Hivi ni Somo la Historia litafundishwa rasmi kwa Kiswahili au kutakuwa na masomo mawili ya Historia huku Somo la Sasa likibaki Kama kawaida?

Hiki ndicho anachokitaka Jiwe.

Hitler alifanya kitabu cha Mein Kempfr kisomwe mashuleni na itikadi za kinazi na hili la jiwe nalo litajaa mambo ya ccm na jiwe.

Naupa muda nafasi kuona huo ushenzi.

Naumia sana kuishi ujana wangu chini ya utawala wa jiwe.
Bado miaka minne tu vumilia kwa sababu hakuna namna. Sisi wahenga tulioanzia kwa Nyerere tupo tunawaangalia tu. JPM naye atapita na atakuja mwingine naye aje apambane.

Ila hawa jamaa wana madaraka makubwa mno na bila kuwa na katiba mpya kama ile ya Warioba hakuna kitakachobadilika.
 
Magufuli haondoki leo sababu kubwa ccm imechoka kufanya siasa sasa hivi kinapata ahueni juu ya uwepo wake yeye.

Bila udikteta wake kingekuwa kinamalizikia tu.
 
Bado miaka minne tu vumilia kwa sababu hakuna namna. Sisi wahenga tulioanzia kwa Nyerere tupo tunawaangalia tu. JPM naye atapita na atakuja mwingine naye aje apambane.

Ila hawa jamaa wana madaraka makubwa mno na bila kuwa na katiba mpya kama ile ya Warioba hakuna kitakachobadilika.
Ni ngumu sana kuvumilia upuuzi kwa muongo mzima.
 
Uwekezaji nao inategemea mkuu, jamaa kapanda miti yake ya mbao huko Mafinga umekomaa baada ya miaka dahari kavuna kauza kapata milioni zaidi ya 300. Mara paaa fwedha imedakwa yote huko kwa akaunti.
Khaa kwanini?
 
Kuna haja ya kuwa na taasisi imara na sio kufata hisia za mtu mmoja, mbona marekani walimnyoosha Trump. Kufata matakwa ya mtu badala vision na future ya taifa ni hatari.
Kwa hii katiba iliyompa raisi mamlaka makubwa kiasi cha kujiona mungu hiyo habari ya urais kuwa taasisi sahau.
 
Kwa hii katiba iliyompa raisi mamlaka makubwa kiasi cha kujiona mungu hiyo habari ya urais kuwa taasisi sahau.
Katiba yetu mbovu Nyerere walicopy katiba za kifalme ambako huko waliko copy hawaitumii tena
 
Aliyeleta huo ufala alikuwa ni Mkenya mmoja akiitwa Mungai kama sikosei. Aliunganisha masomo kibao na kufuta mengine. Yaani wizara muhimu pengine kuliko zote imegeuzwa kuwa shamba la bibi. Kila waziri anayekuja anakuja na lake. Akaja Kawambwa na naibu wake bomu aliyetoa kali kwenye kongamano huko Afrika Kusini kwa kudai eti Tanzania is a union of Tanganyika and Zimbabwe. Alikuwa akiitwa Mgulu nadhani.

Mfumo mzima wa hii elimu uchwara unatakiwa kufumuliwa na hili linapaswa kushirikisha wadau wote muhimu - wazazi, walimu, wanafunzi, wataalamu wa mitaala, wachumi na hata sisi watu wa mitaani tuliokomea la saba. Hii kukurupuka tu kwa maagizo ya wanasiasa hatutafika po pote.
Philip Mulugo
 
Mulugo na sasa hivi karudi tena bungeni
Philip Mulugo
MHE.MULUGO.jpg
 
Aliyeleta huo ufala alikuwa ni Mkenya mmoja akiitwa Mungai kama sikosei. Aliunganisha masomo kibao na kufuta mengine. Yaani wizara muhimu pengine kuliko zote imegeuzwa kuwa shamba la bibi. Kila waziri anayekuja anakuja na lake. Akaja Kawambwa na naibu wake bomu aliyetoa kali kwenye kongamano huko Afrika Kusini kwa kudai eti Tanzania is a union of Tanganyika and Zimbabwe. Alikuwa akiitwa Mgulu nadhani.

Mfumo mzima wa hii elimu uchwara unatakiwa kufumuliwa na hili linapaswa kushirikisha wadau wote muhimu - wazazi, walimu, wanafunzi, wataalamu wa mitaala, wachumi na hata sisi watu wa mitaani tuliokomea la saba. Hii kukurupuka tu kwa maagizo ya wanasiasa hatutafika po pote.
Hii wizara ya elimu ni nyeti Sana sijui kwanini wahuni wahuni ndo huteuliwa Mimi nikiwa form one tulianza na hyo physics with chemistry Hadi definition yake in short ilikuwa vituko Ila after three months wakarudisha normal Ila ndo wakafuta somo la agriculture mpaka leo ambapo agriculture imeajiri asilimia 80% ya watanzania si Bora wangerudisha hilo somo kuliko history ambayo tayari ipo.
Akaja mulugo naye na big result wakaongeza kutoka division form na zero, hyo zero ikafutwa ikawa eti division five.
Mimi naona viongozi wengi wa wizara ya elimu ni mamluki wanaoharibu elimu ya taifa letu, na Ili taifa lisiendelee chezea elimu, sasa na mama ndalichako anafuata nyayo za Mungai na mulugo kuharibu hii elimu ya taifa. Kweli kuwa prof wa madesa na ku deliver Mambo ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Anachokitaka jiwe ni yeye kusomwa kwenye hiyo historia kama alama ya nchi.

Jiwe ni mpuuzi sana
Hii nchi yetu ujue yeye kasoma chemistry sasa anafikiri watoto hawasomi hayo wakati historia ya taifa ipo Hadi kwenye general studies. Waache kuongeza masomo yenye same content kwa kurudia rudia na kuchosha watoto, si bora wangewekeza veta, na pyschical studies aisee
 
Dunia yote sasa hivi wanaangalia miaka 20, 50, 100 huko mbele itakuwaje. Wanatabiri kuwa Artificial Intelligence (AI) itakuwa ime-dominate maisha ya mwanadamu karibu katika kila nyanja; na kazi nyingi zitakuwa automated. Karibu kila mtu anachacharika kuimarisha mitaala ya Kompyuta, Hisabati na Sayansi ili asiachwe nyuma. Sisi ndiyo kwanza tunaanzisha mitaala mipya ambayo ni redundant kufundishana Historia ambayo tayari ipo na inafundishwa vizuri tu. Akina Mangungo, Mkwawa na Kinjeketile Ngwale, Mangi Sina, akina Mirambo na Nyerere si tunawasoma vizuri tu jamani?. Kama ina mapungufu mtaala wake ungefanyiwa marekebisho tu kwa kuongezewa topics mpya hapa na pale mambo yakasonga mbele. Ingekuwa somo kama Agriculture ndiyo linafanywa kuwa la lazima (tena kwa vitendo) angalau ningeelewa kidogo...
 
Mkuu somo la historia la sasa lina content zote muhimu za historia ya Tanzania, na waalimu wabobezi wanasema liko poa kabisa. Kama kuna kasoro au maboresho basi hilo ni suala la wadau wa elimu kupendekeza, na sio presha za wanasiasa.

Pili, historia ya Tanzania inatajwa kwenye somo la Historia, Maarifa ya jamii, Civics na somo la Kiswahili. Kwa sasa Rais na Waziri wake wa Elimu wanapanga kuleta somo jipya la Historia ya Tanzania (kwa kiswahili)!!

Ni upuuzi mpya.

Hivi waziri alishindwa kujadiliana na Rais kuhusu hili?
 
Back
Top Bottom