Hivi wafanyakazi wa TRA mna matatizo gani? Mnaomba omba hela za rushwa kila huduma kwa mteja!

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,953
7,476
Juzi juzi mwisho wa mwaka nilienda TRA kuulizia nadaiwa kodi kiasi gani mfanyakazi anaomba elfu 15 ili aniangalizie! Nikamuuliza ya nini? Akajibu siunajua bro ya maji kidogo!

Nimenda tena jana kufanya bond cancellation ili wafanye bond cancellation wanataka hela yaani ni tabu tupu! Nimebana kuwapa hela kazi hawafanyi! Sasa najiuliza kwa mwenendo huu wa TRA wafanyakazi kupenda kupewa fedha ili wafanye kazi za wateja wao inaleta picha mbaya sana!

Hawa wafanyakazi wa TRA wanamisharhara wanalipwa kutokana na kodi zetu! Huu upuuzi wa kutaka kitu kidogo ndo utoe huduma serkali uiufanyie kazi!

Wananawapotezea mda wananchi na wawekezaji kama mwananchi au mwekezaji hatajiongea kutoa rusha au kitu ndo mambo yake yafanyiwe kaiz atabaki pale hata wiki wakati ni jambo la saa moja linaisha!

TRA ndo kibubu cha taifa ila kunapokuwa na hawa vijana wanaotaka maisha makubwa ya shortcut ndo inapelekea huduma kugeuka kuwa nongwa na kudumaza makusanyo yetu hali inayopelekea huduma mbovu katika sekta zingine!
Asanteh!
 
Njaa kali sana na wanataka ku-maintain status quo kuwa kila mfanyakazi anayefanya kazi TRA yuko financially stable, yaaani wafanyakazi wa TRA hawana tofauti na members wa JF kila mtu mambo safi
 
Njaa kali sana na wanataka ku-maintain statsus quo kuwa kila mfanyakazi anayefanya kazi TRA yuko financially stable, yaaani wafanyakazi wa TRA hawana tofauti na members wa JF kila mtu mambo safi
Kaka hawa watu hata sijui wanamatatizo gani rushwa rushwa na ubabaishaji! Wanapiga stories mda mrefu pia ukikuta anongea na simu utasubiri mpaka uchoke customer care ndogo sana! Tunafanya mambo kwa mazoea sana!
 
Hivi TRA wana mishahara mikubwa au wanapata kwenye hayo mazingira ya kitu kidogo
 
Sio TRA tu kila sekita neenda mahakamani utajionea madudu, neenda passport office, magu aliaharibu hi nchi sanaa watu hawakua na uzalendo isipokua wanamhofu yeye tu.
Inaweza kuwa kweli ila tujifunze kufanya kazi kwa juhudi na maarifa! Mi naamini ukifanya kazi hata Mungu anakubariki sana! Mda mwingine issue sio kuwa na hela ila hela uliyoifanyia kazi inadumu sana na unafanya vitu vya maana!
 
Inaweza kuwa kweli ila tujifunze kufanya kazi kwa juhudi na maarifa! Mi naamini ukifanya kazi hata Mungu anakubariki sana! Mda mwingine issue sio kuwa na hela ila hela uliyoifanyia kazi inadumu sana na unafanya vitu vya maana!
Ndo maana ma traffic police wengi hawana maendeleo wakati wanasimama tu barabarani wanaanza kupokea rushwa asbhi hadi jioni. Ila tembelea wanoko ishi huzo pesa hazina baraka za Mungu
 
Kaka hawa watu hata sijui wanamatatizo gani rushwa rushwa na ubabaishaji! Wanapiga stories mda mrefu pia ukikuta anongea na simu utasubiri mpaka uchoke customer care ndogo sana! Tunafanya mambo kwa mazoea sana!
Sasa uende TRA ukahudumiwe na Binggi mjamzito mwenye mimba changa, haalfu siku hio network imekaa kushoto.....utajuta mbona? au ukute wale watoto wanaokwenda field, kamepewa kugawa form pale au pale customer care au pale kitendo cha kuprint TIN hahahaaha eti TIN anataka umpe 10,000
 
Wanashindana kujenga majumba yA thamani na kufungua miradi uchwara isiyoendana na vipato vyao.
Hahaha ukiwakuta wanavimba na iphone macho matatu maboya sana hawa! Lakini hawana finemcial growth ya uhakika! Mimi huwa naawaambia ibeni sana saizi ila meza ikipinduka vyote vinaisha maana sio vyoko! Uliwaomba watu uwatunzie!
 
Juzi juzi mwisho wa mwaka nilienda TRA kuulizia nadaiwa kodi kiasi gani mfanyakazi anaomba elfu 15 ili aniangalizie! Nikamuuliza ya nini? Akajibu siunajua bro ya maji kidogo...
Si nasikia huko wanalipwa mishahara minono sasa hizo elfu 15 si kujidhalilisha? Pesa wanaweka wapi?
 
Njaa kali sana na wanataka ku-maintain status quo kuwa kila mfanyakazi anayefanya kazi TRA yuko financially stable, yaaani wafanyakazi wa TRA hawana tofauti na members wa JF kila mtu mambo safi
Mi mambo yangu wala sio safi brother
 
Nchi hii imejengwa kwa rushwa kuanzia ngazi ya mjumbe, taasisi hadi serikali kuu.

Mkuu wacha wachukue tuu pesa kidogo, maana wao hawana nafasi kwenye dili ndogo ndogo
Sawa Tajiri kichwa ila ngoja ukutane nao una issue sensitive utaona hawafai sana hawa watu!
 
Back
Top Bottom