Mheshimiwa Rais; Hivi kati ya wabunge wote wa sasa aliyesoma uchumi ni Mwigulu peke yake?

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,498
37,792
Heshima kwako Mama.
Kilio na malalamiko ya Wananchi kuhusu tozo Leo vimemuibua Waziri wako wa fedha na uchumi Mwigulu Lameck Nchemba. Ametoa ufafanuzi akisingizia Wananchi ndio waliomwambia akaweke tozo Benki hata kwenye hela ambazo zimeshakatwa Kodi kama PAYE. Anasema ni Wananchi ndio waliomshauri aweke tozo kwenye hela ya mkopo àmbao kikundi cha kina mama kinakopeshwa na SACCOS inayolipa Kodi. Yaani Wananchi (nadhani wa jimboni kwake) ndio waliomwambia wapangaji Wana nguvu na mamlaka kwenye nyumba za kupanga Kwa hiyo kabla hawajamlipa mwenye nyumba 60,000 wachukue elfu 6 wapeleke TRA na kama ni mbali wachukue na elfu 3 ya Bodaboda kwenda na kurudi halafu mwenye nyumba akipita wampa 51,000 yake.

Hii si mara ya kwanza Waziri huyu kuleta tozo zinazoumiza Wananchi masikini na wanapolalamika anasingizia wao ndo wamependekeza Ila atakaa arekebishe Kwa vile eti ni msikivu.
Hivi ni msomi gani huyu ambaye Kila wakati anaanzisha vitu ambavyo Hadi wanafunzi wa darasa la 7B wanamkosoa na yeye anakiri kwenda kubadilisha?
Mwaka Jana tozo za simu zilifikia Hadi 10000 na kelele zilipozidi zikarudi Hadi 7000 na kisha 4000 na Leo amekiri Hilo. Waliopiga kelele zaidi ni wafanyabishara wa vibanda vya M_pesa na Wafanyakazi wao àmbao wengi ni darasa la 7 àmbao walisema kuna upungufu mkubwa wa miamala maana watu wameacha kutumia huduma ya kutuma fedha Kwa simu na hivyo hata fedha iliyokusudiwa haiwezi kipatikana. Yaani Kwa maana nyingine hata Kodi ya serikali + tozo ikawa chini ya Kodi iliyokuwa inakusanywa awali.

Labda niulize tena, siku hizi wasomi wa uchumi hawahusishi hesabu kwenye masomo Yao? Yaani Mtu anaweza kufikia ngazi ya Daktari wa uchumi bila kugusa Arithmetics? Zamani kulikuwa na somo linaitwa Business arithmetics, siku hizi mitaala mipya imelitupilia mbali?

Turudi kwenye hoja yangu;
Mheshimiwa Rais, pale Bungeni mwenye kujua uchumi Hadi wizarani kote ni Mwigulu Peke yake kiasi kwamba akiondoka Kila kitu kitasimama? Kama ni hivyo naomba angalia Kama Katiba inakuruhusu teua Mbunge mwingine (Ila asiwe Mwalimu wa Mwigulu) akusaidie kuendesha hiyo wizara kurudisha Imani ya Wananchi. Vinginevyo huyu anakwenda kukupa kazi ngumu 2025 uingie dhambi ya wizi na dhuluma ya Kura kama 2020.

Lingine ni suala la tuhuma.
Juzi ukiwa CCP Moshi umeongea vizuri Sana kuhusu Ile video ya Askari traffic wa Njombe ambapo kijana raia alikuwa anapokea kitu toka Kwa madereva na traffic wako pembeni wanaangalia. Mimi na wewe na Watanzania wote walioona video Ile ni mashahidi. Hakuna aliyeona hela ikipokelewa zaidi ya kuonekana kikipokelewa kitu, ni karatasi, ni hela, wanasalimiana hatujui. Lakini busara ya kawaida ikatutuma kusema haiwezekani raia ahatarishe maisha yake Kwa kushikana mikono na dereva gari linatembea halafu Askari wako pembeni wasikemee kitendo hicho kama si wanufaika. Tukakubaliana kwamba Ile ni rushwa katika mazingira yoyote na wanufaika Wakuu ni wale Askari na nasikia walifukuzwa kazi kabla hata hujafika Moshi.
Sasa Kwa Mwigulu mwenye tuhuma kibao yeye ni Nani labda? Anajiona Nani Hadi atuhimiwe kuwa na ukwasi usioelezeka, anatuhumiwa kumiliki kampuni kubwa ya Mabasi (Esther), timu ya Singida Big Stars, zamani tuliambiwa alimiki Singida United na yeye aliwahi kukiri mbele ya Mkutano wa wananyanga kwamba ndiye aliyemsajili mwanao Feisal Salim (nasikia wanamuita Feitoto na siku za karibuni Byuti Byuti) na kisha kumpeleka Yanga anayoshabikia.

Mama najua Kwa Umri wako unaijua vizuri hadithi ya usafi wa mke wa Mfalme kwamba hata tuhuma tu hazipaswi kumwacha salama. Anayetuhumiwa ni Mwekahazina Mkuu wa nchi, na yeye amekiri amezaliwa na kukua na kisha kusoma akiwa masikini. Je, haya anayotuhumiwa nayo kayapata kihalali? Yaani mweka hazina wetu wa Kamati ya harusi analewa Hennessy Kila siku wakati kabla ya hapa alikuwa analewa komoni tena weekend?

Hapana mama, hebu wasikie Watanzania hawa masikini wanaolalamika Kila siku wakiongelea watu wale wale.
Vinginevyo ukicheka na Nyani jiandae kuvuna mabua.
 
Back
Top Bottom