedly injured.

MDG--Kenya---Deep-Sea-Slu-008.jpg

The population of Deep Sea has doubled over the past 15 years, he says, estimating its size at 15,000. Slum surveys giving 'invisible' inhabitants a say in urban planning | Global development | guardian.co.uk

in-Nairobi-Kenya-005.jpg

Every day up to 10,000 people sift through the rubbish at Dandora, one of Africa's largest dumps, 8km from the centre of Nairobi. The city's only dump site is the subject of Trash and Tragedy, a report from Concern Worldwide and other agencies highlighting the health hazards it poses to local people Surviving off rubbish in Kenya's slums

Men and women pick through a rubbish truck, looking for anything they can sell on or take home to use. Campaigners have long pressed for the site to be relocated away from the slums. A report says the site represents ‘one of the most flagrant violations of human rights' in the country, affecting more than 200,000 people
in-Nairobi-Kenya-009.jpg
in-Nairobi-Kenya-011.jpg
 
Ukikutana nao nje ya nchi wana confidence za kufa mtu. wakiwa kwao hawataki longo longo na kama hawaelewani watapigana mikwaju kisha wanadeliver

Tazama KTN au KBC picha ziko clear, news zimetulia, watangazaji wametulia

Soma gazeti la NATION au Standard...huwezi fananisha na lile gazeti la Michuzi (daily nyuz) au lile la copy and paste (guardian)

sisi tuna watu wengi zaidi, rasili mali nyingi zaidi, wanasiasa wengi zaidi, vyama vya siasa vingi zaidi, magazeti mengi zaidi, JF ndio zaidi, cabinet yetu kubwa kuliko ya kwao, katiba yao (na mahakama ya kadhi ndani) ndio walipitisha, sasa kwa nini hawa wana deliver na sisi hatuna kitu?

I've tried to hate them lakini nimeshindwa, cant hate their ambition esp based on their national interest.

Halafu wao kujenga li Superhighway kama hili ili iweje?

ahh sisi hata kuthubutu tunashindwa sijui kwa nini
ooh my nanihii...proudly to be kenyan......tusiende mbaali sana ukianzia hapo aisee mnaweza kulia ukiangalia wale wamama wa itv na yule bibi wa tbc wanavyotangaza habari aiseee...kichefu chefu....uje kwa vibinti vibichiiiii vya citizen vina ipad mkononi vyatamba tu kwenye bonge la mjiscreen mkubwaa huku vimebana vijihips vyao...aisee arifu nakuambia ile news at 9 huwa sikosi citizen.....

mambo mengi tu tz hovyo hovyoooo.......unakutana usiku wa manane na jizee zima kama kitilya lasaka machangudoa limelewa chakariiii hapo unategemea nini TRA......

sasa majizee kama wasira si mzigo kwa watz tu.....lafanya nini lijimtu kama lile...hivi lina faida gani aisee??? haya jimtu kama nape lina akili kweli.....haya jana nimemuona jizee msekwa aiseee kwenye general on monday..ana akili kweli yule?.....haya jizee kama pm kayanza....hivi pm kayanza anaweza ku debate na kijana wa darasa la 8 wa kikenya?? si atakkuwa alamba lamba vidole...na kufuta futa mawani......

haya angalia majizee yalioko kwenye maofisi hovyo sana....kizazi cha b4 uhuru sijui vipi.....unakutana na mzee makini kidogo kama gen ulimwengu....haya angalia mavijana mazimaaa eti yana degree ukikutana nayo usikie wanayoongea masaa yote....ubishi wa arsenal na man city....phuuuh......yaani likijana jizima la discuss soka asubuhi mpaka jioni...likitoka hapo laenda bar beer na kitimoto.....kisha utayakuta mavijana tena ma graduate hao wa udsm hao wana first class zao na walipata one za 3 na one za 7 hao.....wanajisifia eti jana wamechapa mademu.....si upuuzi huo.....mtashindana vipi na wenzenu wanaowaza ni lini watapiga hatua kimaendeleo.....

haya ona jimama kama sophia simba...hivi kweli wewe imagin unakutana na bi sofi...imagine wee imagine tu vuuuu vaaap umekutana nae kwenye korido za wizara..unafikiria ukimsalimia atakuambia nn??? ushakutana na jimama hili banki wewe? linavyojishaua ujue kwamba yeye waziri......

haya sasa kutana na ati mwanadiplomasia mkuu wa nchi benadi....huyu hatakuwa na mpya atakuwa ana maadui hawampendi...ukimuuliza vipi yahee wizara yao mbona undugu mwingi ubalozini...atakuambia wivu wa maadui zake......

utashindana vipi na wakenya wewe???

uje kwenye sekta za hovyo hovyo kama u misss na burudani....sasa kama wizaraa yaandaa mkutano na washereheshaji inawatoa kenya...kuna kitu hapo.....

yaani acheni kabisa....kaeni hivyo hivo......yaani upuuzi uje kwenye eti soka hivi nyieeeee mna akili kweli???
ntaandika mpaka kesho......
 
Lakini na wewe muandishi wa huu uzi umepotosha kidogo.Kutoka gazeti la East Africa la wiki hii na iliyopita liripoti kuwa hiyo highway imejengwa kwa msaada wa nchi ya moja ya kiasia ambayo ni china.na miradi mingi ya kijenga miundombinu ya kenya ni misaada ya China na Japan (kupitia JICA).kwani na sisi tunashindwa kutopa hela china?na kwa hiyo hawajajenga highway kutoka mapato ya ndani-kodi.​

** huyo jamaa hapo juu kweli ni chizi, kwani cc watz tunapewa misaada mingapi na hata robo ya hiyo misaada tupewayo haitumiki kufanyia kile kilicho lengwa,hebu funguka kichwa wewe.. hongereni watani wetu wa jadi kenya..tz huko kufika ni majaliwa..serikali ilivyo ya kijinga inaishia kuumiza kichwa kujenga dar tu wakati kuna sehemu kibao ambazo hazija songamana kama dar ambapo wanaweza kufanya mambo mazuri na kupunguza hilo ghasia la dar es salaam..kila kukicha dar dar, kwani mwanza sio tz, arusha nako?mbeya? moshi? na kwingineko..tuamkeni watz bila hivyo tumekwisha...
 
Don Draper,
Wakenya hawajatushinda chochote, labda wametushinda kwa kuwatelekeza masikini wao (Wakenya) vibaya sana kiasi ukienda uswahilini kwa Wakenya utashangaa umasikini ulivyikithiri na tusibabaishwe na kibarabara hicho cha Athi Road ''super highway' chenye viji- by-pass na urefu wa hiyo highway haizidi kilometa 40.

Tizama jinsi masikini wanavyopigika Kenya:

31418.jpg

a fire broke out in Deep Sea settlement, Nairobi, destroying 80-90% of their housing structures. According to the Kenya Red Cross, up to 10,000 people may have been affected by the fire – a majority of who have been made homeless, and dozens reportedly injured.

MDG--Kenya---Deep-Sea-Slu-008.jpg

The population of Deep Sea has doubled over the past 15 years, he says, estimating its size at 15,000. Slum surveys giving 'invisible' inhabitants a say in urban planning | Global development | guardian.co.uk

in-Nairobi-Kenya-005.jpg

Every day up to 10,000 people sift through the rubbish at Dandora, one of Africa's largest dumps, 8km from the centre of Nairobi. The city's only dump site is the subject of Trash and Tragedy, a report from Concern Worldwide and other agencies highlighting the health hazards it poses to local people Surviving off rubbish in Kenya's slums

Men and women pick through a rubbish truck, looking for anything they can sell on or take home to use. Campaigners have long pressed for the site to be relocated away from the slums. A report says the site represents ‘one of the most flagrant violations of human rights' in the country, affecting more than 200,000 people
in-Nairobi-Kenya-009.jpg
in-Nairobi-Kenya-011.jpg

wewe ndungu yangu uliyetuma hizi picha,kwani kwetu tz hakuna watu hawa?nenda madampo makubwa utawaona,mfano kule mtoni kwa azizi ally kuna dampo kubwa kacheki.. panapokuwa na maendeleo ndugu uache ujinga fikiri ndugu, na penda maendeleo..acha kuweka vitu ambavyo hata kwetu tz vipo na sio tz tu dunia nzima wapo hao watu waokotaji..eti 40km haya sisi watz tujenge tu flai ova pale ubungo ambayo haitachua hata km 2,kuanzia kwenye base yake chezea km40 wewe..hongereni watani wa jadi a.k.a harambee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom