Hivi ni Somo la Historia litafundishwa rasmi kwa Kiswahili au kutakuwa na masomo mawili ya Historia huku Somo la Sasa likibaki Kama kawaida?

Kuna haja ya kuwa na taasisi imara na sio kufata hisia za mtu mmoja, mbona marekani walimnyoosha trump. Kufata matakwa ya mtu badala vision na future ya taifa ni hatari
Taasisi imara zitapatikanaje bila kuwa na watu wenye misismamo juu ya kile wanachokiamini ?
 
Elimu inaendelea kuchezewa... Rais mwingine atakaye kuja kufuta hii mitaala.... Nakutoa maagizo mengine
Yani kila Raisi anakuja na Mambo yake kichwani kwanini kusiwe na malengo ya kitaifa Raisi anapoishia mwingine anaendeleza sasa kila mtu kuja na hisia na maono yake badala ya national vision ni hatari. Maana aliyetoa hilo wazo hajui kuwa watu tumesoma Mambo ya nchi kwenye history and social science
 
Taasisi imara zitapatikanaje bila kuwa na watu wenye misismamo juu ya kile wanachokiamini ?
Ndo hapo walioanzisha hili taifa walisahau maana walikipa chsma mamlaka na mwenyekiti nguvu kuliko taasisi. Taasisi zikiwa imara zinabana ukengeufu wa viongozi
 
Naam masomo yatakuwa mawili, la mwanzo litabaki kama lilivyo na hili jipya litaitwa Historia Tanzania na ndilo litakalo fundishwa kwa kiswahili na litasheheni historia yetu tu kama Taifa.
Na vp huo mtaala washauandaa tayari?
 
Halijafutwa kama nilivyoeleza, lipo pale pale ila lile limebeba mambo mengi ya mataifa tofauti duniani.
Hili la sasa ni kwa ajili ya kujifunza historia yetu kabila mpaka kabila, mazingira yetu, asili yetu na yote ambayo yalipotea bila kufundishwa popote.
Sasa kwann wasinge rekebisha somo la history na kuliongezea content za historia ya Tz?

Daah yani mwanafunzi wa PCB anaongezewa somo la historia ya Tz, kwann hiyo historia ya Tz isingewekwa kwenye somo la GS?
 
Ndo hapo walioanzisha hili taifa walisahau maana walikipa chsma mamlaka na mwenyekiti nguvu kuliko taasisi. Taasisi zikiwa imara zinabana ukengeufu wa viongozi
Mimi naamini watanzania ndiyo wenye matatizo zaidi kuliko hata taasisi zenyewe.

Watanzania hatuna tunachokiamini na hatuna tunachosimamia.

Kifupi watanzania ni wanafiki tu.
 
Yani kila Raisi anakuja na Mambo yake kichwani kwanini kusiwe na malengo ya kitaifa Raisi anapoishia mwingine anaendeleza sasa kila mtu kuja na hisia na maono yake badala ya national vision ni hatari. Maana aliyetoa hilo wazo hajui kuwa watu tumesoma Mambo ya nchi kwenye history and social science
Anachokitaka jiwe kwenye hili somo ni yeye na ccm kujaza content ya somo lote.
A pure sign of a dictator.

Time will tell.
 
Mimi naamini watanzania ndiyo wenye matatizo zaidi kuliko hata taasisi zenyewe.

Watanzania hatuna tunachokiamini na hatuna tunachosimamia.

Kifupi watanzania ni wanafiki tu.
Sasa watanzania watafanya nini wakati wenye power ndo wanaamua, ka madudu ya uchaguzi yalifanyika bila aibu Raia wangefanyaje na hawana jeshi. Nikuomba tu kupata viongozi wenye akili kutoka kwenye hii jamii iliyokuwa polluted.
Imagine enzi za mulugo walifuta division zero na kuja na division five eti
 
Anachokitaka jiwe kwenye hili somo ni yeye na ccm kujaza content ya somo lote.
A pure sign of a dictator.

Time will tell.
Labda wanataka kurudisha Mambo ya ccm Kama zamani ilikuwa lazima usome Mambo ya ccm kusifia fikra za mwenyekiti zidumu milele
 
Anachokitaka jiwe ni yeye kusomwa kwenye hiyo historia kama alama ya nchi.

Jiwe ni mpuuzi sana
 
Sasa kwann wasinge rekebisha somo la history na kuliongezea content za historia ya Tz?

Daah yani mwanafunzi wa PCB anaongezewa somo la historia ya Tz, kwann hiyo historia ya Tz isingewekwa kwenye somo la GS?
Mkuu somo la historia la sasa lina content zote muhimu za historia ya Tanzania, na waalimu wabobezi wanasema liko poa kabisa. Kama kuna kasoro au maboresho basi hilo ni suala la wadau wa elimu kupendekeza, na sio presha za wanasiasa.

Pili, historia ya Tanzania inatajwa kwenye somo la Historia, Maarifa ya jamii, Civics na somo la Kiswahili. Kwa sasa Rais na Waziri wake wa Elimu wanapanga kuleta somo jipya la Historia ya Tanzania (kwa kiswahili)!!

Ni upuuzi mpya.
 
Serikali inataka sasa wazazi waanze kupelela watoto Kenya kusoma Kama zamani. Nikiwa form one tulianza kusoma physics with chemistry
Aliyeleta huo ufala alikuwa ni Mkenya mmoja akiitwa Mungai kama sikosei. Aliunganisha masomo kibao na kufuta mengine. Yaani wizara muhimu pengine kuliko zote imegeuzwa kuwa shamba la bibi. Kila waziri anayekuja anakuja na lake. Akaja Kawambwa na naibu wake bomu aliyetoa kali kwenye kongamano huko Afrika Kusini kwa kudai eti Tanzania is a union of Tanganyika and Zimbabwe. Alikuwa akiitwa Mgulu nadhani.

Mfumo mzima wa hii elimu uchwara unatakiwa kufumuliwa na hili linapaswa kushirikisha wadau wote muhimu - wazazi, walimu, wanafunzi, wataalamu wa mitaala, wachumi na hata sisi watu wa mitaani tuliokomea la saba. Hii kukurupuka tu kwa maagizo ya wanasiasa hatutafika po pote.
 
Naiwaza hapa combination ya historia ya tanzania , geography na kiswahili namna itakavyotoboa kimataifa!!
 
Aliyeleta huo ufala alikuwa ni Mkenya mmoja akiitwa Mungai kama sikosei. Aliunganisha masomo kibao na kufuta mengine. Yaani wizara muhimu pengine kuliko zote imegeuzwa kuwa shamba la bibi. Kila waziri anayekuja anakuja na lake. Akaja Kawambwa na naibu wake bomu aliyetoa kali kwenye kongamano huko Afrika Kusini kwa kudai eti Tanzania is a union of Tanganyika and Zimbabwe. Alikuwa akiitwa Mgulu nadhani.

Mfumo mzima wa hii elimu uchwara unatakiwa kufumuliwa na hili linapaswa kushirikisha wadau wote muhimu - wazazi, walimu, wanafunzi, wataalamu wa mitaala, wachumi na hata sisi watu wa mitaani tuliokomea la saba. Hii kukurupuka tu kwa maagizo ya wanasiasa hatutafika po pote.
Mulugo na sasa hivi karudi tena bungeni
 
Back
Top Bottom