Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Ni dhahiri sasa kwa kila anayeifuatilia Kesi ya ugaidi ya kina Mbowe, ameshabaini kuwa hiyo Kesi ni ya michongo na mashahidi wanaoletwa hapo mahakamani pia ni wa michongo!
Hivi unawatuhumu watu kwa ugaidi, halafu kila shahidi anayetoa ushahidi hapo mahakamani anaonekana kuwa amepangiwa ya kusema Ili awatie hatiani akina Mbowe?
Inafahamika wazi kuwa Ili Mahakama iwatie hatiani watuhumiwa, ni lazima upatikane ushahidi usio na shaka yoyote Ili watuhumiwa wahukumiwe kwenda jela.
Kwa mujibu wa ushahidi uliokwishatolewa hadi hivi sasa, hakuna ushahidi wowote wa kuwatia hatiani akina Mbowe, bali ni kuendelea kuwatesa kwa kuendelea kuwaweka mahabusu kina Mbowe kwa kipindi kirefu.
Hivi unawezaje kuwaita watu watuhumiwa wa ugaidi wa kulipua vituko vya mafuta, Ili Hali ushahidi uliotolewa hadi hivi sasa, hauonyeshi sehemu yoyote kuwa watuhumiwa hao walipanga njama za kulipua vituo hivyo vya mafuta?
Unawezaje kuwatuhumu watu kwa ugaidi, huku ukiieleza Mahakama, kuwa eti mtuhumiwa wa kwanza Mbowe, alifadhili ugaidi huo kwa kumtumia pesa mtuhumiwa mwingine shilingi elfu 80 tu?
Unawezaje kuwatuhumu watuhumiwa kuwa walipanga kumuua Sabaya, wakati mashahidi wenu wakidai kuwa hakuna sehemu yoyote Kati ya sms walizozi-hack, iliyomtaja Sabaya kutaka kuuawa?
This must be a joke of the year 😁
Kwa wakuu wa Serikali, akiwemo Rais Samia na IGP Sirro kuutangazia Ulimwengu kuwa wamemkamata Mbowe, wakiwa na ushahidi usio na shaka yoyote kuwa Mbowe alipanga njama na watuhumiwa wenzake kufanya ugaidi wa kulipua vituo vya mafuta na kupanga magogo Barabarani kwa lengo la kutaka nchi yetu isitawalike
Tufike mahala ambapo Mahakama zetu zisimuone Rais Samia kama mungu- mtu na zitambue kuwa yeye ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote, ambaye anaweza kukosea kwa matamshi yake na matendo yake na zihukumu kwa Haki kwa kuifuta Kesi hiyo ya ugaidi ya akina Mbowe, ambayo imeliletea aibu kubwa Sana Duniani kwa watawala wetu kuweza kuwabambikia Kesi kubwa ya ugaidi