Hivi, uislamu uliwahi kuleta nini?

Hivi, uislamu uliwahi kuleta nini?

Muingiliano wa wenyeji na waarabu ambao walikuwa ni waislam ndio kulizaa lugha ya kiswahili.
Lugha ya kiswahili ilikuwepo,nsoma historia ya lugha kiswahili.

Kulikuwa na Lahaja za Kiunguja,Kipemba, kimombasa, kitumbatu, kipate, ni Lahaja za kiswahili yaan Dialects, Lahaja hizo zilichukua maneno toka kiarabu, lakini pia kihindi, kireno,kiajemi!!

Kiarabu kama kilivyo kireno kilichangia maneno kwenye kiswahili.

Mvinyo-toka Kireno
Leso-toka kireno
Bima-toka Kiajemi
Salaam-toka kiarabu
Shukran -toka kiarabu.

Kwahiyo Kiswahili haikuletwa na waarabu/uislamu, kiswahili ni lugha Moja , na kiarabu ni lugha nyingine,

Havifanani na kiswahili katika mfumo wa sarufi muundo, wala maandishi yaani, silabi, irabu na konsonanti.

Kama una nia ya kuelewa nadhani utaelewa!!!
 
Asante , shikamoo, madrasa, mwalimu,marahaba ,gari,gunia,dunia hayo ni baadhi ya maneno yaliyoletwa na hao wageni kutoka mashariki ya mbali na kati
Na kifanya lugha ya kiswahili kuzid kukua
Baadhi ni kiarabu
Mashariki ni kiarabu
Lugha ni kiarabu
Kiswahili ni neno la kiarabu
Kuzidi ni neno la kiarabu
 
kama ni kweli ulivyosema how come nchi za kiislamu ni the poorest dunia hii? top bottom countries zote yemeni, syria, afghanistan, somalia, irak, sudani, mali, mauritania, chad zote full of muslims, kwa nini unafikiri? hata nchi chache ambazo zina waislamu zinazofanya vizuri zilianzishwa na Western Christians kama uae, qatar au hata malaysia na indonesia, lkn nchi zinazofwata uislamu kama way of life ziko back ward kama irani au pakistani kabla ya islamic revolution chini ya shah ilikuwa (irani) prosperous mpaka ilipopindiliwa na uislamu sasa hivi ni pariah state, kwa nini uislamu umeshindwa kuendeleza huko kwa waislamu kama ulioyaandika yana ukweli wowote? ?
qatar, kuwait, etc zote zinafanya vizuri na zinafuata 100% sheria na utamaduni wa kiislamu na hata wazungu walivyopeleka world cup walitaka kubadilisha utaratibu ila ikashindikana, na ukizungumzia nchi kama iraq na syria au libya are u blind to that extent hadi hujui wala huoni uharibifu unaofanywa na wazungu kwenye nchi hizo
ungemsikiliza prof tibaijuka kwenye unterview yake juzi alielezea vizuri sana wazungu wanavyoharibu nchi nyingi hasa za kiarabu kwa ajilo ya ulafi wao
 
Lugha ya kiswahili ilikuwepo,nsoma historia ya lugha kiswahili.
Mnyonge mnyongeni, lakini mchango wa maneno ya kireno ni kidogo sana mchango wa Lugha ya Kiarabu ni mkubwa.

Neno KISWAHILI pia limetokana na neno la Kiarabu SAHEL au SAHIL.

Hauwezi kuitaja Historia ya Pwani ya Afrika ya mashariki bila kutaja mchango wa Waarabu na Waisilamu.👈 👉fact
 
Uisilamu ulileta Biashara na Trade katika pwani yetu ya Afrika ya Mashariki na ndio sababu ya kuzaliwa kwa lugha ya Kiswahili.
Biashara ya utumwa na pembe za ndovu ni mojawapo ya Biashara za hovyo sana kuwahi kutokea duniani.
 
uislamu upo karibia miaka 1000 pwani yetu na sehemu nyinginezo, hivi kipi haswa kimeletwa na uislamu kwa maana ya civilization na maendeleo ya jamii? hata tu mazao labda kuna zao gani ambalo lililetwa na uiaslamu hapa kwetu ?
Waislamu achaneni na Hawa watoto wa PAPA ili wapate muda mzuri wa kuzibuliwa visamvu

Hawa hawataki kujua ila ni ubishi tu
 
Katika mambo yote, ni huu UTAMADUNI walio tuletea ambao sasa tunaona matokeo yake toka kwa viongozi wetu kama tuliye naye sasa.
Huu utamaduni wa kulaghai laghai watu; kutumia lugha laini huku mambo mazito yanayoigharimu nchi yakifanyika kisiri siri. Tabia ya kutokuwa wazi juu ya jambo analonuia kulifanya kiongozi au mtu na UNAFIKI mwingi.
Haya mambo ya UCHAWA sasa hivi ni sehemu ya tamaduni hizi tulizo letewa na watu wa nje kupitia kwenye dini zao.
Sasa huo ni uislamu au ni tabia ya mtu?
 
kabla ya uvamizi wa wareno na husda zao kuanzia Somalia mpaka sofala ilikuwa chini ya dola ya kiislamu na uchumi ulikuwa vizuri sana, tuseme hata magofu ya kilwa hauyaoni? yale maghorofa yalijengwa na wamasai?.
Biashara ya utumwa pia ilishamiri sana.
 
Biashara ya utumwa na pembe za ndovu ni mojawapo ya Biashara za hovyo sana kuwahi kutokea duniani.
Biashara ya Utumwa ilikuwa ya hovyo sana kufanywa na Waislamu na Waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki lakini Biashara ya pembe za ndovu mimi nafikiri Tembo walikuwa ni wengi sana kipindi hicho.
 
uislamu upo karibia miaka 1000 pwani yetu na sehemu nyinginezo, hivi kipi haswa kimeletwa na uislamu kwa maana ya civilization na maendeleo ya jamii? hata tu mazao labda kuna zao gani ambalo lililetwa na uiaslamu hapa kwetu ?
USHIRIKINA...
 
Mimi ni atheist mtu nisiyeamini katika dini wala Mungu.

Na kwa sababu hii, labda ninaweza kuwa mtu mzuri sana wa kujibu swali hili bila kasumba ya kutetea dini.

Uislamu umeleta mengi mazuri na mabaya, lakini moja kubwa zuri Uislamu umeleta utamaduni wa kusoma na kuandika.

Kuna watu wengi wa Afrika Mashariki walijua kusoma na kuandika kwa kupitia Uislamu. Watu walifikia muda mpaka kuandika Kiswahili kwa maandishi ya Kiarabu.

Hivyo, kujibu swali lako, Uislamu ulileta utamaduni wa kusoma na kuandika huku kwetu ambako hatukuwa na utamaduni wa maandishi.
Kama Africa Mashariki ni pamoja na Ethiopia na Eritrea utamaduni wa kusoma na kuandika ulikuwepo kabla ya ujio wa waarabu na Uislamu.
 
Mnyonge mnyongeni, lakini mchango wa maneno ya kireno ni kidogo sana mchango wa Lugha ya Kiarabu ni mkubwa.

Neno KISWAHILI pia limetokana na neno la Kiarabu SAHEL au SAHIL.

Hauwezi kuitaja Historia ya Pwani ya Afrika ya mashariki bila kutaja mchango wa Waarabu na Waisilamu.
Logic ipo hivi, sio kweli wao wamesababisha kuzaliwa kwa kiswahili, Kuzaliwa maanake kitu hakikupata kuwepo kabla.

Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wageni waarabu, wareno, waajemi, Wapersi ambao walikuja Afrika mashariki.

Walipokuja walikuta kiswahili kikiwepo kupitia dialects Lahaja mbalimbali

1.Kipate
2.Kipemba
3.Kihamidu
4.Kitumbatu
5.Kimshovi
6.Kimombasa
7.Kiunguja
8.Kingazija

Hivyo ni viswahili vilivyokuwepo, vilichukua maneno toka kiarabu,kireno, kiajemi,japokuwa kiarabu kina maneno mengi zaidi kulinganisha na lugha nyingine.

Katika ukuaji wa lugha yoyote duniani ni pamoja na njia ya kuchukua maneno baadhi Toka lugha nyingine.

Kwahiyo waislamu wa mashariki ya kati na mashariki ya mbali walipokuja kwenye upwa wa Afrika walikuta waswahili Saheli.

KUSEMA WAO WALISABABISHA KISWAHILI KIZALIWE NI UONGO

Soma ,fanya utafiti wa wanazuoni hasa Shihabudin Shihaghadin
 
Lugha ya kiswahili ilikuwepo,nsoma historia ya lugha kiswahili.

Kulikuwa na Lahaja za Kiunguja,Kipemba, kimombasa, kitumbatu, kipate, ni Lahaja za kiswahili yaan Dialects, Lahaja hizo zilichukua maneno toka kiarabu, lakini pia kihindi, kireno,kiajemi!!

Kiarabu kama kilivyo kireno kilichangia maneno kwenye kiswahili.

Mvinyo-toka Kireno
Leso-toka kireno
Bima-toka Kiajemi
Salaam-toka kiarabu
Shukran -toka kiarabu.

Kwahiyo Kiswahili haikuletwa na waarabu/uislamu, kiswahili ni lugha Moja , na kiarabu ni lugha nyingine,

Havifanani na kiswahili katika mfumo wa sarufi muundo, wala maandishi yaani, silabi, irabu na konsonanti.

Kama una nia ya kuelewa nadhani utaelewa!!!
Unavyoandika kitu humu inabidi uwe na uelewa wa kutosha utachekesha ndugu yangu,kuna mabingwa wa Lugha humu ndani usijione kama uko kijiweni unazungumza na watu unaowajua elimu zao,kiarabu kina asilimia nisema 40 katika maneno ya kiswahili,mimi nimesoma kiarabu,na kileno ndiyo Lugha yangu,aliyekwambia Lesso ni neno la kiarabu nani?Voçe no stà boa de cabeça labda neno ninalojua linafanana na kireno ni Meza peke yake,hiyo lesso inatwa lesenho
 
Miti yote maarufu ya matunda ililetwa na waislamu pamoja na mazoo ya biashara.Ndio maana hiyo miti inaonekana sehemu za mwanzo kustaarabika na zilizokaliwa na waislamu.
Kumbuka kabla ya kuja wazungu waislamu pekee ndio waliokuwa wasafiri kuizunguka dunia.
Swali lako lina majibu tele humu humu pamoja na hivyo ni bora upewe utangulizi kidogo kwani umemaliza shule mwaka jana.
Sip kweli, mazao mengi kama mihogo, mahindi, mchele na matunda kama mananasi, machungwa n.k yaliletwa Africa na Wazungu hasa Wareno.
 
Unavyoandika kitu humu inabidi uwe na uelewa wa kutosha utachekesha ndugu yangu,kuna mabingwa wa Lugha humu ndani usijione kama uko kijiweni unazungumza na watu unaowajua elimu zao,kiarabu kina asilimia nisema 40 katika maneno ya kiswahili,mimi nimesoma kiarabu,na kileno ndiyo Lugha yangu,aliyekwambia Lesso ni neno la kiarabu nani?Voçe no stà boa de cabeça labda neno ninalojua linafanana na kireno ni Meza peke yake,hiyo lesso inatwa lesenho
Punguza jazba we POPOMA,Tafiti zinajibiwa kwa tafiti, mimi sijajitangaza kwamba mimi ni bingwa, ila wewe nakuona huna hoja, zaidi ya mihemko!!

Kabla ya kukosoa uwe unasoma vizuri!! Sijawahi kusema wala kuandika neno leso limetokana na kiarabu, nimeandika ni kireno, Nakupa kiambata bcha nilivyoandika.

Kusoma kwako au UMAHAMUMA wako haubadili ukweli kuwa kiswahili hakikuletwa Hakikuzaliwa na WAARABU, wala Uislamu, Bali kiarabu kimechangia maneno kama lugha nyingine, huo ndo ukweli mchungu.

Na mambo haya nayojibia ni kadiri ya rejea za wanazuoni, ukitaka nenda hata chuo chenu Cha KIISLAMU Muslin University College Morogoro, Idara ya Kiswahili utapata majibu hayahaya.

Namna nyingine malizia futuru tusubiri daku 🤣🤣🤣
 
Attachments

  • Screenshot_20250328-193916.jpg
    Screenshot_20250328-193916.jpg
    50.5 KB · Views: 18
Back
Top Bottom